Babu: Kichuya achana na mademu mwanangu

Babu: Kichuya achana na mademu mwanangu

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Babua wa Mchezaji Shiza Ramadhani Kichuya amemtaka mjukuu wake kutobweteka na starehe za mjini ikiwemo ulevi na wanawake na awazie kuwekeza kwenye ardhi kwenye pesa anayopata kutokana na nyota yake ya sasa Kung'aa Simba

=======

BABU wa Winga wa Simba, Shiza Kichuya, Mzee Ibrahim Mohamed ‘Mzee Mangwende’ amemtaka mjukuu wake kuwekeza kwenye ardhi hasa kwa pesa zake anazozipata akiwa Simba na kukaa mbali na starehe ikiwemo ulevi na wanawake.

Kichuya aliyesajiliwa Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar nyota yake imeng’aa kutokana na mchango wake kwenye kikosi hicho huku akifikisha mabao saba na kuwa kinara wa ufungaji.

Kichuya amekuwa kipachika bao katika kile mechi anayocheza huku bao la mwisho alilifunga juzi Jumamosi walipocheza na Kagera Sugar huku yeye akiwa ametoka kwenye majeraha ya kifundo cha mguu alichoumia wakati wa mechi ya Mbeya City ambayo pia alifunga.

Mzee Mangwende aliliambia Mwanaspoti kuwa mjukuu wake ana kipaji kikubwa ila anahofia kuharibika na starehe za mjini huku akisisitiza kuwa anataka awekeze zaidi kwenye ardhi.

“Kichuya hana tabia za starehe za ulevi wala wanawake ila sasa siwezi kujua huko mjini kama atabadilika ama lah ila sifikirii kupata mabadiliko yoyote. Nimemwambia mambo mawili kuwekeza kwenye ardhi japo awe na kiwanja cha kujenga nyuma yake.

“Nimemlea ila sina ardhi ya kumrithisha na nyumba nina hii tu, hivyo sasa hivi ameanza kupata mafanikio anatakiwa kwa kidogo apatacho awekeze sehemu ambayo ataweza kujenga nyumba ili hata akiachana na mpira awe na mahali pa kuishi,” alisema Mzee Mangwende.

Mwanaspoti
 
Akiwaendekeza hao kona atakuwa anapiga kama goal kick. Maana wanamaliza grease kwenye magoti.
 
Asiendekeze mademu ila aongeze juhudi zaidi katika mazoezi ili afanye vizuri zaidi na kuhitajika kimataifa. Wengi walioendekeza stare katika sanaa na michezo wameshindwa kufikia malengo
 
Afadhali amepata mshauri mapema mana huwa tunajisahau sana.
Huko baadae asijesema sikujua.
 
Wachezaji wa kibongo huwaga hawana malengo makubwa, wao wakishapata kuchezea Simba au Yanga tayari wameshamaliza malengo yao.
 
Amshauri aoe apate Kidude cha halali kwa kuwa haiwezekani aishi bila ya kuch kuch kotae!
Ni sawa na kukataza watu kuchimba dawa njiani wakat hujaweka Vyoo!
 
Ajibu na kelele zote hajawahi kufikisha magoli kumi kichuya akijitahidi 14...na hana uwezo wa hat trick
 
Amshauri aoe apate Kidude cha halali kwa kuwa haiwezekani aishi bila ya kuch kuch kotae!
Ni sawa na kukataza watu kuchimba dawa njiani wakat hujaweka Vyoo!
Hajamwambia asifanye amemwambia asiendekeze...jaribu kutofautisha...
 
Kuendekeza inahesabukaje? Mara moja kwa wiki, siku au Mwezi? Au Demu mmoja wawili au watatu
umeolewa au umeoa? nisije kuta navinja sheria za nchi naomba jibu ukiweka na umri wako itasaidia zaidi...
 
umeolewa au umeoa? nisije kuta navinja sheria za nchi naomba jibu ukiweka na umri wako itasaidia zaidi...

Elewa kuwa Zinaa ndio chanzo cha kushuka kiwango mchezaji sio tendo la ndoa!

Kuna Wachezaji wameoa na wanakula Mzigo daily na nchi zenye soka la kulipwa hakuna Mambo ya kuweka Kambi kabla ya Mechi na bado wana perform vizuri.

Zinaa ni uchafu Ila tendo la ndoa ni tulizo
 
Elewa kuwa Zinaa ndio chanzo cha kushuka kiwango mchezaji sio tendo la ndoa!

Kuna Wachezaji wameoa na wanakula Mzigo daily na nchi zenye soka la kulipwa hakuna Mambo ya kuweka Kambi kabla ya Mechi na bado wana perform vizuri.

Zinaa ni uchafu Ila tendo la ndoa ni tulizo
Eti wanakula mzigo daily...bado hujajibu maswali yangu umeoa/umeolewa? umri wako? nani aliyekwambia ukiwa umeoa tushirikibtendo la ndoa daily... huko ndiyo kuendekeza sasa...
 
Ukishangaa ya Babu yake na Kichuya.. Utayaona ya Paul Pogba!!

£100m Manchester United star Paul Pogba has kept guests at a posh hotel awake with ‘loud sex moans’

Namnukuu jamaa aliokua akikaa karibu na chumba cha Pogba..
"The first time I heard the sex noises was between 1am and 2am the following morning.
"I could also hear them on the nights of September 27, 28 and 30 - on that occasion as late as 4am.
"If it wasn't loud music from his room it was loud moaning.
"The music was as annoying as the sex because it was vulgar hip hop.

Huyu mwingine.. alikua na haya..
"I checked out on September 30. I will never go back to that hotel again."
“The next morning they left the hotel in separate cars.
“We thought it would be a one-off.
“But two days later same thing happened, with loud music heard until late, even ahead of a Manchester United game.
“The night after the game the same thing happened.
“There was loud music and at 2am and lots of friends there.
“And moments later the moanings started again. This time it was louder than ever.
“It sounded as if there was wild sex going on in there. It lasted for two hours."

Source; £109m Manchester United star Paul Pogba has kept guests at a posh hotel awake with 'loud sex moans'

Nakala; kibwenzi Crashwise Pohamba Ngamiani PATO8221 samsun feitty supermarket suudy muhomakilo jr Bigbootylover Amavubi Ngamiani
 
Back
Top Bottom