Babu Tale afikishwa Mahakamani na kurudishwa tena rumande...

Utetezi wa Babu Tale huu hapa chini,

“Mimi na marehemu brother yangu tulifungua kampuni ya Tip Top Connection pamoja, mimi nifanye muziki yeye anisaidie.. Alipoona nimesogea akaona aachane na mimi ili afanye movie. Kwahiyo hakuwa anajua mimi ninachokifanya kwenye muziki, mimi pia sikuwa najua anachokifanya kwenye movie, imeenda akawa anafanya movie, sijawahi hata kushiriki hata kwa njia ya kuonekana location, hata kukaa nao kuongea nao lolote au kusainisha nao mkataba, so I know nothing,” amesema Tale.

“Mwaka juzi wakati nipo Uingereza yule Mzee akasikika kwenye U Heard kwamba anaidai Tip Top Connection milioni 50. Soudy Brown alimhoji akamuambia unamjua Babutale, akasema namjua lakini sijawahi kuongea naye hata siku moja. Akapeleka kesi mahakamani wakati brother yupo hai baadaye akaja akawa amefariki mimi nikawa sijui tena kinachoendelea. Kumbe yule mwanasheria alikuwa na marehemu brother na yule mzee wanakutana mahakamani.

Mwaka huu kama mwezi mmoja uliopita akanipigia mtu simu, simu yangu napigiwa na watu wengi sana hii ‘mimi mwanasheria, unashtakiwa kwa kosa la kumdhulumu mtu kazi.’ Nikamuambia hizi kazi alikuwa akisimamia marehemu brother yangu kwahiyo story unazoniletea mimi unanirusha roho. Nikamwambia mimi naishi maisha yangu sijui kinachoendelea na sijawahi kujihusisha na chochote na hata huyo sheikh kama ana sehemu yoyote ambayo ameona kuna jina langu nimesaini naye niko tayari hata akisema ananidai,” anasisitiza.

“Kwahiyo wakati wanazunguka na kesi yao wakapita Brela kuchunguza hii kampuni wako nani na nani? Wakagundua kuna marehemu Abdul Bonge, mimi hapa na brother yangu mwingine lakini hawajui labda kwamba sisi tuligawana kila mtu na majukumu yake kwasababu kila mmoja alikuwa anafanya kile ambacho anakiweza.”

“Kwahiyo wameenda mahakamani wamepata barua wanikamate kwasababu mimi ninadaiwa. Mimi niko nyumbani wamekuja kugonga nyumbani kwangu kama majambazi. I was like wewe unakuja unajua hapa kwa nani? Mbona unataka kuniharrass rafiki yangu? Wewe unakuja kumkamata mtu usiyemfahamu! ‘Wewe si Tale’ walikuwa hawajui kama mimi ndio Babutale. Kama wao wananitaka wangeniambia mimi nipo Oysterbay polisi hapa, hawajaja. Mimi asubuhi ndio nikatoka nikaenda kumfuaya yule mwanasheria ambaye anasimamia kesi kuaniambia kuna nini naona kama watu wananitumia meseji kwamba nimeshtakiwa, akanihadithia in and out.”

“Tangu nijue kila kitu leo nina siku ya nne, I know nothing, sijawahi kumuona huyo mzee hata akitokezea sehemu simjui kwa sura. Lakini sasa yule mwanasheria wa yule mzee anasema Babutale ana hela, tukimshtaki Babutale atauza nyumba au watu watamchukua au tukimdhalilisha kwenye mitandao ataona aibu atataka kulipa. Vaa kiatu changu, wewe ni sehemu gani unalipa hapo? Sijui chochote, lakini wao wanaamini kwasababu mahakama imewaamuru nimewalipe milioni 250 na wanaamini mimi nina hela basi nitawalipa tu, haiwezekani,” amesema Tale.

Hata hivyo meneja huyo bado yupo njia panda kutafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye hukumu hiyo nzito.

“Sijajua nini nitakachofanya, I know nothing,” anasema. “Anachokifanya ameamua kunichafua bila sababu, hajui kwamba mimi najianda kuwa waziri wa hii nchi na kuwa mbunge, anajiandaa kunifanya nionekane tapeli halafu ni mtu wa dini labda.”

Marehemu Abdul Bonge aliyefariki March 2015 na Mbonde waliingia makubaliano hayo June 16, 2013 kufanya biashara ya kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala DVDs na kuziuza nchini.

Pia alimuahidi kumjengea nyumba, kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake na kumpa shilingi milioni mbili na kumnunulia kanzu na kofia (baraghashia) na kurekodi DVDs zenye ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya Wanawake, Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya Hasara na Maadui wa Uislam, kwa mujibu wa Mwanahalisi.

Kwa mujibu wa Jaji Augustine Jangwa, makubaliano ya awali yalikuwa kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei na jinsi ya kuziuza na kwamba badala yake waliziuza na kuzisambaza nakala hizo na kujipatia faida bila kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi wake.

Awali Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement Kihoko alitaka alipwe shilingi milioni 700 kama fidia ya kuvunja makubaliano yao.
 
Inawezekana labda kutokujua kwake, kulimfanya kuwa na kiburi.
hapa " tuko pamoja ""......ila tatizo mkuu""pesa na umaarufu huwa vina desturi ya kumuotesha mtu mapembe "" ziki Ku control wawez kuhisi wanaume wenzio wote ni makhanithi ila wewe peke yko ndiye shababi ""

May take ""tumuombee Mungu arejee uraiani"" maana mpaka sasa nilichojifunza katika maisha "" matatizo huwa hayana kwao "" leo waweza kumcheka tale " kesho ya kaja kwako kwa taswira nyingine
 
Ela ya WCB inabaki kuwa ya WCB. Leo hii meneja wa Azam adaiwe, Alafu ategemee Azam wamlipie, hamna kampuni itakayofanya ujinga huo hata Bill Gates na Microsoft hawawezi kufanya upuuzi huo.
Labda Bill Gate wa Yombo
 
Utetezi wa Babu Tale huu hapa chini,

“Mimi na marehemu brother yangu tulifungua kampuni ya Tip Top Connection pamoja, mimi nifanye muziki yeye anisaidie.. Alipoona nimesogea akaona aachane na mimi ili afanye movie. Kwahiyo hakuwa anajua mimi ninachokifanya kwenye muziki, mimi pia sikuwa najua anachokifanya kwenye movie, imeenda akawa anafanya movie, sijawahi hata kushiriki hata kwa njia ya kuonekana location, hata kukaa nao kuongea nao lolote au kusainisha nao mkataba, so I know nothing,” amesema Tale.

“Mwaka juzi wakati nipo Uingereza yule Mzee akasikika kwenye U Heard kwamba anaidai Tip Top Connection milioni 50. Soudy Brown alimhoji akamuambia unamjua Babutale, akasema namjua lakini sijawahi kuongea naye hata siku moja. Akapeleka kesi mahakamani wakati brother yupo hai baadaye akaja akawa amefariki mimi nikawa sijui tena kinachoendelea. Kumbe yule mwanasheria alikuwa na marehemu brother na yule mzee wanakutana mahakamani.

Mwaka huu kama mwezi mmoja uliopita akanipigia mtu simu, simu yangu napigiwa na watu wengi sana hii ‘mimi mwanasheria, unashtakiwa kwa kosa la kumdhulumu mtu kazi.’ Nikamuambia hizi kazi alikuwa akisimamia marehemu brother yangu kwahiyo story unazoniletea mimi unanirusha roho. Nikamwambia mimi naishi maisha yangu sijui kinachoendelea na sijawahi kujihusisha na chochote na hata huyo sheikh kama ana sehemu yoyote ambayo ameona kuna jina langu nimesaini naye niko tayari hata akisema ananidai,” anasisitiza.

“Kwahiyo wakati wanazunguka na kesi yao wakapita Brela kuchunguza hii kampuni wako nani na nani? Wakagundua kuna marehemu Abdul Bonge, mimi hapa na brother yangu mwingine lakini hawajui labda kwamba sisi tuligawana kila mtu na majukumu yake kwasababu kila mmoja alikuwa anafanya kile ambacho anakiweza.”

“Kwahiyo wameenda mahakamani wamepata barua wanikamate kwasababu mimi ninadaiwa. Mimi niko nyumbani wamekuja kugonga nyumbani kwangu kama majambazi. I was like wewe unakuja unajua hapa kwa nani? Mbona unataka kuniharrass rafiki yangu? Wewe unakuja kumkamata mtu usiyemfahamu! ‘Wewe si Tale’ walikuwa hawajui kama mimi ndio Babutale. Kama wao wananitaka wangeniambia mimi nipo Oysterbay polisi hapa, hawajaja. Mimi asubuhi ndio nikatoka nikaenda kumfuaya yule mwanasheria ambaye anasimamia kesi kuaniambia kuna nini naona kama watu wananitumia meseji kwamba nimeshtakiwa, akanihadithia in and out.”

“Tangu nijue kila kitu leo nina siku ya nne, I know nothing, sijawahi kumuona huyo mzee hata akitokezea sehemu simjui kwa sura. Lakini sasa yule mwanasheria wa yule mzee anasema Babutale ana hela, tukimshtaki Babutale atauza nyumba au watu watamchukua au tukimdhalilisha kwenye mitandao ataona aibu atataka kulipa. Vaa kiatu changu, wewe ni sehemu gani unalipa hapo? Sijui chochote, lakini wao wanaamini kwasababu mahakama imewaamuru nimewalipe milioni 250 na wanaamini mimi nina hela basi nitawalipa tu, haiwezekani,” amesema Tale.

Hata hivyo meneja huyo bado yupo njia panda kutafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye hukumu hiyo nzito.

“Sijajua nini nitakachofanya, I know nothing,” anasema. “Anachokifanya ameamua kunichafua bila sababu, hajui kwamba mimi najianda kuwa waziri wa hii nchi na kuwa mbunge, anajiandaa kunifanya nionekane tapeli halafu ni mtu wa dini labda.”

Marehemu Abdul Bonge aliyefariki March 2015 na Mbonde waliingia makubaliano hayo June 16, 2013 kufanya biashara ya kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala DVDs na kuziuza nchini.

Pia alimuahidi kumjengea nyumba, kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake na kumpa shilingi milioni mbili na kumnunulia kanzu na kofia (baraghashia) na kurekodi DVDs zenye ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya Wanawake, Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya Hasara na Maadui wa Uislam, kwa mujibu wa Mwanahalisi.

Kwa mujibu wa Jaji Augustine Jangwa, makubaliano ya awali yalikuwa kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei na jinsi ya kuziuza na kwamba badala yake waliziuza na kuzisambaza nakala hizo na kujipatia faida bila kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi wake.

Awali Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement Kihoko alitaka alipwe shilingi milioni 700 kama fidia ya kuvunja makubaliano yao.

Sheikhe Hamisi Mbonde uzee huo ameutoa wapi?Babu Tale bana anamuita mzee mtu aliyemzidi umri labda kwa sababu ya zile ndevu hahahaaaa.

Ila Sheikhe Hamisi Mbonde nae ni shida,Salafi na makesi kama haya wapi na wapi hahahahaaa.
 
Kutoka Atatoka sema Duh kaonjeshwa lupango....jela Haina mwenyewe Mtu yoyote anaweza kwenda ......ukibugi tu

Ova
 
Ela ya WCB inabaki kuwa ya WCB. Leo hii meneja wa Azam adaiwe, Alafu ategemee Azam wamlipie, hamna kampuni itakayofanya ujinga huo hata Bill Gates na Microsoft hawawezi kufanya upuuzi huo.
Terms and conditions kuzingatiwa....
 
Mkuu naona kama unatania,akili yangu inanituma hivyo.......

Huyo kiongozi wao Mondi wiki mbili nyuma tumetoka kumzika mjomba'ake pale Ilala akiugua homa ya mapafu angekuwa na hela za kutosha kiasi cha kwenda kumlipia huyu Tale ambaye siyo damu yake si angempeleka hospital nzuri hata hapo Nairobi?

Wasanii wengi mbwembwe tu wasikujaze upepo sometimes hata bank mill500 hana wao daily mtaani kujionyesha onyesha.
Mmmh...basi sawa
 
Mmh! Mkuu unataka kusema Diamond hana mil 250??? Ndugu huyu jamqaa anapiga show kwa zaidi ya mil 50.
Anaweza kuwa nazo tatizo sisi huwa tunahesabu anazoingiza tu je tumewahi kujiuliza anatumia ngapi? maana unaweza kuwa kwa mwaka unaingiza Milion 500 unatumia milion 400 kwa mwaka pia pesa lazima wagawane. ila kuna a lot of show off.
 
Tena hapo alianzia 700mil ndio wakamshusha mpaka hiyo 250mil,
Sema huyu Babu Tale kawa jeuri maana ilitakiwa tu amfuate Sheikh amuombe wamalizane chobingo, ye akatumia ujeuri.
Dah,
Ila alisemaga eti ile kampuni yao Kaka yake ambae ni Marehemu ndie aliezipiga zile hela, sio yeye.
Kama kasema hivyo kamkosea sana marehemu ndugu yake. sheria za kidini mtu akifariki madeni yake yanalipwa hata wa kuuza mali. kama shekh aliingia mkataba na kampuni ambao yeye ni mmoja wa wamiliki hata kama hukuhusika direct ni deni lako. sawa na kusema ukatie sign mkataba na Voda halafu ikatokea director kaondoka kaja mwingine utasema sio deni la voda, ni lazima zilipwe. yeye alikuwa share na ndugu yake na ndugu yake alitia sign kuwakilisha kampuni mzigo atabeba yeye ndio maana mahakama imemtia hatiani. labda itokee shekh amsamehe marehemu lakini sio kampuni.
 
Ml 250 unaichukulia poa eehh "" Acha masihara kabisa ...hao hela ya kumlipa hawana " halafu niwatu wanaoamini ushirikina mnooo" usikute sababu zilizofanya wasimlipe ilikuwa nikwenda kumroga hakimu na mwenye madai wapate kuifuta hiyo kesi "" lakini wamemkuta hakimu na shekhe ni vyuma vya pua " so albadir zao zimedunda ""
Wenye akili kwa post hii wameshajua ni nani ayeamini ushirikina hapa!
 
Kama kasema hivyo kamkosea sana marehemu ndugu yake. sheria za kidini mtu akifariki madeni yake yanalipwa hata wa kuuza mali. kama shekh aliingia mkataba na kampuni ambao yeye ni mmoja wa wamiliki hata kama hukuhusika direct ni deni lako. sawa na kusema ukatie sign mkataba na Voda halafu ikatokea director kaondoka kaja mwingine utasema sio deni la voda, ni lazima zilipwe. yeye alikuwa share na ndugu yake na ndugu yake alitia sign kuwakilisha kampuni mzigo atabeba yeye ndio maana mahakama imemtia hatiani. labda itokee shekh amsamehe marehemu lakini sio kampuni.
Mfano ww mna kampuni na kaka yako,alafu kaingia mkataba bila kukwambia kesho kafa na ukiangalia ela anayodaiwa huna uwezo wa kuilipa na vile vile una familia inayokutegemea.Je ww kama mwanaume utachagua nini?.Haya mambo yanatokeaga sana tena,watu wanazikana sana kwenye maswala ya ela.Japokuwa marehemu hasemwi lkn alikosea.Ila babutale awe mpole huyo sheikh akikaa nae vizuri yanaisha,ila akileta kiburi jela inamwita.
 
Mimi sijui hiyo kampuni lakini kawaida ya kila kampuni inavyoingia mkataba kuna taratibu zake ni watu gani wanatia signature ili uwe mkataba halali. mkataba hauwezi kuwa halali kama taratibu hazikufwata. kama marehemu alitia mkataba kama yeye basi ni mali za marehemu kuuzwa ila kama kuna watu wanaanzisha kampuni hata kama na ndugu bila kuwa na makubaliano kampuni iendeshwe vipi na maamuzi yatolewe kwa utaratibu gani ni shida. mimi siwezi kusema kitu sababu sijui kampuni yao ilikuwa na utaratibu gani ila kwa kuwa mahakama imemuona na hatia basi kuna kitu kinamfunga katika mkataba. kama ulivyosema ni lazima awe mpole aweze kumaliza nje ya mahakama.
 
Wenye akili kwa post hii wameshajua ni nani ayeamini ushirikina hapa!
acha ushabiki maandazi " huyo Mara kibao amesha kilo kwenye media kuwa huwa anatumia ndumba...nenda you tube tafuta interview yake na Salama jabir " katik show ya mkasi "" kisha urudi hapa
 
Babu tale akae na sheikh Mbonde jalada liondolewe mahakamani watumie best practice ku solve hili suala.B y the way namkubali sana Tale ana uwezo mkubwa wa kujenga na kuitetea hoja. Hizo 250M ni pesa ndogo sana kwa Tale cha msingi wao wakae wazungumzee
 
Mmh! Mkuu unataka kusema Diamond hana mil 250??? Ndugu huyu jamqaa anapiga show kwa zaidi ya mil 50.
Nimeshakwambia achana na maigizo ya mastaa wa bongo...hizo mbwembwe za kujishaua wanahela lakini kiuhalisia hawana kitu....kuna mastaa wakubwa tu na uhakika hata wewe umewapiga gap kimaisha...trust me bongo hakuna staa anayeweza kutoa mil 250 kirahisi..
 
Back
Top Bottom