Plot4Sale Baba yangu anauza kiwanja chake, amekwama anahitajika akatibiwe

Plot4Sale Baba yangu anauza kiwanja chake, amekwama anahitajika akatibiwe

Hiyo ni Madale karibu na kwa Mzee Kawawa...
ila kuhusu ukubwa wa eneo na bei yake ni km Ardhi na Mbingu..
Angalizo..
Wanunuzi wa hilo eneo wawe zaidi ya makini...
Unaweza ukasema kwa urahisi kwa kuwa hayajakufika, uhai wa mtu ni bora zaidi.
 
Ukubwa wa kiwanja chote ni heka 2, lakini kulingana na dharura tunauza heka moja, ndio bei niliyoitaja.
Poleni sana ndugu MTU chako kikufaacho wakati wa shida,afya ni muhimu kuliko mali Mola atamfanyia wepesi Mzee atakuwa sawa tu
 
Shida ya dhamana inataka marejesho je uwezo wa kurejesha upo? Km upo ni vyema kuweka dhamana
 
Muuzaji naomba nicheck PM tafadhali tuongee na hilo eneo mnafahamiana na majirani wa hapo au??Na katika mchoro wa ardhi hicho kiwanja kipo kwenye viwanja vya watu wa makazi au??
 
Mwenye tatizo la namna hiyo hawezi kuuza kwa bei hiyo.
Soma majira kiongozi.
Muombe sana Mungu wako, ili haya yote yasikukute.
Katika mazingira haya si vizuri kuandika chochote kama hakina tija.
Ulitaka aandike shs ngapi? Je wewe unaweza kuimudu hata hiyo 20m?

Fikiria kabla ya kuandika, ila kama unajifunza kupost JamiiForums basi sawa. Mungu wako akusamehe
 
People stukeni, yawezekana ni kweli jamaa yetu ana uguza, ila kwa maeneo hayo, halafu kwenda moja kwa moja kwamba unauza heka moja milion 20, napata wasiwasi. Je mleta Tangazo, ulishawai kutangaza kwamba unauza hicho kiwanja, lets say kwa gharama hiyo hiyo milion 20, bila kuainisha kwamba Mzee wako anaumwa halafu ukakosa mteja? Watu wengi wamekuwa na doubt kutokana na maelezo mengi uliyoandika, kiwanja ni kikubwa na ni kizuri, am sure ungeandika tu kwamba kinauzwa hata milion 25, bila kuweka hayo maelezo mengine ungepata mteja. Kuweni makini wana JF

[HASHTAG]#TooGoodToBeTrue[/HASHTAG]
 
Sipo kusingizia ugonjwa wala kitu chochote, hiyo ni bei ambayo tumekaa kama familia tukaamua kuuza kwa milioni 20, uzuri kiwanja hakina mgogoro wowote, kina nyaraka zote muhimu, majirani wanafahamu hata kwenye ngazi ya serikali za mitaa.

Mtu yoyote yupo huru kuuza kitu chake kwa bei yoyote, baba yangu mzazi anaumwa na nikaona niweke wazi hasa kutokana na maradhi yanayomtesa, ukija kufikwa na hali kama hiyo alafu hauna kitu nadhani ungeweza kuafikiana na hiki nachokisema.

Ila kama unaweza kutusaidia kununua kwa bei ya millioni 25 kama uliyoitamka, tutashukuru pia mkuu.
 
Back
Top Bottom