Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Nimepitia kwenye mitandao nimekuta kuna habari kubwa kumhusu Majaliwa kijana ambaye amevunja vichwa vya habari hapa juzi kwa kuongoza zoezi la kuwaokoa abiria wa ajali ya ndege huko Bukoba.
Baba huyo ametoka hadharani na kudai kwamba pesa ambayo Majaliwa alipewa kama motisha ni ya familia na Majaliwa atawekewa mgao wake. Ameenda mbali zaidi akidai kuwa hali yao ya maisha ni ngumu na wadogoze Majaliwa wanahitaji kusaidiwa kupitia fedha hizo.
Sakata la Majaliwa sasa linachukua sura mpya kutoka kwenye ngazi ya Kitaifa na sasa kuhamia kwenye himaya ya kifamilia ambapo msemaji wa familia ni baba. Msimamo wa baba huyo unaakisi aina ya malezi na desturi ambazo jamii inapaswa kuondokana nazo.