Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Jamaa arudishe moyo tu amsamehe mtoa adhabu ni Mungu tu haina maana kutoa misaada kwa watu huku mtu wa karibu unamtupa

Chibu piga moyo konde msamehe mzee shukuru Mungu una uhai.
Mimi nimezaliwa mpaka namaliza kidato cha sita simjui baba.

Nimesoma kwa shida kubwa sana, kwa kuhangaika sana, kwa uongo uongo na kusaidiwa na wapita njia.

Baada ya kuhitimu kidato cha sita nilikutana na "baba" nikajua labda kwa kuwa hakunilea, sasa atatimiza majukumu yake bila shida, kumbe nilijidanganya tu.

Nimehangaika "mnooo" nimeshinda njaa mpaka siku 4, nimenusulika kuzimia kwenye daladala kwa njaa hapa Dar wakati wa kufukuzia kazi ya ulinzi. Nimekunywa sana juisi za kwenye makopo yaliyotupwa barabarani, nimelala sana mitaani Dar.

Najua alichopitia Diamond na wala hata sioni kama anamkosea huyo mzee. Hana tatizo naye ila ni kuacha kila mtu aendelee na maisha yake kama ilivyokuwa tangu zamani. Tusifuatane fuatane kama ilivyokuwa zamani.
 
Basi kama baba aliamua kuwa sehemu ya maadui wa mwanae aendelee kuwa adui hivyohivyo yaani apambane na maisha yake.... kulialia kila siku usaidiwe ni umama,
binafsi sina huruma na madingi wa hivi.....hawa watu wanajisahau sana man!!
Kabisa mkuuu,unakuta dingi kipindi hicho mpunga wa kutosha anao,lakin anashindwa kukusaidia kwa chochote kile,yaaan kunakipindi unamkataaa moyoni kabisa,ila sasa hivi shilingi imebadirika unaanza kupuyanga
NB:KAMA UMEAMUA KUZAA MTOTO BASI MSAIDIE,LAKINI SIO UNAZAAA MTOTO HARAFU HUNA MCHANGO ILI HALI WEWE UPO VIZURI HAYA NDIO MADHARA YAKE
 
Mkuu umeongea point hapo si kwamba mond lazima amsamehe baba yake hapana tunaangalia ubinadamu tu kuna muda usitahie mema toka kwa mwanadamu tenda wema kisha nenda zako
 
Mtu amtagi Baba Dimond please apate ABC hapa kabla Dimond ajawaomba mod wafute hii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]haya maisha acha tu.

Niliyapitia, tukaja kuwa marafiki wakubwa, muda wake wa mwisho niliwajibika kwa kiwango changu. Bahati haikuwa upande wangu, alitangulia mbele ya haki. Tarehe 27 mwezi huu anafunga mwaka. Upendo wake umeniacha nimkumbuke na kumuombea kila mara.
 
Kwa hiyo mkuu na wewe ukifanikiwa mzee asikujuee...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna watu wanamshauri vibaya mzee wa Nasib,Mungu amsaidie akutane na mwanae kabla hakuja kuchwa.
 
Yaani kuzaa azae yeye kulea aachie wengine ??

Huyu mzee akaziwe liwe fundisho kwa wazee wajinga wajinga kama hawa.
 
Kusamehe mbona ashasamehewa.

Ila anacholazimisha kukipata huyo mzee nadhani ni zaidi ya msamaha.
Mzee anataka ukaribu na mwanae zile za baba na mwana kitu ambacho nadhani anaona hakifanyika
 
Me dingi alinizingua balaa mpaka kunikataa but this time ni marafiki balaa na namlea kuliko hata mama.

 
Wengi wetu humu hatutomuelewa dimondi[emoji23],lakini usiombe wanathaminiwa watoto wa kufikia huku baba yako anakuona huna maaana na uwezo anao
 
Ninyi mliolelewa na baba na mama zenu kama makinda ya ndege "MNATOA USHAURI WA KIPUMBAVU SANA na MNAONEKANA MNA AKILI NA MILA NYEUSI KABISA"

Yaani WEWE UZAE kulea ALEE MWINGINE ??!
 
Du nikikumbuka pemba st na abdu tunagonga viatu jua vumbi letu, we acha tu. Dogo mungu anakuona
 
Hili ni fundisho tosha kwetu sisi wa jinsia ya ME, "Tuwalee na kuwatunza wanetu bila shurti".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…