Babu Tale afikishwa Mahakamani na kurudishwa tena rumande...

Babu Tale afikishwa Mahakamani na kurudishwa tena rumande...

Janja Janja nyingi kwenye maisha ya watu "" sasa hivi wamekutana na Chuma cha pua...kama hajaweka bond nyumba yake ..ili akopeshwe hiyo hela sijui " na bond ya kiasi hicho itategemea na hadhi yenyewe ya nyumba na mahala ilipo "" kama ipo mchamba wima huko " ndio basi tena imekula kwake """ ......usawa huu nani wakukukopesha au wakukupa "" ml.250 kwa acapela tu """ .....labda bashite aingilie kati "" usikute hapo " diamond mwenyewe alikuwa anamtamni mkewe kitambo "" so anasubiri jamaa aende jela aanze kumt......... hahaaa
Atalipiwa na Rais wa Manzese

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wote wa mjini aka Wajanja wa Mjini LAZIMA wapate their day of reckoning in a Criminal Court of Law. Because most, if not all of them, are mean-spirited crooks and criminals operating on the boundaries of Law for maximum profit and/or private gain.
 
Bashite kashafanya yake ya kumpost na kuweka viashiria vya "daddy is coming"
 
Kama kasema hivyo kamkosea sana marehemu ndugu yake. sheria za kidini mtu akifariki madeni yake yanalipwa hata wa kuuza mali. kama shekh aliingia mkataba na kampuni ambao yeye ni mmoja wa wamiliki hata kama hukuhusika direct ni deni lako. sawa na kusema ukatie sign mkataba na Voda halafu ikatokea director kaondoka kaja mwingine utasema sio deni la voda, ni lazima zilipwe. yeye alikuwa share na ndugu yake na ndugu yake alitia sign kuwakilisha kampuni mzigo atabeba yeye ndio maana mahakama imemtia hatiani. labda itokee shekh amsamehe marehemu lakini sio kampuni.
Kampuni ndio inatakiwa ilipe na babu tale , hao wadeni watafute Mali ya kampuni na kuzikamata
 
Utetezi wa Babu Tale huu hapa chini,

“Mimi na marehemu brother yangu tulifungua kampuni ya Tip Top Connection pamoja, mimi nifanye muziki yeye anisaidie.. Alipoona nimesogea akaona aachane na mimi ili afanye movie. Kwahiyo hakuwa anajua mimi ninachokifanya kwenye muziki, mimi pia sikuwa najua anachokifanya kwenye movie, imeenda akawa anafanya movie, sijawahi hata kushiriki hata kwa njia ya kuonekana location, hata kukaa nao kuongea nao lolote au kusainisha nao mkataba, so I know nothing,” amesema Tale.

“Mwaka juzi wakati nipo Uingereza yule Mzee akasikika kwenye U Heard kwamba anaidai Tip Top Connection milioni 50. Soudy Brown alimhoji akamuambia unamjua Babutale, akasema namjua lakini sijawahi kuongea naye hata siku moja. Akapeleka kesi mahakamani wakati brother yupo hai baadaye akaja akawa amefariki mimi nikawa sijui tena kinachoendelea. Kumbe yule mwanasheria alikuwa na marehemu brother na yule mzee wanakutana mahakamani.

Mwaka huu kama mwezi mmoja uliopita akanipigia mtu simu, simu yangu napigiwa na watu wengi sana hii ‘mimi mwanasheria, unashtakiwa kwa kosa la kumdhulumu mtu kazi.’ Nikamuambia hizi kazi alikuwa akisimamia marehemu brother yangu kwahiyo story unazoniletea mimi unanirusha roho. Nikamwambia mimi naishi maisha yangu sijui kinachoendelea na sijawahi kujihusisha na chochote na hata huyo sheikh kama ana sehemu yoyote ambayo ameona kuna jina langu nimesaini naye niko tayari hata akisema ananidai,” anasisitiza.

“Kwahiyo wakati wanazunguka na kesi yao wakapita Brela kuchunguza hii kampuni wako nani na nani? Wakagundua kuna marehemu Abdul Bonge, mimi hapa na brother yangu mwingine lakini hawajui labda kwamba sisi tuligawana kila mtu na majukumu yake kwasababu kila mmoja alikuwa anafanya kile ambacho anakiweza.”

“Kwahiyo wameenda mahakamani wamepata barua wanikamate kwasababu mimi ninadaiwa. Mimi niko nyumbani wamekuja kugonga nyumbani kwangu kama majambazi. I was like wewe unakuja unajua hapa kwa nani? Mbona unataka kuniharrass rafiki yangu? Wewe unakuja kumkamata mtu usiyemfahamu! ‘Wewe si Tale’ walikuwa hawajui kama mimi ndio Babutale. Kama wao wananitaka wangeniambia mimi nipo Oysterbay polisi hapa, hawajaja. Mimi asubuhi ndio nikatoka nikaenda kumfuaya yule mwanasheria ambaye anasimamia kesi kuaniambia kuna nini naona kama watu wananitumia meseji kwamba nimeshtakiwa, akanihadithia in and out.”

“Tangu nijue kila kitu leo nina siku ya nne, I know nothing, sijawahi kumuona huyo mzee hata akitokezea sehemu simjui kwa sura. Lakini sasa yule mwanasheria wa yule mzee anasema Babutale ana hela, tukimshtaki Babutale atauza nyumba au watu watamchukua au tukimdhalilisha kwenye mitandao ataona aibu atataka kulipa. Vaa kiatu changu, wewe ni sehemu gani unalipa hapo? Sijui chochote, lakini wao wanaamini kwasababu mahakama imewaamuru nimewalipe milioni 250 na wanaamini mimi nina hela basi nitawalipa tu, haiwezekani,” amesema Tale.

Hata hivyo meneja huyo bado yupo njia panda kutafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye hukumu hiyo nzito.

“Sijajua nini nitakachofanya, I know nothing,” anasema. “Anachokifanya ameamua kunichafua bila sababu, hajui kwamba mimi najianda kuwa waziri wa hii nchi na kuwa mbunge, anajiandaa kunifanya nionekane tapeli halafu ni mtu wa dini labda.”

Marehemu Abdul Bonge aliyefariki March 2015 na Mbonde waliingia makubaliano hayo June 16, 2013 kufanya biashara ya kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala DVDs na kuziuza nchini.

Pia alimuahidi kumjengea nyumba, kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake na kumpa shilingi milioni mbili na kumnunulia kanzu na kofia (baraghashia) na kurekodi DVDs zenye ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya Wanawake, Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya Hasara na Maadui wa Uislam, kwa mujibu wa Mwanahalisi.

Kwa mujibu wa Jaji Augustine Jangwa, makubaliano ya awali yalikuwa kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei na jinsi ya kuziuza na kwamba badala yake waliziuza na kuzisambaza nakala hizo na kujipatia faida bila kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi wake.

Awali Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement Kihoko alitaka alipwe shilingi milioni 700 kama fidia ya kuvunja makubaliano yao.
Utetezi wa babu tale wa hovyo hivi hakuajili mwanasheria? Yaani kampuni iliyosajiliwa brela na ipo chini yake hajui inajihusisha na nini? Inamaana walikuwa wanafanya mambo yasiyo kwenye articles of association? Na je kampuni haitunzi kumbukumbu kiasi kwamba alikuwa hajui kama kampuni inadaiwa hata baada ya kaka yake kufariki?
Haya ni matatizo ya kuendesha kampuni kihuni.
 
Mkuu kuna tofauti hapa,
Vodacom ni Kampuni Kubwa yenye shareholders mbali mbali, na Management huingia mikataba kwa manufaa ya Kampuni nzima. Tofautisha na Kampuni ya Mfukoni ya kifamilia ambayo mko wawili tu mnaamua kupiga deals kila mtu na dili zake lakini mnatumia jina la kampuni ili kuhalalisha.
Sheria ya makampuni inawataka wote Vodacom na hizo kampuni zingine kuzingatia sheria. Hakimu hana kipimo cha kutofautisha kampuni ya mfukoni na kampuni kubwa. Kampuni ni kampuni tu hata kama inamilikiwa na wanafamilia share ngapi haijalishi kuna msemo wa wanasheria wanasema "one share is enough".
 
Halipwi mtu hapa. Ndio utajua baba mlezi w WCB nchi hii yy nani?
IMG_3606.JPG

Hahhahaaaa
IMG_3605.JPG
 
Back
Top Bottom