Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258
Babua wa Mchezaji Shiza Ramadhani Kichuya amemtaka mjukuu wake kutobweteka na starehe za mjini ikiwemo ulevi na wanawake na awazie kuwekeza kwenye ardhi kwenye pesa anayopata kutokana na nyota yake ya sasa Kung'aa Simba
=======
BABU wa Winga wa Simba, Shiza Kichuya, Mzee Ibrahim Mohamed ‘Mzee Mangwende’ amemtaka mjukuu wake kuwekeza kwenye ardhi hasa kwa pesa zake anazozipata akiwa Simba na kukaa mbali na starehe ikiwemo ulevi na wanawake.
Kichuya aliyesajiliwa Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar nyota yake imeng’aa kutokana na mchango wake kwenye kikosi hicho huku akifikisha mabao saba na kuwa kinara wa ufungaji.
Kichuya amekuwa kipachika bao katika kile mechi anayocheza huku bao la mwisho alilifunga juzi Jumamosi walipocheza na Kagera Sugar huku yeye akiwa ametoka kwenye majeraha ya kifundo cha mguu alichoumia wakati wa mechi ya Mbeya City ambayo pia alifunga.
Mzee Mangwende aliliambia Mwanaspoti kuwa mjukuu wake ana kipaji kikubwa ila anahofia kuharibika na starehe za mjini huku akisisitiza kuwa anataka awekeze zaidi kwenye ardhi.
“Kichuya hana tabia za starehe za ulevi wala wanawake ila sasa siwezi kujua huko mjini kama atabadilika ama lah ila sifikirii kupata mabadiliko yoyote. Nimemwambia mambo mawili kuwekeza kwenye ardhi japo awe na kiwanja cha kujenga nyuma yake.
“Nimemlea ila sina ardhi ya kumrithisha na nyumba nina hii tu, hivyo sasa hivi ameanza kupata mafanikio anatakiwa kwa kidogo apatacho awekeze sehemu ambayo ataweza kujenga nyumba ili hata akiachana na mpira awe na mahali pa kuishi,” alisema Mzee Mangwende.
Mwanaspoti