Babu Seya: Ufafanuzi juu ya uvumi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii

Babu Seya: Ufafanuzi juu ya uvumi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii

Hakuna kosa lisilosameheka duniani ni mangapi tunayomkosea Mungu na tukiomba tunasamehewa ? Mtoa hukumu n Muumba ila binaadamu tumejitwalia mamlaka zisizokuwa zetu kwa imeandika lililofungwa duniani na mbinguni limefungwa sasa binadamu ni nani hata ushindwe kusamehe? Ila kama wamesingiziwa malipo ni hapahapa duniani na chozi la mnyonge linalipwa na Mungu yetu macho.

Jipe muda kidogo wa kusoma sheria ya makosa ya jinai kabla ya kupayuka.

Kwenye rufaa watoto wawili wa babu Seya waliachiwa huru na mahakama ya rufaa.
 
Hawa watu wa kuzusha habari hivi faida wapatayo huwa ni nn haswa?!
 
Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na; Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, DAR ES SALAAM. Septemba 8, 2014.

Aargh..... Nchi hii Inashangaza, eti Jeshi la Magereza linamsaka aliyeanzisha uzushi huu; wanawaogopa Global Publishers au???
 
Back
Top Bottom