Babu Seya, Papii Kocha wamlilia JK

Babu Seya, Papii Kocha wamlilia JK

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Wanamuziki Nguza Viking na Papii Kocha wanaotumikia kifungo cha maisha jela, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete awasamehe kwa makosa waliyofanya.

Nguza na mwanaye Papii walitoa ombi hilo kupitia wimbo wakati wakitumbuiza katika maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Chuo cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.

Ombi hilo waliliwasilisha kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambapo Nguza maarufu Babu Seya na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha), walitumbuiza wakiwa na Bendi ya Wafungwa. Walimwomba Waziri Chikawe kufikisha ombi lao kwa Rais Kikwete.

Babu Seya na Papii Kocha walitoa burudani hiyo huku wakighani mashairi yenye ujumbe wa kuomba Rais awasamehe, hali iliowafanya mamia ya watu waliofurika kwenye hafla hiyo kutulia kimya, wengine wakilengwa na machozi.

Akiimba huku akitabasamu, Papi Kocha alikuwa akionyesha mikono ya kuomba msamaha na kusema: “Kosa gani sisi tusilosamehewa; vifungo vya maisha, miaka 30 gerezani havifundishi.”

“Waziri Chikawe tunaomba umfikishie Rais Jakaya Kikwete ombi letu, mwambie atusamehe. Hata Petro alimkana Yesu mara tatu, lakini Yesu alimsamehe kwa nini sisi….,” alisikika akiimba Papi Kocha na baadhi ya wananchi waliohudhuria uwanjani hapo wakiinamisha vichwa chini na wengine kutokwa na machozi.

Akijibu ombi hilo wakati akiwahutubia wananchi Waziri Chikawe alisema: “Nimesikia maombi yenu, yamefika na nitajitahidi kuyafikisha kwa Rais Kikwete.”

Chikawe akijibu ombi hilo alisema “Mtu akishatumikia kifungo kwa miaka saba au 10 gerezani nina hakika kama ana moyo na nafasi ya kuacha, atakuwa amebadilika hivyo anaweza kupewa msamaha.”

Baadaye Chikawe alitembelea mabanda ya maonyesho na Bendi ya Wafungwa ikipewa tena nafasi ya kutumbuiza. Babu Seya aliimba wimbo maarufu wa ‘Seya tucheze wote’ na umati wa watu kutoka kwenye mabanda ya maonyesho na kumiminika jukwaani kucheza wakiwamo askari magereza na wakishangilia jambo lililowafanya askari kuzuia bendi hiyo kuendelea kutumbuiza.

Awali, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Minja alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na Magereza katika kutekeleza majukumu ya jeshi hilo.
Chanzo mwananchi
 
Kipaji kinachopotea,papii the best rapper kwa upande wangu,hope watasamehewa,inaniwia vigumu kuamini kama kweli baba na mtoto mfanye kwa pamoja ubakaji ila ndio hivyo tena.
 
Dah Pole zao sana!
hivi whats behind this story?
nini kilitokea plz...
 
Duh hawa wafungwa wameomba sana ni wakati sasa wa JK kuwasamehe kwa mujibu wa katika kama aliweza kuwasamee wezi waliokwapua fedha za EPA hata hawa anaweza kuwasamee.
 
Kwa huu mkasa no coment!
Maana muomba na muombwa msamaha wanafahamiana,hivyo nikiweka data zozote kuna uwezkano wa jamaa akapanic na msamaha ikawa ni ndoto kwao.
 
Waondoe mzizi wa fitna . Waite waandishi wa habari huko jela . Waitangazie nchi kupitia hao waandishi wa habari . Na wakiri makosa yao ya kubaka . Na waeleze dhumuni lao hasa lilikuwa nini . Kama ni burudani au mambo ya uganga. Then wawaombe msamaha watanzania wote pamoja wazazi pamoja na hao watoto waliofanyiwa ubakaji. Hiyo itaondoa utata wote wa kumtuhumu rais na bla bla zote. Baada ya hapo kama watasamehewa sawa na hata kama hawatasamehe sawa. Lakini utata utata utakuwa umeisha
 
Dah Pole zao sana!
hivi whats behind this story?
nini kilitokea plz...

Tafuta wimbo wao wa
"SALIMA"

Usikilize vizuri sana ndio tatizo

Nakupa kidogi tu

"oho! salimaaaaa
haaaasas x 2
nilikudanganya ukamuacha yeye....."

Ila UWT wakatengeneza watoto wao eti wamebakwa....ahaaaaa!
 
Duh hawa wafungwa wameomba sana ni wakati sasa wa JK kuwasamehe kwa mujibu wa katika kama aliweza kuwasamee wezi waliokwapua fedha za EPA hata hawa anaweza kuwasamee.

Niki eat Mrs wako utanisamehe? samahan lakin.
 
Waondoe mzizi wa fitna . Waite waandishi wa habari huko jela . Waitangazie nchi kupitia hao waandishi wa habari . Na wakiri makosa yao ya kubaka . Na waeleze dhumuni lao hasa lilikuwa nini . Kama ni burudani au mambo ya uganga. Then wawaombe msamaha watanzania wote pamoja wazazi pamoja na hao watoto waliofanyiwa ubakaji. Hiyo itaondoa utata wote wa kumtuhumu rais na bla bla zote. Baada ya hapo kama watasamehewa sawa na hata kama hawatasamehe sawa. Lakini utata utata utakuwa umeisha

Ujui kitu wewe.
 
Tafuta wimbo wao wa
"SALIMA"

Usikilize vizuri sana ndio tatizo

Nakupa kidogi tu

"oho! salimaaaaa
haaaasas x 2
nilikudanganya ukamuacha yeye....."

Ila UWT wakatengeneza watoto wao eti wamebakwa....ahaaaaa!

ahaaas kumbe huu wimbo una historia hivi basi naupenda mpaka basi inawezekana true story
 
pole sana mungu atawahukumu wote wanao hukumu watu kwa hila na madaraka waliyonayo hapa duniani chadema tukishinda 2015 tuombeni mungu tutawatoa wote walio fungwa kwa hila na uonevu
 
kama kweli walibaka basi waendelee tu kutumikia adhabu yao. na si wao tu waliohukumiwa mbona kuna mamia ya wafungwa kama wao? unless otherwise.
 
Waondoe mzizi wa fitna . Waite waandishi wa habari huko jela . Waitangazie nchi kupitia hao waandishi wa habari . Na wakiri makosa yao ya kubaka . Na waeleze dhumuni lao hasa lilikuwa nini . Kama ni burudani au mambo ya uganga. Then wawaombe msamaha watanzania wote pamoja wazazi pamoja na hao watoto waliofanyiwa ubakaji. Hiyo itaondoa utata wote wa kumtuhumu rais na bla bla zote. Baada ya hapo kama watasamehewa sawa na hata kama hawatasamehe sawa. Lakini utata utata utakuwa umeisha

Si dhani kama hoja yako ina mantiki yoyote kama mahakama ishafanya kazi yake bas hakuna kutangazia kupitia vyombo vya habari kwa ufupi sioni mashiko katika hoja yako maana kisa kipo na lisemwalo lipo sio watanzania wote ni mbulula kama mnavo dhani!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom