Baba yangu alikaa jela mika 7 kwa kosa la kupiga mwizi

Baba yangu alikaa jela mika 7 kwa kosa la kupiga mwizi

Fufua Tumaini Jipya

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2024
Posts
223
Reaction score
469
Mwaka 2006 - pale Nyumbani Mwanza ilitokea wezi wakaenda kuiba .

Baada ya kuiba wakakamatwa na kuulizwa mmeiba wapi na nani huwa mnamuuzia mkisha iba.

Wale wezi wakasema ni huwa wakiiba baadhi ya vitu huwa wanamuuzia mzee .

Mzee wangu by that time alikuwa anauza duka la Vifaa vya ujenzi.

Ni kweli mzee wangu alikuwa anajenga Nyumba yake so baadhi ya mafundi ujenzi na wapiga dili walikuwa wakiiba wanamletea mzee wangu ananua kwa bei rahisi ili atumie katika Nyumba yake.


Ila kilichotokea ni pale mzee Wangu alipigiwa simu na kuambiwa kuna wezi wamekamatwa na wamesema huwa wanakuuzia Mzigo

Maamuzi aliyofanya mzee Wang u ni kuwaambia wale waliompigia sm wamfate na waje na hao wezi .


So alianza kupiga hao wezi na mwisho waliuliwa na kutupwa ziwani wakiwa ndani ya viloba.

Ni kweli wale jamaa walikuwa wanaiba Ila walikuwa wadokoaji tu sio wezi serious wa kuiba mambo ya maana yaani ni wale wezi ambao ulikuwq ukikaa vibaya anaondoka na kiatu ilimradi wakapate pesa ya kunywa Pombe.

Baada ya vifo vya hao wezi , ndugu zao waliifata mili yao ziwani na baada ya hapo ilipigwa postmortem na kuoneka waliuliwa kikatili.

sasa police wakaingia kazini , mzee wangu akakamatwa akapewa kesi ya mauaji .

Alianza anakaataa Ila walipomchukua Alana za vidole akaonekana alihusika na nikweli alitoa vipigo ngumi vibao n.k

Na mwisho kesi ilitolewa hukumu 2009 na kuukukiwa miaka 7 nyuma ya nondo kwahiyo alikuja kuachiwa au kuwa huru mwaka 2013.

Kwa jambo hili hata mwizi aniibie nawaita police siwezi kuhusika kutoa vipigo maan police wakikuta umeua mwizi wanakubadilishia kibao na unapewa murder case.

NB

Naona watu mnakurupuka kukomenti ilimradi bila kutumia akili.


Hawa jamaa waliouliwa hawakuwa wezi mnaowajua Ila walikuwa wadokozi


Nikisema wadokozi ni kwakuwa walikuwa ni wagata
(wabeba mizigo) hivyo walikuwa wakiiba vitu vidogo vidogo mfano anakuta umeacha sufuria au ndo na yeye hana hela ya pombe Anapita nayo.



So hata walipouliwa ilizua taharuki kwakuwa zamani miaka ya 2006 police walikuwa wapo makini achana na hawa polisisiemu wa sasa.



So mob justice is hell nigga - mzee wangu ata asingewaua bado kulikuwa hamna ushahidi wa yeye kuuziwa vitu na hao wezi kwakuwa vitu vyenyewe ambavyo walikuwa wakimuuzia ni one time one time


Kwa wale makuli mnaelewa kuwa wakienda kubeba mizigo wanaiba kimtindo mfuko mmoja wa Cement baadae wanauza.


so Ila siku ya tukio hawa wezi hawakuiba katika sehemu za kubebea mizigo Ila walianua nguo na kwenda kuziuza katika virabu vya pombe na hatimaye kuuliwa
 
Baba yako alikuwa akifadhili matukio ya kihalifu na muuaji.
Amepata hukumu isiyostahili.
Alitakiwa angalau miaka 30, hata hivyo tushukuru Mungu mzee wako ana zali.
Poleni sana.
Usije fanya kitu kama hicho kwenye maisha yako.
 
Tanga ukiiba habari yako kwisho ,polisi wa huko ni tatizo ,wakija wakimkuta mzima wanasema '' tunataka maiti ''

Kile kipigo cha Mwakinyo ni rasha rasha ,kuna mitaa kama Mabovu waliandaa kampeni ya kutokomeza wezi ..Ndani ta miaka miwili kulikuwa peupe ,waliobaki walikimbilia South Africa.


Huruma sio malezi.
 
Asingekuwa mbwa wangu labda ningekuwa na kesi ya mauaji maana hasira nilizokuwa nazo, sijui ingekuaje.

Kuna siku mwizi ameruka ukuta akiwa ananyata hana hili wala lile, kumbe nilishamuona na nimejipanga kukabiliana nae.
Kwakuwa nilikuwa nimeshawahi kuibiwa sana basi nilikuwa na hasira sana na nilitaka nimalizane nae bila kelele kabisa kwakuwa nilikuwa mwenyewe mazingira yale, basi akiwa ananyata hajui kama na mimi namnyatia ili tukutane. Bahati mbaya mbwa akabweka kule bandani kitu kilichoondoa utulivu yule kibaka alibadili plan kurudi alipotoka ikabidi kumkurupusha akawahi kukimbia nikamkosa.
 
Baba yako hakuwa anawapiga kama wezi. Baba yako aliwapiga na kuwauwa akikusudia kupoteza ushahidi wa uhusika wake katika maovu.

Kumbuka baba yako alikuwa anashirikiana na wezi akijua ni wezi kwahyo naye alikuwa mwizi. Wenzie walivyonasa akaamua kuwauwa.

Kimsingi baba yako alicomit first degree murder na alipaswa kuhukumiwa kunyongwa.
 
Back
Top Bottom