Babu Seya kujaribu tena Jumatano

Babu Seya kujaribu tena Jumatano

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Jumatano ya tarehe 12/2/2014 itakuwa ya kipekee kwa Mwanamuziki Nguli nchini Mzee Nguza Viking alias Babu Seya. Ni siku ambayo yeye na mwanaye watasimama mbele ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kuomba marejeo ya hukumu dhidi yao iliyotolewa na Mahakaa ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuthibitishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Itakapokaa kama Dawati Kamili (Full Bench), Mahakama ya Rufani ya Tanzania inasikiliza na kutolea maamuzi Marejeo yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Babu Seya na Mwanaye ambayo,kimsingi, yanalenga kupinga kukutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Nyaraka za kimahakama zinaonesha kuwa Babu Seya na Mwanaye watatetewa na jopo la Mawakili litakaloongozwa na Wakili Msomi maarufu nchini, Mabere Nyaucho Marando. Ili kupata uchambuzi wa kina wa kisheria unaoizunguka kesi hiyo, yaani ushahidi na sheria iliyotumika kama ilitafsiriwa ipasavyo, Mahakama ya Rufani imewaalika Wanazuoni watatu kama Marafiki wa Mahakama(Amicus Curiae) akiwemo Mkuu wa Shule Kuu ya Sheria,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Profesa Boneventure Rutinwa.

Babu Seya na mwanaye wanaendelea na mapambano.Kudai haki zao za kuwa huru.Ya kudai kutendwa kwa haki. Ya kudai kukosewa kwa kukutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Wanaendelea kupambania utu wao.Wanaendelea kupambania utawala wa sheria. Kuujua ukweli.Watafanikiwa??? Majibu ni Jumatano ya tarehe 12/2/2014.

Mengi yanafuata.......!!!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
kama rufaa isingekuwa na ukomo wa muda, basi tungesema wasubiri awamu ya 4 ipite ili waje kujitetea awamu ya 5 yaani rais mwingine
 
Back
Top Bottom