Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
Mkizisikia tena nyimbo za nani kama mama msizime runinga abadani wala kupunguza sauti ya redio, bali ngojeni hadi ubeti wa mwisho tusikie angalau huenda baba nae atatajwa.
Na hata asipotajwa basi msimdhihaki mtunzi huenda kwake alilisifu tunda zuri na tamu, lakini hakuona juhudi za mti uliopambana kustahimili jua, mvua, ukame na upepo ili tu kutoa tunda hilo zuri.
Methali za kuwapongeza mama zetu sio mbaya, ila ubaya ni kwamba tutazisikia hadi lini angalau hata na baba nae apate nafasi katika masikio yetu.
Nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba, hata sisi tunaunga hoja ya kutopongeza mapambano ya mzazi wetu wa kiume kisa tu sifa nyingi zenye kumuinua mzazi wa kike.
Msininukuu vibaya, sijasimama hapa kushindanisha majukumu yao wala sijasimama hapa kupima uzito wa baba na mama, tena sijasimama hapa ili kuwakataza kuitikia kibwagizo cha 'nani kama mama'
Ila nimesimama hapa kuwakumbusha kuwa katika nyimbo zenu nyingi za sifa za mama, basi tengeni angalau ubeti mmoja kumkumbuka yule aliyewatafutia huyo mama.
Yule ambae alipambana sana kwa ajili yetu maana faraja yake ilikuwa ni kutuona sisi watoto wake tukipendeza na kuishi vizuri mbele ya macho ya kila mtu.
Sasa ikiwa ninyi mna historia tofauti na sisi basi kila mtu kwanzia sasa ataimba nyimbo zake. Sisi tunahitaji angalau tupate nafasi ya kuimba nyimbo za baba. Baba zetu wapambanaji, baba zetu ambao wapo radhi kutukinga na jua ili wao waungue sisi tupate kivuli.
Baba zetu ambao wanalala ili kupambazuke na wala si ili wapumzike. Baba zetu wenye mioyo ya mishumaa, yani wanateketea wao ili tu kutupa mwanga sisi.
Suruali anayoivaa baba, hakuna yeyote inaemtosha. Majukumu yake ni mazito, kwani ni mara ngapi umeshuhudia bakuli ya baba ilikijazwa mboga nyingi sababu nafasi yake ni pengo kubwa lisilozibika hata kwa meno ya ndovu.
Baba ni nguzo imara zaidi ya mnara wa babeli, na ndio maana nguzo hii inapodondoka basi familia ni lazima itetereke.
Mungu awajaalie maisha marefu baba zetu wote mlio hai, lakini pia awarehemu baba zetu waliotangulia mbele ya haki. Hakika mchango wenu ni mkubwa, tunathamini na kujali juhudi zenu. Ni sisi tu wachache, wema, tunaojielewa tumeamua kuimba nyimbo yenu, wale wenzetu waliobaki wamekataa kabisa.
Wenu katika kalamu [emoji2398] Amani Dimile [emoji1607]
#amanidimile #misemo_ya_hekima #baba #mpendwababa #tungomaridadi #fikrazadimile