Baba Levo na ajenda ya kuomba misaada, Je tutafanikiwa kulinda kizazi kijacho?

Baba Levo na ajenda ya kuomba misaada, Je tutafanikiwa kulinda kizazi kijacho?

Joined
Oct 14, 2026
Posts
32
Reaction score
43
Watanzania wakati mwingine tujitahidi kuwaza mbali tusipende kurahisisha vitu.

Ni vema kuwaza, tuondokane na haya maisha ya kuombaomba.

Ni urithi mbaya sana wa kifikra huu tunaachia watoto wetu. Kumbe huwa mnawasimanga bure wagogo ombaomba, nimegundua hii ni tabia ya watu wengi na ipo kwenya damu bila wao kujua.

Lakini pia tujiulize kama hii ndio kazi hasa ya mbunge au ni kupalilia njia yake kurudi tena mjengoni.?

NYIE JIULIZENI KITU KIMOJA, MAMA YETU ALIVYOINGIA TU MADARAKANI HATA MWEZI HAKUMALIZA AKAANZA KUZUNGUKA DUNIANI KUOMBA OMBA, KIKO WAPI !!!

SASAHIVI HATAKI HATA KUSIKIA.

HAKUNAGA KITU CHA KUPEWA BURE NYIE TUKANENI LAKINI NAJUA UKIKAA PEKE YAKO UKATAFAKARI KWA UNDANI UTANIELEWA.

Na hapa naomba nieleweke vizuri, SIPINGI msaada unaowanufaisha wananchi napinga mfumo unaoweza kufanya msaada wa wahisani uonekane kama mbadala wa wajibu wa Serikali. nieleweke vizuri,
Fikra tunazozipandikiza kwenye kizazi chetu ni kwamba ili uwe Mbunge lazima uwe na uwezo binafsi wa kushawishi watu Kutoa misaada sasa wabunge wote wakiwa hivi ni nani atamfanya kazi ya kuiwajibisha na kuisimamia Serikali.?

HUWEZI KUTATUA TATIZO LA KUDUMU KWA SABABU ZA MUDA MFUPI, yani mfano kwa joto hili unaamua kuuza kiwanja ili ununue feni na friji. Joto litaisha utaingia msimu WA baridi lakini pia friji au feni haitadumu Ila kiwanja kimeenda.

Ndo kinachofanyika sasa,, Mashule yanaongezeka, mahitaji ya madawati yanaongezeka na Siku moja Baba levo hatakuwepo, Lakina kama IPO MIFUMO imara ya kuiwajibisha serikali itatusaidia vizazi na vizazi.

Wahisani wanaweza kusaidia, lakini upatikanaji wa madawati, dawa na huduma nyingine za msingi haupaswi kutegemea uwezo wa Mbunge kuombaomba kwa watu.

Tusifike mahali ambapo tunamsifu Mbunge kwa kutafuta msaada wa kutatua tatizo ambalo Serikali ilipaswa kulishughulikia kupitia mifumo yake ya kawaida.

Tunapaswa kupima uongozi si kwa misaada iliyopatikana pekee, bali pia kwa namna kiongozi anavyohakikisha taasisi za Serikali zinatimiza wajibu wake.

Sasa kwa mwendo huu tutawezaje kuashawishi watoto wetu walinde migongo?
Kumbuka Siku anapokabidhi hiyo misaada lazima awataje wafadhili ambao ni watu au mashirika binafsi kwaio watoto wanajua,,aahh kumbe sio Serikali.

Je, inatuma ujumbe gani kwa watoto kuhusu serikali Yao kama sio kupanda chuki mapema?
Screenshot_20261103-121701.jpeg
1793695723961.jpeg
1793681849377.jpeg
 
Amejitahidi sana ila ni vema ahamasishe na wazazi ambao wanaweza kutengeneza dawati hata Moja wafanye hivyo kwa kuwapa mfano baada ya mwaka Moja au miwili hatakuwa na shida ya dawati baada ya hapo wahamie kwenye ku digitalize shule hasa ubao
 
Sahihi
 
Kiukweli hili suala linatafakarisha. Hizi mambo za misaada huwa zina ukakasi sana. Kwa mfano Morogoro road kwenye kona ya kwenda Muhimbili kuna banda la traffic police limeandikwa kabisa donated by kampuni fulani. Sasa hii kampuni haiwezi tumia hii misaada kupata upenyo wa kuvunja sheria na polisi kukausha tu? Ninaisihi serikali yangu tukufu ikwepe misaada ya hawa wafanyabiashara badala yake iwabane kulipa kodi na hizo kodi ndo zitumike kutengeneza madawati na mambo mengine ya maendeleo. Hakuna mfanyabiashara anayeweza toa kitu bila kujua atafaidikaje... HAKUNA HAKUNA HAKUNA!...
 
Kabisa Mkuu,,
Hakuna mfanyabiashara mjinga kiasi hicho...
Na sio tu mfanyabiashara,,
Nijuavyo Mimi hakuna kitu Cha kupewa bure lazima kuwe na value exblchange hata kama ni kwa baadae.
 
UKiwa kigoma utashuhudia malori yakiwa ba shehena za miti ikisafirishwa kwenda kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa.

Kisha unakutana na mbunge wa eneo husika akienda kuomba msaada wa madawati!

Ama kwa hakika, katikati ya maji, mpumbavu anaona/ anahisi kiu kwa kukosa maji!
 
Aibu sana
 
Back
Top Bottom