Atukuzwaye
Senior Member
- Oct 5, 2026
- 191
- 250
Mtoto asimulia namna anavyodai kubakwa na mzee wa miaka 65 tangu akiwa chekechea Arusha. Mtoto wa miaka 10 anayesoma darasa la nne, mkazi wa Mtaa wa Kaloleni Mashariki, Kata ya Kaloleni, Wilaya ya Arusha Mjini, amesimulia mwanzo hadi mwisho namna anavyodai kufanyiwa vitendo vya ubakaji na mzee mwenye umri wa miaka 65, akieleza kuwa vitendo hivyo vilianza tangu akiwa chekechea.
Tukio hilo lilidaiwa kugundulika Oktoba 22, 2025, majira ya saa moja jioni, baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa akienda dukani kumkuta mzee huyo akiwa amevaa boksa pekee ndani ya geti la nyumba yake, huku akimwamuru mtoto huyo ainame chini ili asionekane na watu.
Mwanamke huyo aliposhuhudia hali hiyo, alimwambia mtoto akimbie. Baadaye alimfuata nyumbani kwao na kumuuliza kuhusu tukio hilo, ndipo mtoto alipofunguka na kueleza kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo hivyo tangu akiwa chekechea hadi sasa anaposoma darasa la nne. Kwa mujibu wa maelezo ya mtoto, mtuhumiwa alikuwa akimlazimisha kufanya vitendo vya kingono ikiwemo kumuwekea uume wake mdomoni na kumtaka kumeza majimaji ya uzazi.
Akizungumza na Kusaga TV leo Novemba 2, 2026, majirani wa eneo hilo wameeleza kusikitishwa na tuhuma hizo, wakidai kuwa wamefuatilia suala hilo katika ngazi mbalimbali za uongozi ili hatua za kisheria zichukuliwe. Majirani hao wamesema mzee huyo alikamatwa, lakini baadaye walimwona akiwa mtaani. Wamehoji mwenendo wa suala hilo na kutaka mamlaka husika kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zilizochukuliwa. Kwa upande wake, Mtendaji wa Mtaa amethibitisha kuwa taarifa za tukio hilo zinafahamika na kwamba uongozi umelishughulikia kwa upande wake, huku suala hilo likiachwa kwa vyombo vinavyohusika kuendelea na taratibu za kisheria.
Jeshi la Polisi limekuwa likisisitiza ushirikiano na wananchi katika kupambana na ukatili dhidi ya watoto, pamoja na kutoa elimu ya kutambua, kuzuia na kuripoti vitendo hivyo ili kulinda haki na usalama wa watoto.