Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Huyu mzee ni mpuuzi sana...[emoji16] [emoji16]
Yaani kila anapo taka kupaza sauti, ni lazima aongee na watu wa media...[emoji55] [emoji55]
Na mbaya zaidi ni kwamba anajiskaha kama hao wanao muhoji ni watafuta fursa. Yaani wanatumia jina la Diamond na kumuhoji baba yake, kisha wanaanika kwenye public ili wapate pesa....[emoji57] [emoji57]
 
Mzazi ni mzazi tu no matter what. Hatujui kipi hasa huyu mzee alimfanyia Diamond lakini kiubinadamu nafikiri imetosha sasa ameanza kulia siku nyingi sana mzee wa watu! Angemsamehe tu, amuwezeshe Hata kidogo then aendelee na mambo yake! Nafikiri Hata mama Diamond ni kikwazo kwa Diamond kumsamehe mzee Wake, akifikiria jinsi mama alivyopambana kwa ajili yake anashindwa kwenda kinyume na mama yake!
 
Watajaza wenyewe na maisha yao. Ila niseme tu huyo baba awache kulalamika kwenye vyombo vya habari sababu suluhu haipatikani huko.
Afanye nini sasa kama hakuna altrnative, ogopa sana una matatizo then huna alternative unaweza ukafa kwa uchungu tu.
 
Diamond ni mjinga sanaa,asichokijua kuwa mayeso ya mzee wake ndiyo yaliyompa hasira hadi akapambana hadi kufikia Hapo alipo kwanza angetakiwa amshukuru sanaa mzee .huenda baba asingefanya aliyomfanyia basi angekuwa bado kitaa anapambana na hali hii mbovu mbovu.
 
Akifanya mahojiano na gazeti mwananchi baba mzazi wa msanii diamond platnumz ambemuomba mwanae angalau amkatie bima ya afya kwani Hali yake kwa Sasa sio nzuri.
Ilinichukua muda kumshawishi na baadaye kufanya mahojiano na Abdul Juma Isack ambaye ni baba wa msanii wa maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.
Ungeweza kukata tamaa ya kuendelea kumshawishi kwa sababu ana hoja nyingi na pengine nzito.
“Sioni mabadiliko kwangu,” anasema baba huyo mwenye umri wa miaka 52 wakati akieleza sababu za kukataa kufanya mahojiano.
“Tangu nianze kuhojiwa, nilikuwa nikiamini kuwa ningeweza kubadili msimamo wa mwanangu anayetajwa kuwa msanii tajiri namba moja Tanzania.
“Badala yake naonekana kama nalilia kusaidiwa na mtoto wangu. Pamoja na kuwa na mtoto maarufu ndani na nje ya nchi, maisha yangu ndio kama hivi unavyoyaona. Naishi Magomeni Kagera na nyumba yangu ya kawaida tu, ambayo naamini hata siku Diamond akikwama kimaisha atakuja kuishi kwa kuwa hapa ni kwao, japokuwa simuombei hilo.”
Abdul anasema kwa muda mrefu Diamond amekuwa hafanyi mawasiliano naye na hajui sababu .
“Najiuliza ni nini kikubwa namna hiyo nilichomkosea?” anahoji baba huyo.
“Ninatamani siku moja nikutanishwe katika mahojiano na Diamond na mama yake ili kila mmoja atoe alilonalo moyoni.
“Huyu mtoto kanipa majina mengi kutokana na yanayoongelewa mtaani kwamba nilimtelekeza, wakati hakuna ukweli wowote. Mimi niliachana na mama yake wakati akiwa kidato cha kwanza.
Kwa umri hu alikuwa anajielewa na anajua sababu za kuachana kwetu. Kama kuna jingine wanalolijua wao kwamba nimewakosea, basi tuhojiwe hata mbele za watu ili lifahamike na kuyamaliza kuliko hiki wanachofanya kwangu.
“Kasababisha kila kona ninayopita nanyooshewa vidole kuwa niliwatosa. Ifike mahali haya mambo tuyaweke sawa kwa kuwa naumia sana, hawajui tu. Si kwamba, labda ni kwa kutaka msaada wao, hapana. Bali kila mtu awe ameitakasa nafsi yake na kuondokana na vinyongo.”
Baba huyo wa Diamond anasema hata mawasiliano na mzazi mwenzake ni pale anapojisikia.
“Tena wakati mwingine na maneno ya karaha, lakini ana afadhali kuliko mtoto ambaye mara ya mwisho tuliwasiliana akiwa na Wema Sepetu ambaye alikuwa akija naye hapa mara kwa mara kunisalimia,” anasema.
Kwa sasa maisha si mazuri
Abdul anajihusisha na biashara ya viatu. Huchukua viatu kwa malikauli katika soko la Karume na kuvipeleka kwa wateja wake mahali walipo.
“Lakini maisha kwa sasa si mazuri kwa kuwa nasumbuliwa na tatizo la miguu. Inanifanya wakati mwingine nishindwe kutembea muda mrefu,” anasema mzazi huyo.
“Kama unavyoniona miguu inaniuma na wakati mwingine nashindwa kuinuka hata kitandani.
“Naona ni wakati sasa na mimi kuwa na eneo la kufanya biashara hii, lakini ndio hivyo uwezo, walau ningekuwa na gari ningeweza kuzunguka nalo hata kwa kuendeshwa ili nisiwapoteze wateja wangu, lakini sina namna.”
Anasema hata uwezi wa kugharimia matibabu, hana. “Labda ningekuwa na bima ya afya ingekuwa msaada kwangu lakini ndio hivyo sina,” anasema.
Apata msaada mtandaoni
Hata hivyo, msaada wake mkubwa uko kwa mtoto wake wa hiari anayeishi London, Uingereza anayeitwa Zubeda. Walijuana na mtoto huyo katika mitandao ya kijamii baada ya kuona mahojiano yake akielezea maisha anayoishi.

Mwananchi sourceView attachment 968793
kavaa cheni na kujichora tatoo.....
 
Watajaza wenyewe na maisha yao. Ila niseme tu huyo baba awache kulalamika kwenye vyombo vya habari sababu suluhu haipatikani huko.
Siti yako inakusubiri kule kitwe ya mbele kabisa uone burudani
 
Huyu mzee ni mpuuzi sana...[emoji16] [emoji16]
Yaani kila anapo taka kupaza sauti, ni lazima aongee na watu wa media...[emoji55] [emoji55]
Na mbaya zaidi ni kwamba anajiskaha kama hao wanao muhoji ni watafuta fursa. Yaani wanatumia jina la Diamond na kumuhoji baba yake, kisha wanaanika kwenye public ili wapate pesa....[emoji57] [emoji57]
Fikili nje ya Box basi, bila us ku publish kwenye public angempata hata uyo zubeda anayemwita mwanaye wa iyari.

Wanadamu tukiwa kwenye furaha tunahisi kama teyari tupo peponi dunia haipo rahisi boss.

Ukitaka kujua nenda jukwaa la kazi na tenda utayajua maisha.
 
Asichojua Diamond mzee wake akifa ataandamwa sana, na itakuwa ni kama laana kwake. Namsihi achukue hatua mapema kabla mambo hayajaharibika. Misaada anayotoa kilasiku haina maana kama ameshindwa kumsaidia babayake
 
Huyu mzee ni mpuuzi sana...[emoji16] [emoji16]
Yaani kila anapo taka kupaza sauti, ni lazima aongee na watu wa media...[emoji55] [emoji55]
Na mbaya zaidi ni kwamba anajiskaha kama hao wanao muhoji ni watafuta fursa. Yaani wanatumia jina la Diamond na kumuhoji baba yake, kisha wanaanika kwenye public ili wapate pesa....[emoji57] [emoji57]
Ficha upumbavu wako mkuu..
 
Akianza kuwa mahututi ndio watajifanya wanampeleka India. Ila dingi nae anafeli si achukulie Kama Hana mtoto tu
Unajua mjomba...kuna kipindi una kaza kama mwanaume halafu unapiga moyo konde na kujiuliza..."huu ukauzu unaweza niua"...hapo ndio hatua aliyofikia baba Chibu...anaona kwa nini aishi kwa mateso wkt watoto anao....
Ila Chibu kama anaakili na kujali.....arudishe moyo tuu....anafanya mengi sana ya kumpatia thawabu kwa muumba wake...lakini hili la mzazi wake aliangalie kwa mapana yakee....hii ndio thawabu namba moja
 
Akifanya mahojiano na gazeti mwananchi baba mzazi wa msanii diamond platnumz ambemuomba mwanae angalau amkatie bima ya afya kwani Hali yake kwa Sasa sio nzuri.
Ilinichukua muda kumshawishi na baadaye kufanya mahojiano na Abdul Juma Isack ambaye ni baba wa msanii wa maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.
Ungeweza kukata tamaa ya kuendelea kumshawishi kwa sababu ana hoja nyingi na pengine nzito.
“Sioni mabadiliko kwangu,” anasema baba huyo mwenye umri wa miaka 52 wakati akieleza sababu za kukataa kufanya mahojiano.
“Tangu nianze kuhojiwa, nilikuwa nikiamini kuwa ningeweza kubadili msimamo wa mwanangu anayetajwa kuwa msanii tajiri namba moja Tanzania.
“Badala yake naonekana kama nalilia kusaidiwa na mtoto wangu. Pamoja na kuwa na mtoto maarufu ndani na nje ya nchi, maisha yangu ndio kama hivi unavyoyaona. Naishi Magomeni Kagera na nyumba yangu ya kawaida tu, ambayo naamini hata siku Diamond akikwama kimaisha atakuja kuishi kwa kuwa hapa ni kwao, japokuwa simuombei hilo.”
Abdul anasema kwa muda mrefu Diamond amekuwa hafanyi mawasiliano naye na hajui sababu .
“Najiuliza ni nini kikubwa namna hiyo nilichomkosea?” anahoji baba huyo.
“Ninatamani siku moja nikutanishwe katika mahojiano na Diamond na mama yake ili kila mmoja atoe alilonalo moyoni.
“Huyu mtoto kanipa majina mengi kutokana na yanayoongelewa mtaani kwamba nilimtelekeza, wakati hakuna ukweli wowote. Mimi niliachana na mama yake wakati akiwa kidato cha kwanza.
Kwa umri hu alikuwa anajielewa na anajua sababu za kuachana kwetu. Kama kuna jingine wanalolijua wao kwamba nimewakosea, basi tuhojiwe hata mbele za watu ili lifahamike na kuyamaliza kuliko hiki wanachofanya kwangu.
“Kasababisha kila kona ninayopita nanyooshewa vidole kuwa niliwatosa. Ifike mahali haya mambo tuyaweke sawa kwa kuwa naumia sana, hawajui tu. Si kwamba, labda ni kwa kutaka msaada wao, hapana. Bali kila mtu awe ameitakasa nafsi yake na kuondokana na vinyongo.”
Baba huyo wa Diamond anasema hata mawasiliano na mzazi mwenzake ni pale anapojisikia.
“Tena wakati mwingine na maneno ya karaha, lakini ana afadhali kuliko mtoto ambaye mara ya mwisho tuliwasiliana akiwa na Wema Sepetu ambaye alikuwa akija naye hapa mara kwa mara kunisalimia,” anasema.
Kwa sasa maisha si mazuri
Abdul anajihusisha na biashara ya viatu. Huchukua viatu kwa malikauli katika soko la Karume na kuvipeleka kwa wateja wake mahali walipo.
“Lakini maisha kwa sasa si mazuri kwa kuwa nasumbuliwa na tatizo la miguu. Inanifanya wakati mwingine nishindwe kutembea muda mrefu,” anasema mzazi huyo.
“Kama unavyoniona miguu inaniuma na wakati mwingine nashindwa kuinuka hata kitandani.
“Naona ni wakati sasa na mimi kuwa na eneo la kufanya biashara hii, lakini ndio hivyo uwezo, walau ningekuwa na gari ningeweza kuzunguka nalo hata kwa kuendeshwa ili nisiwapoteze wateja wangu, lakini sina namna.”
Anasema hata uwezi wa kugharimia matibabu, hana. “Labda ningekuwa na bima ya afya ingekuwa msaada kwangu lakini ndio hivyo sina,” anasema.
Apata msaada mtandaoni
Hata hivyo, msaada wake mkubwa uko kwa mtoto wake wa hiari anayeishi London, Uingereza anayeitwa Zubeda. Walijuana na mtoto huyo katika mitandao ya kijamii baada ya kuona mahojiano yake akielezea maisha anayoishi.

Mwananchi sourceView attachment 968793
Huyu mzee apambane tu na hali yake... Watu kama hawa wanakera sana..yaan hujui hata uchungu wa mwana ni nn... kaz yako ilikuwa kuweka mimba tu....akabeba mwingine,,akazaa kwa uchungu,,akalea kwa tabu...Leo analalamika lalamika hovyo...ajifunze kwanza mfyuuuu
 
Unajua mjomba...kuna kipindi una kaza kama mwanaume halafu unapiga moyo konde na kujiuliza..."huu ukauzu unaweza niua"...hapo ndio hatua aliyofikia baba Chibu...anaona kwa nini aishi kwa mateso wkt watoto anao....
Ila Chibu kama anaakili na kujali.....arudishe moyo tuu....anafanya mengi sana ya kumpatia thawabu kwa muumba wake...lakini hili la mzazi wake aliangalie kwa mapana yakee....hii ndio thawabu namba moja
Hapa wa kuwekwa sawa ni mama chibu. He has been brainwashed by her. Nachibu anasimamia Sana kauli za bimkubwa
 
Hili liwe funzo kwa madingi ambao wanakimba majukumu yao.....angeliambatana nao enzi za shida asingelipata shida nyakati hizi za mavuno.

Hapa anavuna mbegu ya chuki aliyoipanda miaka tele nyuma.
 
Back
Top Bottom