Baba Lishe avunja dhana potofu za jinsia katika Tamasha la Chakula

Baba Lishe avunja dhana potofu za jinsia katika Tamasha la Chakula

News TZ

Senior Member
Joined
Jun 17, 2015
Posts
132
Reaction score
75
Baron Stanslaus 1.JPG


Dar es Salaam, 29 Septemba 2024 – Tamasha la chakula la Coca-Cola Tanzania maarafu kama ‘Coca-Cola Food Fest’ limezidi kunoga huku muuzaji mmoja, maarufu "Baba Lishe," akiibuka kuwa kivutio cha kipekee. Stanlaus Baron, ambaye ni muuzaji wa chakula anayekua kwa kasi, amejitokeza kupinga mitazamo ya kijinsia inayokita mizizi katika tasnia ya upishi, akionyesha kuwa jiko si la wanawake pekee.

Baron amepata umaarufu kupitia chakula chake chenye ladha ya kipekee cha tambi na maini huku mwenyewe akipinga wazo la kwamba upishi ni kazi ya wanawake pekee. "Kupika ni kipaji kama kazi nyingine yoyote," alisema Baron alipokuwa akihojiwa huku wateja wakiendelea kufurika kwenye banda lake.

Tamasha la Chakula la Coca-Cola Tanzania limekuwa jukwaa muhimu la kuonyesha vipaji vya upishi kwa wilaya ya Kinondoni wiki hii baada ya kutembelea wilaya ya Ubungo wiki iliyopita, huku likileta pamoja wachuuzi wa chakula kutoka sehemu mbalimbali. Hata hivyo, hadithi ya Baron imechukua umaarufu wa kipekee, ikilenga kuvunja dhana potofu za kijinsia zilizodumu kwa muda mrefu ndani ya jamii ya Kitanzania.

Baron, ambaye alikua akivutiwa na upishi tangu utotoni, anasema alikumbana na upinzani kutoka kwa jamii na hata familia yake kwa sababu alikuwa mwanaume aliyeonyesha mapenzi makubwa kwa upishi. "Watu walikuwa wakiniambia kupika ni kazi ya wanawake, lakini sikukubaliana na hayo mawazo. Kupika ni ustadi muhimu, na furaha ya kuwahudumia watu kwa chakula kitamu haifananishwi na kitu chochote," alisema.

Akiwa katika tamasha hilo, Baron alitoa wito kwa wazazi na walezi kote nchini kuacha kuwabagua watoto wao kwa misingi ya kijinsia, hasa linapokuja suala la vipaji vyao. Aliwataka wazazi kuwaunga mkono watoto wao, iwe ni katika upishi, uhandisi, au hata michezo. "Tunahitaji kuwapa watoto uhuru wa kufuata ndoto zao bila hofu ya kuhukumiwa," aliongeza.

Kupitia mapokezi mazuri aliyopata kwenye tamasha hilo, Baron sasa ana mipango ya kupanua biashara yake, akiwa na ndoto ya kufungua mgahawa wake mwenyewe. "Hii ni mwanzo tu. Nataka kuendelea kuthibitisha kwamba yeyote, bila kujali jinsia, anaweza kufanikiwa jikoni," alisema kwa kujiamini.

Ujumbe wa Baron unaonekana kuleta mabadiliko, sio tu katika tasnia ya upishi, bali pia katika jamii kwa ujumla. Katika tamasha ambalo limekuwa likitangaza vipaji vya upishi, hadithi ya Baron imeibuka kuwa moja ya za kukumbukwa zaidi mwaka huu, ikiashiria kuwa wakati mwingine, ujasiri na dhamira ndiyo viungo muhimu zaidi katika safari ya mafanikio.
 
Hahaha ni rost ya kawaida kabisa mkuu
Mahitaji.
1.Dagaa
2.Karoti 4
3.Hoho 2
4.kitunguu maji
5.mafuta ya alizeti
6.Curry powder
7.Chumvi (kidogo)

Mtindi mdogo wa kuburudishia mdomo
🙄😂 Umeikumbuka Hadi curry powder?na Yogurt for taste🙄😂😂😂 kwa asilimia 200 wewe ni Kataa ndoa automatic 😏😏
 
Hizi ni dhana na upotoshaji tu
Mama atapika nyumbani na ndio tumekuwa tukiona hivyo maana baba haiingii jikoni akiwa nyumbani
Lakini likija suala la mapishi ya mahoteli wanaume ndio wana dominate kwa sababu kwanza inachukua mda mchache sana kwa mwanaume kupika kuliko mwanamke (fact)

Mimi mwenyewe sasa hivi nimeandaa prawns wangu nawakaanga vizuri na nitakula na wali mweupe wenye harufu ya saffron

Angalia dunia nzima wapishi wa mahoteli makubwa wanaume ndio wanapika
Hizi dhana ni muflis kwa wanaojua mapishi
 
baba yangu alikataza katakata hata kusogelea jiko. wameru mfumo dume kama wakurya. nimekuja kujifunza kupika utu zimani. lakini huona uvivu kupika nikikaa na mwanamke.
 
Back
Top Bottom