Baba Mchakachuaji, Mama Mchakachuaji

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Wajameni
Kuna rafiki yangu kanifuata kuniomba ushauri afanyaje nami nikaona niombe msaada hapa jamvini,
Baba yake ni Dereva wa magari ya mizigo anaesafiri mara kwa mara mikoani na hata nje ya nchi.
Ilipofikia wakati wa kuoa rafiki yangu huyo alimpata msichana mmoja chuoni Mzumbe alikokua akisoma na kwenda kumtambulisha nyumbani kwao lakin Baba yake alimkataa bila sababu,
Ili kutomvunjia baba yake heshima akaamua kwa shingo upande kuachana na yule msichana. Lakin baada ya kama mwaka hivi jamaa alimaliza chuo na kupata kazi hapa Dar ambako alipendana na msichana mmoja hivi wa ofisini kwao, cha ajabu kumpeleka home Baba yake akamkataa tena.
Jamaa ilibidi atafute faragha na Baba yake kuuliza kulikoni ambako alijibiwa kua wale walikua ni dada zake wa Kambo ila mama yake hajui na asimwambie.
Jamaa kwa uchungu alishindwa kuvumilia ikabidi amueleze mama yake kinaga-ubaga sababu za Baba yake kukataa, lakini alijishauri sana jinsi ya kumuanza maana alijua mama yake angehuzunika.
Cha ajabu mama yake alivyosikia hivyo alicheka sana na kumjibu kifupi tu ''we kamuoe yoyote kati ya hao, kwani unafikiri hata yeye ni Baba yako mzazi basi? Wewe nilim'bambikia tu, hivyo hata hao wanawake si damu moja na wewe''
Sasa jamaa hajui afanyaje ndio kaniomba ushauri afanyaje!!
 
Ndoa ndoano....

Na huyo mama ni kauzu zaidi ya dagaa lol
 
Ama kweli hii kiboko...........tukue na kusikia mengi.
 
mla nae huliwa! Ninawasiwasi hata cheti cha ndoa kitakuwa feki
 
Sawa,
Lakini tusaidiane basi jinsi ya kumshauri jamaa.
Maana anafikiri hata akitafuta mwengine anaweza nae kua dada yake, so aoe tu mmoja kati ya hawa wa mwanzo? Sina hakika kama yule wa mwanzo bado yuko 'single'
 
Duh! Anyway, Jamaa akifata ushauri wa mama yake atatengeneza mgogoro mkali sana baina ya wazazi wake. Ajaribu kufata ushauri wa Baba yake, na afiche siri aliyoijua kutoka kwa Mama yake. Maisha bana!!?
 
Huyu ameamua kuwa popo, usiku anaruka kama ndege, na akitotoa ananyonyesha[Aamue moja tu] arudi kwa dingi amuulize naye ammpe siri zote kuwa hao dada zake wengine wako wapi na wanaitwaje, akishaijua mipaka alikoishia baba yake aanzie hapo kwenye boundary asonge mbele aswage atakavyo atampata tu Mungu aliyemuwekea kama yupo. maana wakati mwingine vikwazo hutokea kwa vile hujapangiwa na wewe kuwa na uzao wako. Vilevile hajachelewa sana, hivi kuna limitation ya age kujiunga na useminarini? Jaribu na huko maana maisha popote:car::kev: halafu ishia zako
 
Usikute hao dada zako wa kambo ulishaonja wewe, maana siku hizi vijana ati mnafanya Road test kujua majambozi yatakuwaje mkiwa ndani kwenu? Kuwa mkweli. Kama ulishajuana nao kihivyo, hapo hatari kubwa shukuru hawakupata ujauzito maana mnetuongezea waishio katika mazingira hatarishi
 
Kwa hakika kabisa kwa tabia ya baba yake yawezekana kwa asilimia 99 hao nao ni mama zake wadogo na huenda hata huko baba yake atabambikiwa dada zake wa kambo wengine, Mpe pole dunia hii haina maana
 
Imepikwa hii story haiwezekani coincidence zitokee namna hii
 
Imepikwa hii story haiwezekani coincidence zitokee namna hii
Nimewahi isikia kijiweni.........kama ni kweli basi jamaa atafute mwingine tu wa kuoa ili kuepusha mgogoro.
 
Nimewahi isikia kijiweni.........kama ni kweli basi jamaa atafute mwingine tu wa kuoa ili kuepusha mgogoro.
<br />
<br />
Na huyo mwingine atakuja ambiwa ni dada yake.
 
Sawa,
Lakini tusaidiane basi jinsi ya kumshauri jamaa.
Maana anafikiri hata akitafuta mwengine anaweza nae kua dada yake, so aoe tu mmoja kati ya hawa wa mwanzo? Sina hakika kama yule wa mwanzo bado yuko 'single'

Aoe mhindi, mchina au mzungu ambaye hajachanganya damu na mwafrika. Au aende nje ya Tanzania ambako baba yake huwa hasafiri na Malori kwenda huko. Lakini alishawahi kujiuliza kuwa huenda mzee mzima anawatamani hao mabinti anaokwenda nao na hivyo anamkatisha tamaa tu ili akiwaacha mzee awatokee kiulaini?
 
Hii nakumbuka kama ilishawahi kutoka ktk Ze Komedi. Sina uhakika kama double concidence of want inaweza kutokea twice.
 
Nadhani asonge mbele....kwa sbb kaishajua dingi wembe mama mkasi...anaweza kuwa Padri pia...sio lazima sana uoe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…