Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,469
- 12,391
Akiongea na kipindi Cha Shilawadu cha clouds tv,Mzee Abdul Nasibu baba mzazi wa diamond ametoa baraka zake zote kwa mtoto wa Hamisa Mobetto ambae inasemekana amezaa na Diamond na kupewa jina La baba mzazi wa Platnumz Abdul Naseeb.
Mzee Abdul Amesema yeye kama Mzazi anaona mwanae Diamond hajafanya kosa lolote kuzaa na Hamisa kwani yeye ni mwanaume na anaweza kuzaa na kuoa wanawake zaidi ya mmoja kwani dini inamruhusu,ameendelea kusema hali ya kuzaa na mwanamke zaidi ya mmoja sio mpya inatokea kwa watu wengi,
kwa vile Diamond ni mtu maarufu ndio maana imekua gumzo,hata hivyo amemtaka Diamond awaoe wote Zari na Hamisa ili kujiepusha na kuzini kwani kwa sasa anazaa hovyo bila ndoa ambapo dini hairuhusu.
Akijibu Swali alilouliza kama Kati ya wajukuu zake Tiffa,Nilan na Abdul atampenda yupi,Baba Diamond Aemesema atawapenda wote kwa vile ni wajukuu zake ila anatoa shukrani za dhati kwa Hamisa kwa kumkumbuka kwa kumpatia mwanae jina lake hii inaonyesha wana upendo kwake.
Mwisho Baba wa Msanii Diamond amemtaka Mwanae afanye hima atoe urithi kwa watoto wake wote watatu kwa kuwa ana mali nyingi.