Baba yangu ameingia chumba cha upasuaji dua zenu nyote

msumeno

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2009
Posts
2,826
Reaction score
1,734
Waungwana baba yangu, baba yenu wengi wenu ni babu yenu mida hii ya saa kumi kaingizwa chumba cha upasuaji hapa hospitali ya Namanga Tegeta.

Nakuombeni sana dua zenu atoke salama ili hatimae arudi nyumbani Tabora akiwa mzimaa na kuugana na familia yake Insha Allah Ameen
 
Mungu ni Mwema
Atafanya kila jambo kuwa jepesi na hatimaye Baba kufanyia upasuaji vizuri ili aweze kurudi kwenye hali yake ya awali ya uzima .
 
Mungu ajaalie ili kila kitu kiende salama ili afya yake irudie kama ilivyokuwa awali.
 
Mungu muumba asimamie hili kama ambavyo kawezesha mengi na magumu!
Aamin
 
Nina wafunika wote ndani ya chumba cha upasuaji kwa damu ya Yesu, wafanye kazi yao kwa uongozi wa Roho mtakatifu na kufanikiwa katika upasuaji na mgonjwa kutoka salama. Jina la Bwana libarikiwe. Amina
 
Mungu atakuwa upande wake na atatoka salama
 
InshaAllah kwa uwezo wake mola kila kitu kitaenda sawa.....malaika wema wasimame kila kona
.usisahau kutuletea taarifa anaendeleaje baba angu
 
Mungu yupo kazini sasa, baba atatoka salama kabisa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mwenyezi Mungu amponye na amjalie maisha marefu ya afya njema na furaha
 
Inshallah kwa rekma za Allah baba atatoka salama na shughuli itaendelea salama
 
Mungu ni mwaminifu kwa kila jambo.amjalie uponyaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…