Hiyo habari ukiisoma kwa makini ina utata. Aya ya kwanza binti anasema Baba amekuwa akimlazimisha kuwa na mahusiano kwa muda mrefu tangu mama yake afariki.
Binti alikuwa anasoma Iringa, inaonyesha mama wa binti alifariki mwishoni mwa 2008. Kama Baba mzazi alikuwa ameanza kumdenda mwanae kwa muda mrefu, ilikuwaje binti akakubali kulala na baba yake kitanda kimoja na huku akijua kwamba baba amekuwa akimdenda? Hivi kweli binti wa F2 anajua kila kitu na anajua madhara ya kulala kitanda kimoja na mwanaume anaemdenda, bado alikubali kulala na baba yake kitandani? Hivi hakukuwa na mikeka ama virago vya kulalia ili atandike chini alale kwa amani?
Kama stori ni ya kweli basi binti nae amechangia katika hilo tendo kufanyika. The moment alipoanza kudendwa na baba yake alitakiwa atimke bila kuangalia nyuma na kwenda kuripoti kwa ndugu zake. Sasa kwenda kusema kwa ndugu wakati maji yameishamwagika wala haina msaada wowote, ni kujitia aibu yeye mwenyewe. Maana akina Keil (wadadisi) wako wengi watamhoji ilikuwaje akaachia hali hiyo iendelee kwa muda mrefu na huku akiona mazingira wanayolala yana utata. Alichofanya huyo binti ni sawa na mbuzi kujichanganya kwenye banda la chui na akijua chui anatokwa na udenda wa kutaka nyama ya mbuzi.
Vitendo kama hivi vimekuwa common kwenye jamii zetu, wengine wanadai ni masharti ya waganga wa kienyeji, wengine wanadai akina baba wa siku hawajiheshimu inafika mahali wanatamani watoto wao wenyewe. Kuna mengi sana ambayo yanatakiwa kuchunguzwa ili kuona nini kifanyike ili kuondokana na hali hii. Cases zinazokuwa reported ni chache sana ukilinganisha na wingi wa matukio hayo yanayofanyika kwa usiri mkubwa sana.