Mbunge wa Kigoma Mjini Clayton Revocatus (Baba Levo), akichangia Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa 2026/2027, leo Juni 22, 2026 Bungeni, amesema hatokubali ongezeko la tozo kwa Maafisa Usafirishaji ‘Bodaboda’ akisisitiza kuwa kundi hilo ni miongoni mwa Vijana waliowahi kuwa msaada mkubwa wakati wa kampeni za uchaguzi.
"Hatutakubali kuona vijana wanaongezewa mzigo, nendeni mkachunguze, 75% ya bodaboda ni darasa la saba ambao darasa la saba ambao wametengwa kwenye wizara karibia zote. Ukituona juzi kulikuwa na kazi zimetangazwa jeshini, wanatangaza kuanzia form four, form six, chuo. Darasa la saba mmewaacha mtaani. Angalieni wizara zote.
Sasa sehemu ambayo wamejiegemeza tunataka kwenda kuwakandamiza zaidi ya 75%. Na mimi darasa la saba niko humo ndani, siwezi kuwageuka ndugu zangu, siwezi kuwageuka. Kwahiyo tunaomba hizi tozo zipelekwe kwingine. Si mtuletee sisi watu wa tungi? Bia ilikuwa inauzwa 1,000 mkapandisha 2,000, 3,000 tunalipa tu. Watoleeni bodaboda, tuleteeni sisi watu wa tungi sisi tutalipa hiyo haina shida yoyote."