Baba mtoto wake arudi kwa kishindo

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
14,422
Reaction score
7,350
Wanabodi mnisaidie....!kuna dada mmoja niko nae katika mahusiano sasa inafikia mwezi..huyo dada ana mtoto mmoja amezaa na kaka mmoja yupo mkoani..ila tokea alivyo mbebesha mimba jamaa alimtelekeza,mpaka huyo dada alipojifungua, jamaa akaja kumcheki mtoto alafu akapotea tena kama mwaka mmoja na nusu..jamaa akipigiwa simu hapokei,akaja kumcheki mtoto Pasaka mwaka huu.akapotea tena mpaka hapa juzi aliposikia huyu dada amepata mpenzi(yaani ndo mimi)ameanza kumsumbua katika simu kila siku anampigia anambembeleza naona na huyu dada kama mashart ameanza kulegeza..!wakati tulipoanza mahusiano kila siku alikua anasimbua nimwambie kuwa tuwe wote pamoja..mimi nikawa ninamwambia MDA NDO UTASEMA,sababu nilikua nina wasiwasi baba mtoto aliezaa nae asije akarudi ikawa tete,nilikua nikimwambia kuhusu mzazi mwenzie anadai hawezi kuwa nae tena,,eti alishanawa..ushauri niendelee au
 
Mtalaka hatongozwi...pole sana kama kuna dalili hizo achia mzigo utaishi kwa wasiwasi sana katika maisha yako na huyo mwanamke...kumbuka mawasiliano ya mzazi mwenzake kimsingi hayata koma..
 
Mwezi si muda mrefu wako na yeye mwambie aamue nini anataka maisha na wewe au baba watoto. Kama ni usumbufu wa simu abadilishe namba au simply asipokee. Zungumza nae mpaka kieleweke
 
Haya mambo sipendi kuyasikia kabisa.
 
Weweeee....awali ni awali hakuna awali mbovu....sepawewe huna chako apo..usipoteze muda. Huyo jamaa anampenda mtuwake alikuwa anatikisa kiberiti tuu,si unaona sasa moyo unamuwasha kwa wivu baada ya kusikia ana mwingine...angalia mustakabali wako bro hunachako apo.SEPAA.
 
Leo nitaenda mpasulia ukweli wake...!
"Vox populi,Vox dei"
 

Kwa kifupi dada katelekezwa sana tu na huyo jamaa, yani kadhalilishwa sana na hajaonja upendo wa huyo jamaa kwa kipindi kirefu sana na mbaya zaidi ndio kipindi alichomuhitaji zaidi.
Kama analegeza masharti baada ya kutendewa haya yote basi its obvious she really loves him...
Mi nashauri waache walee mtoto wao.
 
kuna wanaume wengine wanamuacha mwanamke wakifikiri kua huyo mwanamke hataweza kupata mwanaume mwingine na hivi yuko bize na mtoto..sasa akishajua ana mtu kale kawivu kanarudi...mtu ka huyo hawezi kua anampenda huyo dada wakati kamuacha yeye na mtoto wake..
 

Ulichosema ni sahihi..huyu Dada aliniambia kua mzazi mwenzie anaishi na mwanamke mwingine..alikua anamjibu vibaya akimuuliza..mfano alimwambia hawezi pata mwanaume mwingine sababu ameshamzalisha...
 
unajua kuna mijanaume yenye tabia hiyo....

akiona ex kapata mpya anarudi kujilambalamba....

lakini inategemea na msimamo wa msichana wako.....

ila akimrudia ex wake atakuwa sio mzima.....
 
Mhhh...mdogo wangu hapo ni akili ya huyo mwanamke tu..maan kama ni kupendwa na huyo mzazi mwenzie ni wazi kabisa hapendwi.kma unauhakika anataka kurudi kwa mzazi mwenzie mwache tu aende akauone moto..na wewe endelea mbele na maisha yako..
 
Wanaume hua wanataka akikuacha ubaki single milele, akisikia una mpenzi mwingine utamuona anaanza kujipendekeza!
 
Kaka, jipange sawa sawa. Huyo bwana ameanza hizo mbwembwe sasa hivi za kupiga simu, kuna siku atakuja kuona mwanae hapo itakuwa mbinde.

Tumuombee huyo madam aone mbali, akae na wewe huyo ex ni mwendawazimu tu hana mapenzi kwae.
 
achia nanga by the way mwezi mmoja bado ni mda mfupi,,, mwepuke huyo dada,,, utajajuta later. Remember its easy to forget abt the past when future seems to sound good.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…