Baba wa Diamond atoa baraka kwa mjukuu wake mpya

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Akiongea na kipindi Cha Shilawadu cha clouds tv,Mzee Abdul Nasibu baba mzazi wa diamond ametoa baraka zake zote kwa mtoto wa Hamisa Mobetto ambae inasemekana amezaa na Diamond na kupewa jina La baba mzazi wa Platnumz Abdul Naseeb.

Mzee Abdul Amesema yeye kama Mzazi anaona mwanae Diamond hajafanya kosa lolote kuzaa na Hamisa kwani yeye ni mwanaume na anaweza kuzaa na kuoa wanawake zaidi ya mmoja kwani dini inamruhusu,ameendelea kusema hali ya kuzaa na mwanamke zaidi ya mmoja sio mpya inatokea kwa watu wengi,

kwa vile Diamond ni mtu maarufu ndio maana imekua gumzo,hata hivyo amemtaka Diamond awaoe wote Zari na Hamisa ili kujiepusha na kuzini kwani kwa sasa anazaa hovyo bila ndoa ambapo dini hairuhusu.

Akijibu Swali alilouliza kama Kati ya wajukuu zake Tiffa,Nilan na Abdul atampenda yupi,Baba Diamond Aemesema atawapenda wote kwa vile ni wajukuu zake ila anatoa shukrani za dhati kwa Hamisa kwa kumkumbuka kwa kumpatia mwanae jina lake hii inaonyesha wana upendo kwake.

Mwisho Baba wa Msanii Diamond amemtaka Mwanae afanye hima atoe urithi kwa watoto wake wote watatu kwa kuwa ana mali nyingi.
 
Dunia ya sasa maadili yamekwisha kabisa,yaani badala ya baba mzazi wa kijana atoe onyo kwa kijana wake kuhusu tabia yake mbaya ya uzinzi na kuzaa zaa hovyo na wanawake ambao hajawaoa na uwezo wa kuwaoa na kuwatunza anao yeye ndo kwanza anabariki uchafu unaofanywa na mwanae.na hii yote inatokana na ukweli kwamba kijana ndiye anaempa maisha mzee ndo mana anaogopa kumkanya anaogopa akienda against nae atamwaga mboga.

sent from my Infinix S2 Pro using JamiiForums mobile app
 
Huyu Mzee siyo mzima, kwani mwanae kamuambia kuwa ana mtoto mwingine?Mimi kama baba ninge comment pale mwanangu anaponiambia baba nna mtoto mwingine, diamond hajakubali bado ningemuongeza mwaka mmoja wa Kusota na maisha yake na huyo biiiitch angeisoma namba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimae mzee abdul baba mzazi wa diamond platnumz amejitokeza hadharani na kuonyesha kufurahiswa na kitendo cha mkwewe hamisa mobeto kumwita mtoto wake aliezaa na diamond platnumz jina lake, kama vile haitoshi mzee abdul kamsifia mwanae kwamba hivo ndivo inavotakiwa kufanywa ukizingatia diamond ni mtoto wa kiislam na dini yake inamruhusu kuoa mpaka wake wanne, kapendekeza awaoe wote zari na hamisa kwa kua uwezo wa kuwahudumia anao.

haya wale wazee wa mapovu mambo yanazidi kumwedea vyama hamisa, naona wazazi wa diamond wote wanamkubali.

USHAHIDI HUU HAPA:

 
ameacha kulilia matunzo, sasa anafurahia jina. hahahahaha anaona dalili za kukumbukwa
 
Ivi Yule dogo wa mwisho kwa zari ni wa diamond kweli,..???
 
Hivi hamisa kaona mtoto ndio wa kumpaisha kiumaarufu au chanzo cha mapato. Daah wamama wa siku hizi bure kabisa. Mtoto mdogo hata mwezi hana anatukanwa matusi mazito kisa kutafuta followers wengi na umaarufu khaaa!
 
Hivi hamisa kaona mtoto ndio wa kumpaisha kiumaarufu au chanzo cha mapato. Daah wamama wa siku hizi bure kabisa. Mtoto mdogo hata mwezi hana anatukanwa matusi mazito kisa kutafuta followers wengi na umaarufu khaaa!
Hivi kumbe huwa una adabu kiasi hiki..!
 
Huyo binti ni mpuuzi
Umejibebesha mimba ya singleboy mtoto wa kwanza baba kakukacha.
Unafungua tena uzazi unazaa na mwanaume mwenye familia ambayo ulimwengu mzima unaijua, baba anakukataa wewe na mtoto unangangania na kulazimisha utambulike
Kama alishindwa kumstiri yule aliyekuwa free ataweza kustiriwa na huyu mwenye familia??

Anajitengenezea mazingira ya kuchina na kuwa nungayembe.
Nani atakubali kubeba/kuoa mama wa watoto wawili wenye baba tofauti???
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…