Babu Seya/Papii Nguza kweli walibaka? Tukielekea kureview kesi yao oct 30

Babu Seya/Papii Nguza kweli walibaka? Tukielekea kureview kesi yao oct 30

ninachoamini mimi ni kwamba, baba, na vijana wake (Familia) hawawezi kufanya ujinga kama huo, bora angewasingizia kuuza madawa ya kulevya kidogo inge make sense, Babu seya ni innocent na Mungu anajua!!

Kama ulikuwa ukifuatilia mwenendo wa ile kesi, ni wazi hao watu wa familia walifanya ushenzi wa ajabu kwa vijana wetu na hiyo adhabu waliyopata haitoshi walitakiwa wahukumiwe kunyongwa mpaka wafe!!
 
Mtaani kuna maneno !tulishasikia babu Seya na mwanaye walishaachiwa wakarudi Kongo .
 
Kama ulikuwa ukifuatilia mwenendo wa ile kesi, ni wazi hao watu wa familia walifanya ushenzi wa ajabu kwa vijana wetu na hiyo adhabu waliyopata haitoshi walitakiwa wahukumiwe kunyongwa mpaka wafe!!

Inawezekana mkala sahani moja na mzazi wako?
 
wakiwa court of Appeal wakili mabere marando alisikika akisema "katika umri wangu wote sijawahi sikia ama kuona mtoto wa miaka chini ya nane akaingiliwa na mtu mzima kisha mzazi wake asigundue siku ileile hadi mtoto alipoanza kuoza "

hebu tufikiri kwa pamoja, watoto zaidi ya watano walikua below eight wakati huohuo wanadai waliingiliwa mara kadhaa na watoto wa babu seya na babu seya mwenyewe, well ! sasa tuamini kuwa wazazi wa watoto wale wote walikuwa si waangalifu kuweza kutambua hilo mapema ? kwa watoto wetu hawa mpaka darasa la tatu wanaogeshwa na kufuliwa nguo hadi za ndani !>? tujiulize damu hazikuwatoka ? je madoa hayakubaki kwenye chupi zao >? ingekuwa mmoja unaweza kusema kiwango chake cha uvumilivu labda ni kikubwa, lakini kwa watoto zaidi ya watan ? hapana...maana mtu mzima mwenyewe akiingiliwa bila ridhaa cha moto anakiona sembuse hao watoto wadogo hivyo >?

nami naungana na wengine kuona mashaka makubwa ya ushiriki wa familia nzima kuwanajisi watoto wadogo hao .
 
wakati wa kusikiliza rufaa wakili Marando alisema kesi ni ya kubambikiwa.
ila ukweli Mungu anaujua.
 
Don't jump into conclusions...ile kesi imeshasikilizwa mara 2 wakaonekana wana hatia. Na ninvyofahamu mimi (kwa uelewa wangu mdogo wa sheria),
kesi ya kubaka watoto/mtoto unahitajika ushahidi wa aina 2 tu kukutia hatiani...1 - Mtoto mwenyewe kusema kwamba ni mtu 'huyu' ndio kambaka (wale watoto walipoint kuwa babu Seya na wanae wamewabaka wakahadithia kwa ufasaha walivyofanyiwa),
2 - Daktari kuthibitisha kwa watoto wametendewa kitendo hicho (Daktari alithibitisha hilo, namfahamu Daktari aliyewafanyia uchunguzi wale watoto na ni kweli walifanyiwa hivyo, ripoti na picha ya athari walivyoharibiwa zipo kwenye mafaili yao)....Sioni jinsi gani Babu Seya na wanae watatoka hapo.

zaidi ya hapo, mmoja kati ya majaji wanaoreview hiyo kesi ni jaji Nathalie Kimaro...soma historia yake wakati yuko mahakama ya Kisutu kuhusu kesi za ubakaji na kunajisi watoto!

ndugu , Mahakama imeweka ngazi zote hizo kuona haki inatendeka , na ndio maana hata jopo la wasikiliza/wapitia hukumu husika kwa ngazi hiyo huwa makini zaidi, na zito zaidi.....! hiyo ni hatua ya mwisho...
usibeze ushahidi na maelezo ya mashahidi na mawakili wa kina Papi kocha.
Pamoja na maelezo ya daktari, ushahidi wa watoto husika mbona Nguza Mbangu and Francis Nguza waliachiwa baada ya kuwa wamekaa jela for some years ?
 
mi nilisikia walibaka walikuwa wanatengeneza porno movie na hao watoto zinauzwa nje.

Rafiki unaniangusha, hata wewe unanaswa na cheap rumours kama hizo?

Ingekuwa kweli si yungeshapewa dvd au youtube tujionee wenyewe ili asionewe huruma?

Hizo video zinaangaliwa sayari gani?

Atleast issue ya ushirikina ndio hoja pekee inayoweza kufanya familia nzima kuji-involve na upuuzi huo.
 
hii source yangu ni kubwa sana matola! huwezi amini ila ndo hivo
 
narudia tena sijawahi kuona hakimu wa aina hii na hukumu ya aina hii ambayo hakimu aliamua kuweka maoni yake binafsi kwani kinachowatia hatiani washtakiwa katika kesi zote ni ushahidi na siyo maoni ya hakimu.

"Ni wajibu wa mahakama kutafakari ushahidi wa utetezi hata kama hauna uzito; sasa huyu Lyamuya katika hukumu yake amewataja mashahidi wa utetezi waliokuja kutoa ushahidi bila kueleza mashahidi kwa mapana walieleza nini!

"Kwa mkanganyiko huu uliofanywa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Lyamuya, siyo tu alikosea kisheria; nasema alifanya makusudi na alikuwa ameshaamua kuwapeleka jela warufani!"
wakili Mabere Marando.

hayo yalikuwa baadhi ya maneno ya Marando alipokuwa mahakama ya rufaa...~>>~
 
ndugu , Mahakama imeweka ngazi zote hizo kuona haki inatendeka , na ndio maana hata jopo la wasikiliza/wapitia hukumu husika kwa ngazi hiyo huwa makini zaidi, na zito zaidi.....! hiyo ni hatua ya mwisho...
usibeze ushahidi na maelezo ya mashahidi na mawakili wa kina Papi kocha.
Pamoja na maelezo ya daktari, ushahidi wa watoto husika mbona Nguza Mbangu and Francis Nguza waliachiwa baada ya kuwa wamekaa jela for some years ?

Masikitiko yangu tu ni kwamba kama watu wanafabricate mpaka nyaraka za Usalama wa Taifa je ndio ije kuwa hiyo medical examinations?

Sioni namna ya Babu Seya kushinda kesi hii kama watu walishafabricate taarifa ya Dr. Na ukumbuke ni madoctor hawa hawa walio mahiri kwa utoaji mimba mitaani je anaweza kuacha offer ya 20 million kutoa taarifa ya uongo?

Siko hapa kuwanjia geshima Madoctor lakini tumeona kwa ushahidi wasomi kama kina Dr Bana wanavyoweza kutumiwa na watu kwa sababu ya njaa zao.
 
Mkenya tuliyeambiwa kuwa mtekaji wa Ulimboka alieleza ukweli mahakamani alivyotekwa na kulazimishwa kuiambia uongo mahakamani. Kama Nguza naye alibambikiwa ubakaji, angeieleza mahakama chanzo cha bifu lake na hao wabambikizaji, kama ni kula wake wao au vinginevyo. Potelea mbali hata angebaki gerezani lakini ukweli ungejulikana kwa umma, na pengine kwa ukweli huo siku moja angesamehewa adhabu yake.

...Kama Kesi Iliishasukwa Kiasi hicho, Nani Angemuamini? Si Wangeona ni Kutapatapa kwa Mfa maji tu??:A S 39:
 
Binafsi siamini, kwasababu ukifuatilia kwa kiwango kidogo tu utagundua watu kibao tu walioko jela kwa kusingiziwa au kwa kutotosha utetezi,
ni wengi sana walioonewa, sasa kwa kesi hii inamashaka sana na kila sababu za kufanya mtu upate ukakasi kuamini hukumu!
Natumaini siku moja Nguza Viking na Papii kocha watarudi tu uraiani na tutafurahia tena uwepo wao pamoja nasi!
Mungu fanya njia.
 
Inakuaje unaamua kuwapa watu msala kwa staili hiyo ili kumkomoa tu mwingine?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Masikitiko yangu tu ni kwamba kama watu wanafabricate mpaka nyaraka za Usalama wa Taifa je ndio ije kuwa hiyo medical examinations?

Sioni namna ya Babu Seya kushinda kesi hii kama watu walishafabricate taarifa ya Dr. Na ukumbuke ni madoctor hawa hawa walio mahiri kwa utoaji mimba mitaani je anaweza kuacha offer ya 20 million kutoa taarifa ya uongo?

Siko hapa kuwanjia geshima Madoctor lakini tumeona kwa ushahidi wasomi kama kina Dr Bana wanavyoweza kutumiwa na watu kwa sababu ya njaa zao.

naelewa mantiki yako, na kama haya yasemwayo mitandaoni ni kweli kuwa kuna mkono mzito nyuma ya kesi hii hakika haki ni ngumu kupatikana unless otherwise alieitengeneza awe ameridhika kuwa chamoto wamekiona so waachwe waende zao .
 
kuna Wimbo wa Bushoke unaitwa Msela Jela,anadai alienda kumtembelea msela(papi) jela na akamueleza ukweli wa kesi yote ile na kama ukisikiliza kwa makini bushoke anasema rais mtoe piiii unganisha dots kesi ya kubaka haina msamaha wa rais lkn bushoke akasema rais mtoe piiiiii nomaaaa sanaaaa jamani..kuwapoteza watu kisa kugegedewa demu?
 
Back
Top Bottom