Baba mzazi halisi wa mtoto atabaki kama siri ya mama mzazi

Baba mzazi halisi wa mtoto atabaki kama siri ya mama mzazi

I M

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2012
Posts
434
Reaction score
767
UTANGULIZI

MUHIMU: Kisa hiki ni cha kweli sio hadithi ya kusimuliwa wala kufikirika na nitakiandika kama ninvyokikumbuka. Kisa nitakiandika kwa ufupi na kukigawa iwe rahisi kusomeka.

ANGALIZO; Majina yote ya wahusika yaliyotumika sio halisi.

WAHUSIKA
Nikiwa hometown nafanya kazi sehemu wakati nasuburi kuingia chuo baada ya kumaliza kidato cha sita miaka kadhaa iliyopita nilifahamiana na Kendrick na girlfriend wake Magie kupitia boss wangu.
Kendrick alikua videographer na producer, saivi yupo media moja maarufu nchini Tanzania na Maggie alikua anasoma diploma chuo X. Maggie alikua na tabia ya kuja sana ofisini hivyo nilimzoeana zaidi kuliko Kendrick.

Siku zikasogea nikapata chuo. Nikiwa chuoni nikakutana na Florian tukawa marafiki, tunaosoma coarse moja pia tunatoka mkoa mmoja.

Kama wengi mjuavyo mambo ya vyuoni, vijana wengi hujifunza kuutumia uhuru wao kwa mara ya kwanza na kuanza kujaribu mambo mengi.

Rafiki yangu Florian alikua na girlfriend mkoa mwingine na chuo chetu kilipo, hivyo weekend kadhaa alienda huko kumuona. Ni kama masaa manne hivi kwa bus, maana ni mikoa inayopakana.

Florian ana rafiki yake mwingine anaitwa Charles hapo chuoni na urafiki wao ulianza kabla ya chuo. Charles alikua ni mtu mjanja janja sana ukilinganisha na sisi wengine.

At this point, almost all important characters have been established.

Kisa kinaanza, Siku moja karibia na semister ya kwanza kuisha nikiwa room, Florian aliniambia yuko na mgeni anataka anitambulishe then wao jioni wataenda kulala nyumba za wageni (Lodge).

Nikawakaribisha waje room, walipofika na kuwafungulia mlango, kumbe! mgeni ni Maggie. Maggie baada ya kuniona alishtuka sana, Florian akauliza mnajuana? Maggie akajibu, ananijua kupitia boss wangu nilipokua nafanya kazi kabla ya chuo na nilikua naendelea kila likizo.

Tukapiga story za hapa na pale, Maggie ni mchangamfu sana hivyo jioni ni kama iliwahi kufika wakasepa. Japo kwa Florian ilikua inachelewa sana 😆

Baada ya kama dakika moja wao kuondoka, Maggie alinitumia text, kafurahi kuniona ila naomba nimtunzie siri akipata nafasi atanieleza vizuri. Kijana sikutaka makuu kwa lolote nikawaacha vijana wakaichafue miili yao.

Itaendelea .....
 
SEHEMU YA PILI
Baada ya weekend kuisha Maggie alirudi mkoa chuo chake kilipo. Maisha yakaendelea. Maggie alikuja kuniambia yuko kwenye mchakato kwa kuachana na Kendrick sababu haoni future pamoja na hilo wana imani tofauti. Maggie alikua mkristo tena mmoja wa viongozi wa USCF na Kendrick alikua ni muislam.
Mwaka wa kwanza ukaisha tukarudi nyumbani (home town).

USALITI
Tukiwa likizo weekend moja usiku Charles na Maggie walikutana club (sijui kama walipanga au ilitokea tu ila ninachojua usiku huo mtu na shemeji yake wakaelekea lodge badala ya nyumbani wakisingizia pombe).
Florian akajua rafiki yake katembea na girlfriend wake (mpaka leo sijui alijuaje au taarifa zilimfikiaje ila ilijulikana na hakuna kati ya wahusika aliyekana).

Maggie akawekwa pembeni, Florian akampata Happy... na penzi likawa HAPPY HAPPY

NGOMA BILA BILA
Likizo Ikaisha Mwaka wa Pili ...
Florian na Charles wakaja kusameheana ila mipaka ikaimarishwa sana. Florian akamhurumia Maggie sababu ya machozi aliyokua akimlilia kila siku hivyo akapretend kurudiana nae ila hakuachana na Happy.
Baada ya mda Florian na Maggie wakaanza kutembeleana tena. Kipindi hiki Maggie alionesha yuko serious sana na kaacha makandokando yote na Florian yupo peke yake.
Je, ni kweli?

Likizo fupi baada ya semister ya kwanza ya mwaka wa pili kuisha, nikiwa kwenye kazi zangu zilezile akaja Kendrick katika mazungumzo akasema anaenda kumuona Maggie. Hahaha
Kwa kifupi Maggie alikua na mahusiano na Kendrick na Florian wote kwa wakati mmoja na Florian alikua na mahusiano na Maggie na Happy wote kwa wakati mmoja.

Anyways, Fast Forward here to Mwaka wa Tatu ...
Maggie baada ya kumaliza diploma, akapata chuo kilichopo mkoa mmoja na chuo chetu na kuanza safari ya kuitafuta Bachelor degree.
Mda wote huu sikuwahi kumwambia Florian kua Maggie alikua au yuko na Kendrick, sababu hakua serious nae baada ya usaliti. Pia, sikuwahi kumwambia Maggie kua Floriani yupo na Happy.
In short niliamua kuwaachia mambo yao wenyewe.

NJIA PANDA
Ukaribu wa vyuo uliwaleta karibu sana Florian na Maggie ukizingatia Happy alikua akiishi hometown. Kipindi hiki nilikua nakaa chumba kimoja na Florian. Maggie alikua mgeni wetu wa mara kwa mara.
Tukiwa mwaka wetu wa nne na wa mwisho, semister ya kwanza katikati Florian alirudi kutoka kwa mchepuko wake Maggie akiwa amepanic! Baada ya kuwekana sawa akaniambia Maggie ana mimba yake.
Je, watoe au walee?
Changamoto zilikua nyingi lakini mwisho wa siku msimamo wao ulikua ni kulea.
Maggie akamsihi Floriani kama wanatunza aende akajitambulishe kwa wazazi wake. Florian akapanga kwenda kujitambulisha kabla Maggie hajajifungua na akapanda mipango ya hela na kaka yake ambaye alikua anafanya kazi na alikua financially good.

Majukumu humfanya mtoto kua mtu mzima. Florian alibadilika gafla kuanzia kufikiri, kuongea mpaka kutenda kwake. Hela zikapatikana kutoka kwa kaka yake, tayari kwa ajili ya utambulisho na mahali kabisa.
Jambo kubwa lililokua limebaki kwa Florian ni anawaambiaje wazazi wake kwamba kuna binti ana mimba yake na anatarajia kuoa baada ya kumaliza chuo.
Wakati bwana Florian anawaza na kupanga atakavyowaambia wazazi wake .
Maggie nae anajikuta yupo njia panda na hajui cha kufanya na mda haupo upande wake.

Itaendelea ...
 
SEHEMU YA TATU
KWELI HUMWEKA MTU HURU
Florian hajawahi kutilia shaka kabisa kuhusu mimba aliyoibeba Maggie. Florian alitumia likizo na field ya mwaka wa tatu jiji moja maarufu hapa nchini huku Maggie akiwa hometown. Hivyo wakati wa likizo hii ndefu hawakua karibu kimwili kabisa.

Wahenga walisema mda utaamua, hili lilimkuta Maggie baada ya kuona kitumbo kinaanza kutoka. Maggie alimlazimu atoke njia panda na kuchagua njia moja. Maamuzi hayakua marahisi ila ilibidi anyooshe mikono na kumwambia ukweli Florian.

Ilikuaje?....
Maggie alidanganya miezi ya mimba ili Florian akipiga mahesabu yake ajue kweli yeye ni mhusika. Florian alikua anajua mimba ni ya mwezi mmoja na nusu ila uhalisia mimba ilikua imezidi miezi mitatu kwa weeks au siku kadhaa.
Maggie baada ya kuona dalili ya ki bump kwa mbali akaomba akutane na Florian wazungumze. Florian akaambiwa ukweli kwamba wakati wa likizo akiwa jijini, kama wahenga walivyosema fimbo ya mbali haiui nyoka, alipasha kiporo na Ex wake anaitwa Kendrick. Kendrick tena!
Wakati huu sasa Kendrick alikua kaoa tayari. Maggie akamsihi sana kwa machozi mengi waendelee na mpango wa kuoana kwani Kendrick hana future nae isitoshe kaoa tayari mke wa kwanza na yeye hawezi kua mke wa pili au kubadili dini, ilikuwa bahati mbaya tu.

Hapa kweli ilimueka mtu huru ila sio msema kweli bali mpokea kweli. Florian akawa mtu huru na ilimfanya awe makini sana kwenye masuala ya mahusiano.
Florian safari hii hakuangalia nyuma.

Je, Huo ndio ukweli wote?

HAMNA SIRI DUNIANI
Florian baada ya kurudi akaniambia yote yaliyojiri na uamuzi alioufanya. Nikamtania na kumpongeza kwa kuponea tundu la sindano maana uhalisia ni kwamba wangekua ndani ya ndoa au likizo angepata nafasi ya kukutana kimwili basi ni dhahiri angelea mtoto asiye damu yake. Miezi miwili ilikua ngumu sana kuficha kwa mazingira yao.

Sasa kesi ikarudi kwangu, nilikua namjua Kendrick na nikakaa kimya nisimwambie. Siri imetolewa na mwenye siri mwenyewe.
Ilinibidi nimwambie kweli najua mahusiano yao ila sikuona haja sababu uliniambia unaachana nae, isitoshe wewe pia nina siri zako, ili nikwambie siri zake ilitakiwa nimwambie na yeye siri zako. Akacheka bila kuongeza neno, ila alifurahi sana kwa kua hakua amepanga maisha ya kulea na ndoa mapema hivi na hakujua nyumbani namna ya kuwaeleza.

Siku iliyofuata Maggie alinitafuta na kuniomba nimuombee msamaha kwa Florian. Kwa kweli sikuweza kuongea neno lolote zaidi ya pole.
Hali hii ya kunitafuta iliendelea kwa mda mrefu kiasi cha kutaka kuleta shida kwenye mahusiano yangu ya wakati huo.

Siku zikaenda masomo yakaisha....
Nikiwa hometown katika kazi zangu nikapigiwa simu na Maggie kunipa taarifa kua kajifungua yupo nyumbani kwao. Siku ya pili yake nikatafuta kifurushi cha mtoto kuelekea kumuona Maggie na mtoto wake.

Je, tuliyokua tunayajua ndio ukweli wote au kuna siri zingine bado?

Itaendelea ...
 
Hakuna Siri na ushahidi upo mwingi tu. Wewe endelea na paragraph nyiiiingi lakini hakuna la maana. Kuna kabila moja mwanamke akishajua kavuruga ujauzito anameza dawa na mtoto akizaliwa anaoneka ni spice ya mle ndani. Lakini ukweli ni kwamba natural DNA, Tabia na Developed DNA zinagoma.
 
  • Thanks
Reactions: I M
SEHEMU YA NNE

CHELEWA CHELEWA UTAKUTA MWANA SIO WAKO
Nilifika na kupokelewa vizuri na familia. Tukasalimiana na kumpa hongera kwa kujifungua salama.
Sikuwaza kabisa kuchunguza mtoto anafanana na nani. Wakati wa kuondoka nilimuuliza Maggie kama kampa taarifa Kendrick. Alinijibu taarifa anayo anajipanga aje maana hawezi kuja hivi hivi bila utambulisho. Kendrick kipindi hiki alikua ameshahamishia makazi yake Dar.

Nikarudi town kuendelea na mishe mishe zangu za kila siku. Baada ya miezi kama mitatu kupita Kendrick akaja hometown akafika kututembelea mpaka ofisini.
Kendrick alifika kumuona mtoto, ila mama wa mtoto ( Maggie) kamzuia asiende nyumbani sababu hajajitambulisha rasmi, wazee wake hawawezi kukubali hivyo wakutane sehemu.

Tulipiga story za hapa na pale mpaka mama na mtoto wakawa tayari. Kenderick akaenda kuwafuata ili waende sehemu waliyopanga. (Joke! apate na picha mbili, tatu za kupost Happy Father’s Day )

Kipindi chote cha mimba mpaka kujifungua Kendrick alikua ameyabeba majukumu yake japo kuna wakati kinyonge lakini hajawahi kataa majukumu aliyopewa. Nasema haya maana kuna kipindi Maggie alikua ananilalamikia Kenderick kamtumia hela pungufu na aliyokua anahitaji.

Je, Kendrick atagundua chochote kuhusiana na mtoto wake anayemhudumia? Je, mtoto amebeba jina la nani?

Baada ya kumuona mtoto Kendrick hakuridhika na hali ya kumuona mtoto kiwizi wizi isitoshe soon Maggie anarudi kumalizia shule na alitaka aweze kumuona mtoto hata kama Maggie hatakuwepo nyumbani.

Kitu kingine kilichomchanganya Kendrick mtoto hakupewa jina la ukoo (Surname) la Kendrick bali la baba wa Maggie. Akaambiwa ndio utaratibu wa kwao mpaka utambulisho rasmi ufanyike ndio litabadilishwa.

Kendrick kesho yake akaja kuaga anarudi jijini ila atarudi tena akiwa na mzee wake waende jitambulisha vizuri kwenye familia ya Maggie.

Mda ukapita kidogo, boss wangu akaniambia amepigiwa simu na Kendrick wataenda kujitambulisha kwa Maggie hivyo siku hiyo hatakuwepo ofisini.
Team ikakamilika na boss wangu akiwemo ndani. Safari ya kwenda kujitambulisha ikaanza.
Walipofika walikaribishwa vizuri, zawadi zikapokelewa. Mazungumzo ya hapa na pale yakaendelea. Ili utambulisho ukamilike ilitakiwa Maggie aje amtambue/amtambulishe Kendrick kwa ndugu na wazazi wake.
Maggie akasalimia, akakubali kumjua Kendrick, ila...

Akamalizia Kendrick sio baba wa mtoto wake.
Watu wakajua utani, anamtania mtu wake, binti kakaza Kendrick sio baba wa mtoto.
Wazee wakajaribu kutumia busara labda ni hasira kuna kitu hakijakaa sawa siku hiyo, wapi! Kendrick sio baba wa mtoto ( watani wangemalizia full stop).
Shughuli ikaishia pale, watu wakarudi zao.

Je, baba halisi ni nani?

Itaendelea...
 
SEHEMU YA MWISHO

Unaweza ukawa unamhisi Charles ila ni jibu ni hapana!
Kendrick akaondolewa rasmi ila mpaka leo sijui kwanini aliamua kumfanyia hivi mbele ya familia yake, ni kisasi au roho kumsuta, Maggie ndio anajua.

Swali la msingi lililobaki ni mtoto wa nani?
Baada ya mda kupita Maggie mwenyewe akaja kuniambia kuna kijana mmoja tumuite John ndio baba halisi wa mtoto.
Je, John alikua anajua mda wote huu kua yeye ni baba wa mtoto wa Maggie?

Hapana, John alifichwa kabisa sababu alikua haonekani kama maisha yake yana future inayoeleweka.
Ila baadae maisha yakabadilika John akajipata kwa kiasi fulani na ndio akapewa majukumu rasmi na mapenzi yao yakaanza upyaaa. Japo aliniambia Maggie mwenyewe ila nina mashaka na ukweli wake.

Mwisho wa siku mawasiliano na Maggie yalikata na nikahama hometwon kutafuta maisha sehemu nyingine.

Nimeikumbuka hii story baada ya ya kupewa taarifa na kadi ya mchango kwamba Maggie anaolewa.

Jambo ambalo sio la kushangaza bwana harusi sio JOHN.

MWISHO
 
Kawaida sana katika maisha ya mwanadamu Duniani hapa
 
  • Thanks
Reactions: I M
Siwezi kuiacha hiyo power ya kuujua ukweli kuhusu mtoto ibakie mikononi mwa Mwanamke halafu mimi nibaki naishi kwa imani. Hiyo ni kwa wasiojielewa pekee.
Mimi siyo mtu wa imani, bali knowledge, siku zote natafuta knowledge.
Kwenu nyie waumini ambao imani pekee inatosha ndiyo mnaweza mkaendelea kuaminishwa hadi kwenye mambo sensitive yanayogusa vizazi vyenu
 
Ndiyo maana wengine mambo ya kitanda hakizai haramu hawawezi.
 
  • Kicheko
Reactions: I M
Sasa aliruhusu vipi wakajitambulishe?? Kama sio mhusika
Sio aliruhusu tu yeye ndio alitaka iwe hvyo, ila mwisho wa siku dada akamkana.
Kama ni kweli ni jambo zuri maana jamaa angeendelea kulea mpaka lini?

kama ndio baba halisi wa mtoto hapo sasa sijui.
 
Siwezi kuiacha hiyo power ya kuujua ukweli kuhusu mtoto ibakie mikononi mwa Mwanamke halafu mimi nibaki naishi kwa imani. Hiyo ni kwa wasiojielewa pekee.
Mimi siyo mtu wa imani, bali knowledge, siku zote natafuta knowledge.
Kwenu nyie waumini ambao imani pekee inatisha ndiyo mmaweza mkaendelea kuaminishwa hadi kwenye mambo sensitive yanayogusa vizazi vyenu

Hizi case zimekua nyingi sana ni bora kupima mapema.
 
Mhh! Hii dhambi ya kudanganya baba wa mtoto iniepuke.

Hao niliofanikiwa kuwajua, kuna uwezekano wapo na wengine ila sio wa karibu mimi kuwajua.
Ukweli ni mzuri hata kwa watoto huko mbeleni.
 
Back
Top Bottom