GE2025 Baba Levo: Askari atakayewanyanyasa bodaboda na bajaji Kigoma Mjini atatafuta nyumba ya kwenda jimbo lingine

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Clayton Revocatus Chipando, maarufu kama Baba Levo, leo ameanza rasmi kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025-2030. Uzinduzi wa kampeni hizo ulifanyika katika Viwanja vya Mwanga Community Center, ambapo Baba Levo alikusanya umati mkubwa wa wakazi wa Kigoma.

Akizungumza mbele ya wananchi, Baba Levo alijikita katika kutoa sera na ahadi mbalimbali ambazo atatekeleza endapo atapata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo. Alisisitiza kuwa anataka kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa Kigoma, akitaja masuala muhimu kama huduma za afya, elimu, maji, na miundombinu bora kwa wananchi wake.

Moja ya ahadi zake kuu ni kufuta vumbi na kuboresha mazingira ya jimbo lake. Pia, aliagiza kutatua changamoto za huduma za afya, kujenga miundombinu bora ya maji, kuboresha elimu na stahiki za walimu, pamoja na kupambana na unyanyasaji wa bodaboda. Aidha, Baba Levo alijikita katika kuboresha masoko ya jioni kwa faida ya wakulima na wafanyabiashara wa mkoa wa Kigoma.

Mnasema Mwanza ni Mujii, Kigoma ni bhurekiyaao..Ona vyuma vimebhebhanaa(treni na reli)..Watani mpoo Baba levo atawapaisha japo wanasiasa siwaamini.
 
Naona anapanga kete zake vizuri lakini kwa mbinu ile ile ya kutumia bodaboda na bajaji kama kundi la wapiga kura watiifu...
 
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Clayton Revocatus Chipando, maarufu kama Baba Levo, leo ameanza rasmi kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025-2030. Uzinduzi wa kampeni hizo ulifanyika katika Viwanja vya Mwanga Community Center, ambapo Baba Levo alikusanya umati mkubwa wa wakazi wa Kigoma.

Akizungumza mbele ya wananchi, Baba Levo alijikita katika kutoa sera na ahadi mbalimbali ambazo atatekeleza endapo atapata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo. Alisisitiza kuwa anataka kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa Kigoma, akitaja masuala muhimu kama huduma za afya, elimu, maji, na miundombinu bora kwa wananchi wake.

Moja ya ahadi zake kuu ni kufuta vumbi na kuboresha mazingira ya jimbo lake. Pia, aliagiza kutatua changamoto za huduma za afya, kujenga miundombinu bora ya maji, kuboresha elimu na stahiki za walimu, pamoja na kupambana na unyanyasaji wa bodaboda. Aidha, Baba Levo alijikita katika kuboresha masoko ya jioni kwa faida ya wakulima na wafanyabiashara wa mkoa wa Kigoma.
Hizi ni story kama story nyingine, nchi inanuka rushwa polisi hawajabadilika bado!
 
Back
Top Bottom