Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,629
- 34,199
Mimi nimezaliwa mpaka namaliza kidato cha sita simjui baba.Jamaa arudishe moyo tu amsamehe mtoa adhabu ni Mungu tu haina maana kutoa misaada kwa watu huku mtu wa karibu unamtupa
Chibu piga moyo konde msamehe mzee shukuru Mungu una uhai.
Nimesoma kwa shida kubwa sana, kwa kuhangaika sana, kwa uongo uongo na kusaidiwa na wapita njia.
Baada ya kuhitimu kidato cha sita nilikutana na "baba" nikajua labda kwa kuwa hakunilea, sasa atatimiza majukumu yake bila shida, kumbe nilijidanganya tu.
Nimehangaika "mnooo" nimeshinda njaa mpaka siku 4, nimenusulika kuzimia kwenye daladala kwa njaa hapa Dar wakati wa kufukuzia kazi ya ulinzi. Nimekunywa sana juisi za kwenye makopo yaliyotupwa barabarani, nimelala sana mitaani Dar.
Najua alichopitia Diamond na wala hata sioni kama anamkosea huyo mzee. Hana tatizo naye ila ni kuacha kila mtu aendelee na maisha yake kama ilivyokuwa tangu zamani. Tusifuatane fuatane kama ilivyokuwa zamani.