Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Wajameni
Kuna rafiki yangu kanifuata kuniomba ushauri afanyaje nami nikaona niombe msaada hapa jamvini,
Baba yake ni Dereva wa magari ya mizigo anaesafiri mara kwa mara mikoani na hata nje ya nchi.
Ilipofikia wakati wa kuoa rafiki yangu huyo alimpata msichana mmoja chuoni Mzumbe alikokua akisoma na kwenda kumtambulisha nyumbani kwao lakin Baba yake alimkataa bila sababu,
Ili kutomvunjia baba yake heshima akaamua kwa shingo upande kuachana na yule msichana. Lakin baada ya kama mwaka hivi jamaa alimaliza chuo na kupata kazi hapa Dar ambako alipendana na msichana mmoja hivi wa ofisini kwao, cha ajabu kumpeleka home Baba yake akamkataa tena.
Jamaa ilibidi atafute faragha na Baba yake kuuliza kulikoni ambako alijibiwa kua wale walikua ni dada zake wa Kambo ila mama yake hajui na asimwambie.
Jamaa kwa uchungu alishindwa kuvumilia ikabidi amueleze mama yake kinaga-ubaga sababu za Baba yake kukataa, lakini alijishauri sana jinsi ya kumuanza maana alijua mama yake angehuzunika.
Cha ajabu mama yake alivyosikia hivyo alicheka sana na kumjibu kifupi tu ''we kamuoe yoyote kati ya hao, kwani unafikiri hata yeye ni Baba yako mzazi basi? Wewe nilim'bambikia tu, hivyo hata hao wanawake si damu moja na wewe''
Sasa jamaa hajui afanyaje ndio kaniomba ushauri afanyaje!!