Babu Tale afikishwa Mahakamani na kurudishwa tena rumande...

Babu Tale afikishwa Mahakamani na kurudishwa tena rumande...

Kuna mdau kasema sio kesi hii kumbe, ni kesi ya Video Chafu

CC mahondaw

anashatakiwa kwa kutumia sheria ya mitandao ya mwaka 2015...

inasemekana walifanya vile ili kumuumiza RUGE siunajua boss ndio anasimamia shoo ya kadada ketu.....
 
anashatakiwa kwa kutumia sheria ya mitandao ya mwaka 2015...

inasemekana walifanya vile ili kumuumiza RUGE siunajua boss ndio anasimamia shoo ya kadada ketu.....
Duh, aisee.
Sasa Video ilifika fika vipi kwake?
Maana nimewaza pale labda angekamatwa Bill Nass labda.
 
Duh, aisee.
Sasa Video ilifika fika vipi kwake?
Maana nimewaza pale labda angekamatwa Bill Nass labda.

hiyo video haikuwahi kuwa kwa bill... acording to nandy mwenyewe... ilikuwa kwenye simu yake na akavunja simu yan unatoa simu alafu unaongeza hela nyingine ili upate simu kali zaidi kuna vitu alisahau kufuta....

mtu wa kwanza kukamatwa kwa hyo ishu ni jamaa wa udakutz.. hii inaendea wiki sasa kwa hyo yeye ndio kamtaja bwana mkubwa kuwa ndiye aliyempa kazi ya kupost hyo video
 
Anhaa,
Nimekupata Mkuu wangu.
So Pengine alipovunja alivunja kwa Babu tale au Jamaa yake na Tale labda.
 
Ufafanuzi.....

Tale ametiwa mbaroni kwa amri ya mahakama kuhusu kesi ya madai ya Bwana Mbonde ambaye anamdai Tale 240 Milioni,hivyo kesi haihusiani na taarifa ya makosa ya mtandao kwa kuvujisha video ya Nandy kama inavyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii
 
kweli mahakamani kuna baridi kali, kavaa sweta kabisa! duh
 
Ufafanuzi.....

Tale ametiwa mbaroni kwa amri ya mahakama kuhusu kesi ya madai ya Bwana Mbonde ambaye anamdai Tale 240 Milioni,hivyo kesi haihusiani na taarifa ya makosa ya mtandao kwa kuvujisha video ya Nandy kama inavyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii
OK mimi mwenyewe nilishangaa, ujinga aufanye mwenyewe Nandy, kukamatwa akamate mwingine na mwenyewe nandy anakuambia video aliirekodi miaka miwili, iliyopita sasa babutale avujishe leo ili iweje cha msingi babutale atafute njia ya kumalizana na Ostaz mbonde la sivyo jela inamwita.
 
Duh!! huyo ustazi kweli nuksii,, ati alitaka mil700,, kwa content gani ss??

Unaeza kuta huyo Tale mwenyew kala mil 3 au 4 af ustaz anataka mil 250
 
July 19, 2016

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa hati ya kukamatwa kwa Hamis Tale ‘Babu Tale,’ ambaye ni meneja wa mwanamuziki wa bongo fleva, Diamond Platnumz, anaandika Faki Sosi.

Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na Babu Tale kutotii amri ya mahakama iliyomtaka amlipe Shekhe Hamis Mbonde Sh. 250 milioni.

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

Kutokana na Babu Tale na mwenzake Iddi Tale kushindwa kulipa fedha hizo kama ilivyoamriwa tarehe 18, Februari mwaka huu, mahakama ilitoa hati ya kukamatwa kwa wadaiwa hao tarehe 8 Julai mwaka huu.

Katika hati hiyo, mahakama ilimuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala kuwa, hadi leo tarehe 19 Julai mwaka huu awe amewakamata wadaiwa hao ili wafike mahakamani kueleza kwanini wasipewe adhabu kwa kukiuka amri ya mahakama.

Shauri hilo limetajwa tena leo mbele ya Juma Hassan, Kaimu Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo ametoa hati nyingine kumuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni kuwakamata wadaiwa hao.

Msajili Juma ametoa hati hiyo baada ya Mwesigwa Muhingo, Wakili wa Shekhe Mbonde, kuomba hati hiyo ipekwe Kinondoni kwa kuwa Babu Tale anaishi huko na si Wilaya ya Ilala kama hali ya kwanza ilivyoeleza.

Tarehe 18 Februari mwaka huu, Jaji Augustine Shangwa, aliwaamuru wadaiwa kulipa Sh. 200 milioni kama fidia ya kuvunja haki miliki ya Shekhe Mbonde na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunja makubaliano.

Katika uamuzi wake Jaji Shangwa amesema, Juni 16, 2013, Mbonde aliingia makubaliano na wadaiwa hao na wenzake ya kufanya biashara ya kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala DVDs kwa ajili ya kuziuza nchini.

Wadaiwa hao waliahidi kumjengea nyumba, kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake pia walimpa Sh milioni mbili na kumnunulia kanzu na kofia (baraghashia) na kurekodi DVDs zenye ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya Wanawake, Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya Hasara na Maadui wa Uislam.

Amesema, makubaliano ya awali yalikuwa kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei na jinsi ya kuziuza, badala yake waliziuza na kuzisambaza nakala hizo na kujipatia faida bila kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi wake.

Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement Kihoko, alifungua kesi ya madai namba 185/2013 akiiomba mahakama iamuru wadaiwa wamlipe Sh. 700 milioni kama fidia ya kuvunja makubaliano na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunjwa kwa makubaliano.
sheria ni msumeno, wizi wa hakimiliki za wanyonge utaisha tu siku moja. peleka ndani huko.
 
Amedhurumu pesa ya watu
Deni halikimbiwi aisee ajichange change akalipe hela za watu.

Na usawa huu ulivyo tight kama bikra mill240 kuzipata watu wanaweza kumshikisha ukuta ili wamlipie au asubiri aende jela.
 
Back
Top Bottom