Baba Mzazi wa aliyekuwa Spika wa Uganda asema mwanaye alipewa SUMU iliyosababisha kifo chake

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Nathan Okori ambaye ni Baba mzazi wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah amesema Mtoto wake (Spika Jacob) alipewa sumu ambayo ndio imesababisha kifo chake.

Mzee Okori ametoa kauli hiyo leo wakati wa shughuli za mazishi ya Spika Jacob.

"Sitaki niomboleze na kulia kwa ndani tu nataka kuweka ukweli wazi, Jacob alipewa sumu, aliniambia kabla hajafariki, sumu ile iliathiri afya yake sana na wakati anasafirishwa kwenda nje ya Nchi (Marekani) kwa matibabu tayari walikuwa wamechelewa na hakuweza kupona," amesema mzazi huyo.

Jacob alifariki dunia Machi 20,2022 nchini Marekani alipokuwa akipatiwa matibabu.

PIA SOMA:
- Jacob Oulanyah, Spika wa Bunge la Uganda afariki dunia

Source: Eagle
 
Nianze na ombi Mode naomba Uzi huu usiuunganishe na ule wa Job maana huu una maspika wawili mmoja wa Uganda inasemekana amefariki baada ya kulishwa SUMU!

Pamoja na Spika wa Tanzania aliyejiuzulu.

Tuanze kwa huyo wa Uganda, ukipitia kwenye mitandao utakutana na kauli hii ya spika wa Uganda alilishwa SUMU, na aliyetoa taarifa hiii ni Baba ake Mzazi namnukuu: "Siwezi kuomboleza kiundani, aliyelala hapa ni mwanangu na amefariki kwa kulishwa SUMU."

Anaongezea kuwa marehemu mwanae alimjulisha kuwa amelishwa sumu, na ilimuumiza sana hata serikali ilipokuwa ikimpeleka hospitali za nje tayari alisha athirika sana na hasingeweza kupona.

Je, kwa nini walimlisha sumu? Najua JF hapa ni pahala sahihi sana najua naweza pata. Majibu ya hili swali.

Je, Yu wapi Job Ndungai? Nimejiwa na wasiwasi maana Spika wa Uganda sikuwahi sikia akiwa na mgogoro na mtawala ila huyu wetu alikuwa na mgogoro na utawala, je uko aliko kupo salama kiasi gani huko?
 
cheza na kitu kingingine usicheze na ndugai
 
Siku nyingine jaribu kuandika vizuri ili ueleweke
 
Una hoja japo uandishi wako unatatiza kidogo.

Hili la Job nadhani mpaka limefika bungeni, na wahusika pale mjengoni naona wanatoa majibu ya rejareja alipo mgogo.

Hii ina maana gani?

Job yupo kizuizini, Job anatumikia adhabu kama ilivyopangwa, Job amekumbana na Karma, Job ni mgonjwa, tukumbuke ndiye mgonjwa ghali kuwahi tokea tangu Tanganyika iumbwe, Afya yake ipo mikononi kwa Authority.
 
Sasa ni nani kweli sisi watz tujibu Kama tupo nchi ya Uganda?

Ajabu kuna watu watajibu as of wanaishi mitaa ya kampala
 

Yuko wapi Ndugai? Hilo ni swali la msingi lenye kuhitaji majibu.
 
Mkuu umeandika kimamlaka Sana Asante kwa TAARIFA!!!
 
Yule speaker aliingia kwa mgongo wa museveni alikuwa chawa wake kwelikweli hadi aliwahi mfananisha mu7 na Yesu itakuwa kundi la kina kadaga speaker wa zamani
 
Kwa Job Dunia ni duara kwakweli,aliyekuwa anawaambia watu wazima kachini,toka nje askali towa huyo alaka, daa sasa yeye kajificha kichaka gani!!!
 
wamuhoji vizuri waliekua amegombea nae usipika inakuaje awe waziri na mbunge na hajawahi hudhuria vikao vya bunge au yeye alijiongezaga yaleyale unatongoza mke wa mwezako mwezako huyohyo anakugongea mkewe kabla wewe bado kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…