Baba kasema "Hakuna Akiba mbaya". Heri ya kuzaliwa Analyse

Baba kasema "Hakuna Akiba mbaya". Heri ya kuzaliwa Analyse

Analyse

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
17,637
Reaction score
47,413
Namshkuru Mwenyezi Mungu kwa kuniweka hai na salama mpaka siku hii ya leo (28th April).

Nimeamka asubuhi mida ya saa 12,nikakuta msg tatu zote toka kwa mpenzi wangu akinitakia heri katika hii siku ya leo. Nikareply then tukachat kidogo. Baada ya muda ikaingia msg toka kwa Mama, nae akinitakia heri ya siku yangu ya kuzaliwa. So far hao ndio watu pekee walioweza kunitafuta nje ya mitandao ya kijamii.

Baada ya kuoga, nikaamua kumpigia simu mzee wangu. Maongezi yalipoanza hadi kuisha, hakuzumgumzia lolote au kuonesha anajali siku yangu ya kuzaliwa. Ila nilivutiwa sana na maongezi yake, ndio maana nikaamua kushare na nyie hapa.

Baada ya salamu na story chache, aliniambia. "Unajua hii corona imekuwa tatizo sana, ila uwepo wake umeweka somo kubwa sana. Unajua imezoeleka kwamba, tunafanya kazi, na kuwekeza kwenye vyanzo tofauti tofauti vya mapato ili kujikwamua kiuchumi. Lakini toka ili gonjwa lije, limegusa uchumi wa kila mtu kwa namna moja au nyingine, na kama litaendelea, basi hata wenye vyanzo vingi nao watatetereka sana,kipindi ambacho wengine mpo hoi "

Wekeza kadri uwezavyo,ila ningependa kukukumbusha kwamba hakuna akiba mbaya. Ikitokea leo hii umepata tatizo la kiafya na hauwezi kufanya kazi,vyanzo vyako vya mapato vitakuokoa. Na ikitokea wewe ni mzima kiafya,ila vyanzo vyako vya mapato haviwezi kufanya kazi,akiba yako itakuokoa,jifunze kuweka akiba."

Maneno yake yalikuwa hayo. Yakafatwa na ukimya kidogo. Kisha tukaagana.

Naomba nirudie ndugu zangu. Hakuna Akiba Mbaya.

Heri ya kuzaliwa Analyse.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
1st to wish you HBD tuachane na hayo keki tunakatia wapi mkuu??
 
Uzi wa birthday wenye mafunzo japo kwa jinsi tulivyoususa ni dhahiri wengi wetu hatujawekeza na hatuna vyanzo vya mapato vya kutosha ambavyo baadae vinaeza tuokoa hivyo kila tukisoma tunaona giza tu hapa. 😀

Kheri ya kuzaliwa Mkuu.
 
Hivi Wadogo zangu ukhuty, Carleen na Lenie hivi tangia jana hamjauona huu uzi kweli. 🙈🙈 (Leo zamu yangu kuwachokoza)

Hebu mkuje mumuwish Mleta uzi kabisa mupokeepo na ujumbe. 😅💃
Jana sjui nlikua na pilika gani hadi sikuzurura sana humu, asante my dada Shadeeya ujumbe mzuri nmeuelewa vema kabisa.

Happy bday to you mkuu Analyse Mungu akujalie maisha mema yenye baraka tele.
 
Hivi Wadogo zangu ukhuty, Carleen na Lenie hivi tangia jana hamjauona huu uzi kweli. 🙈🙈 (Leo zamu yangu kuwachokoza)

Hebu mkuje mumuwish Mleta uzi kabisa mupokeepo na ujumbe. 😅💃
😂😂😂
Basii dadaangu mzuri Shadeeya hapo unaona 'umetuchokoodha' mwenyewe, basii wewe ni mpole sana! Nilivyoona 'uchokozi' nikajua nitakuta mpaka vyombo vimevunjika JF? Majukwaa yamevurugika kiasi kwamba nitaikuta love connect kule jukwaa la Intelijensia.??

Happy belated birthday mkuu Analyse simulizi ya maisha yako bado inaishi ndani yangu.! My love to Dad and your Son.!
Point is well noted.!!
 
Nashkuru mkuu.
Uzi wa birthday wenye mafunzo japo kwa jinsi tulivyoususa ni dhahiri wengi wetu hatujawekeza na hatuna vyanzo vya mapato vya kutosha ambavyo baadae vinaeza tuokoa hivyo kila tukisoma tunaona giza tu hapa. 😀

Kheri ya kuzaliwa Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom