Baba Jitahidi kurudi nyumbani mapema wakati mwingine watoto wanakuhitaji sana

Baba Jitahidi kurudi nyumbani mapema wakati mwingine watoto wanakuhitaji sana

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Baba wengi wakati mwingine wanachelewa kurudi nyumbani kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo za kikazi.

Lakini Baba wengine akishahakikisha kila kitu ndani kipo basi ndo kamaliza hivo. Atakuwa anarudi usiku mnene wakati mwingine anaweza asionane na watoto wiki nzima na hajasafiri.

Baba ni yeye tu na marafiki, Marafiki wape muda na watoto wape muda.

Baba wengine hawawezi hata kuwapeleka watoto kwenye michezo hata siku moja. Hata kumtoa out mama mjengo pia hawezi.

Umuhimu wa Baba kurudi nyumbani. Kwanza watoto wanafurahi sana na hasa ukikaa nao kuwauliza maswali ya shuleni na kusaidia homework.

Pili watoto wanapenda kuona baba na mama wakiwa na furaha.

Tatu inasaidia kujenga ukaribu na familia.

Hitimisho
Baba wewe ni wa muhimu uwepo wako nyumbani huleta faraja kybwa sana. Punguza muda wa kukaa na marafiki kila siku wahi nyumbani ndiko amani ilipo.

Tunawapenda wababa ❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️
 
Kama nyumbani panalizisha yani wife yupo romantic mazingira yapo safi tutawai kulidi ila kama mwanamke ana gubu kila wakati mikwaluzano hapo kuludi nyumbani ni mida ya wanga.
😅😅😅😅
 
Hii muhimu sana.
Tukishamaliza kufanya homework tunacheza karata wote. Inaleta amani sana na furaha Kwa familia.

Shida Kuna wakati mnashindwa dhibiti visirani vyenu mtu unaona bora uchelewe kurudi au ikitokea umewahi upitilize chumbani tu.

Uanaume kazi sana, achilia mbali kuwa Baba.
 
Ukiona baba anachelewa kurudi nyumbani shida ipo kwa mama, vinginevyo kazi zimembananisha hana namna.

Kuna baadhi ya wanawake ni mnaongea mnafyatuka ova mmeza radio
 
Tuvumilie tu
 
Ukiona baba anachelewa kurudi nyumbani shida ipo kwa mama, vinginevyo kazi zimembananisha hana namna.

Kuna baadhi ya wanawake ni mnaongea mnafyatuka ova mmeza radio
Sasa mbona tunawamiss
 
Upo sahihi mama halisi,Baba yeyote mwenye kijitambua lazima awe na muda wa kuwa karibu na familia vinginevyo kuna shida mahali.
Hivi kwa maisha ya Daslam kweli kuna watu wanafurahia ndoa zao? Maana unakuta huyo Baba mida mibovu bado hajafika Nyumbani,mama nae ndio yupo huko huko barabarani kwenye mihangaiko yake watoto wameshalala wanaonana na wazazi mara Moja kwa wiki.
 
Back
Top Bottom