Pascal_TZA
Member
- Mar 25, 2014
- 27
- 76
Baba mdogo wa marehemu Naomi Marijani ambaye aliuawa na kuchomwa moto na magunia mawili ya mkaa, Robert Marijani amesema kuwa kama familia wameridhika na Hukumu iliyotolewa leo na upande wao sasa wanajiandaa kuzika upya mabaki ya mwili wa Naomi, baada ya kesi kumalizika.
Marijani ameyasema hayo leo February 26,2024 alipokuwa akizungumza na baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumuhukumu mfanyabiashara, Khamis Luwongo, kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mke wake Naomi Marijani na kisha mwili wake kuuchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa na lita tano za matuta ya taa na kuchukua majivu pamoja na mabaki ya mifupa yake na kwenda kuyazika katika shamba lake lililopo kijji cha Marogoro, Wilaya ya Mkuranga.
Pia soma > Aliyemteketeza mkewe kwa magunia mawili ya mkaa ahukumiwa Kunyongwa mpaka Kufa
View: https://youtu.be/JLaDS44zq0M?si=TyI6xAeCV8o0nh-R