Baba Levo kudai fidia kuhusu kesi yake aliyoshitakiwa na Harmonize

Baba Levo kudai fidia kuhusu kesi yake aliyoshitakiwa na Harmonize

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Msanii Baba levo anefunguka leo akiwa kwenye press conference yakutangazwa kuwa balozi mpya wa Soka bet amesema baada ya kushinda hii kesi aliyoshitakiwa na Harmonize atamfungulia mashitaka harmonize ya kuchafua brand yake.

Akafunguka zaidi kuwa Harmonize amekurupuka kumshitaki bila kutumia akili pamoja na mwanasheria wake mimi nitamuonesha hasara ya kukurupuka ni nini nataka hii kitu kiende Mahakamani na sitaki tumalize kiundugu huwezi kunishitaki nimevujisha video zako za utupu ikiwa me sina ukaribu na wewe ninashangaa sijui hiyo video unaipataje sijui atadhibitashe Mahakamani.
 
Yuko sahihi akuanzae mmalize,ila sema hawa wote kuanzia harmonize na kundi la vanny ni washenzi.
kosa la Baba levo ni kushupalia upuuzi, jamaa sasa ni mtu mzima na alikuwa na jina lake hapa nchini hakutakiwa kuongelea mambo kama hayo ya ma video ya utupu
 
Hawa watu bwana,,, hivi sisi umma story za hivi zinatufaidisha nini? Tumenyimwa Bunge live kwa madai ya kwenda kufanya kazi lakini udaku live nje nje
 
Kutokuwa na ukaribu nae haimaanishi kuwa hawezi sambaza hizo video..yeye alipoletwa asinge zipost kwa wengine....kusema hajui atathibitishaje huko mahakamani..sasa si ndio angoje akaone!
 
Hivi hiyo "kitu" ya harmonize ikwapi? Nataka kuishuhudia
 
  • Mshangao
Reactions: rr4
Baba levo Yuko sahihi harmonize anatakiwa akaiambie mahakama ni kwa vipi baba levo kavujisha video za utupu wake
 
Daaah hii ndo bongo bhana.

baba levo leo kawa balozi wakati vanny hajawai hata kupewa ubalozi wa pipi.
Usishangae ukakuta ni mkataba wa huyo chawa wa millioni moja au mbili..

Ishu sio kuwa balozi,ishu ni mkataba ni wa bei gani?
 
kosa la Baba levo ni kushupalia upuuzi, jamaa sasa ni mtu mzima na alikuwa na jina lake hapa nchini hakutakiwa kuongelea mambo kama hayo ya ma video ya utupu
Hilo jina lilimpa nini kipindi hicho? Uoni now anakula madeal tu.
 
mkuu, jamaa alikuwa Diwani, na ana fao la udiwani
Diwani mshahara 350000 na posho za kindezi kabisa. Sasa uoni now anashine kuliko kipind hicho labda Kama wewe unambishia muhusika maana nimewahi kumsikia mwenye akitamka maeneno hayo, kuwa sasa ana maisha mazuri zaidi ukilinganisha na kipind hicho.
 
Mkuu,haya kwakuwa mwenyewe amesema hivo ngoja nikubali
 
Back
Top Bottom