Babu Tale akiri kuna wasanii wa WCB nyota zao zimeshindwa kung’ara, aeleza hatua walizochukua

Babu Tale akiri kuna wasanii wa WCB nyota zao zimeshindwa kung’ara, aeleza hatua walizochukua

Shilandula

Member
Joined
Nov 30, 2019
Posts
6
Reaction score
6
Meneja wa WCB, Babu Tale amefunguka kuzungumzia ishu ya baadhi ya wasanii wa label hiyo nyota zao kushindwa kung’aa.


Lebo hiyo ina wasanii watano, ambao ni Diamond, Rayvanny, Mbosso, Lavalava pamoja na Queen Darleen.

Katika mahojiano maalum na gazeti la Mwananchi, Babu Tale alikiri kwamba Lavalava pamoja na Queen Darleen ni wasanii ambao nyota zao zimeshindwa kung’ara na kueleza hatua walizochukua.

“Kwenye familia za kawaida wapo watoto wenye mafanikio na ambao hawana, hivyo hivyo kwa familia ya WCB kuna baadhi ya wasanii nyota zao zimeshindwa kung’ara” alisema Babu Tale

Aliongeza, “Hivyo sisi kama viongozi wa labo tunachokifanya ni kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao, kama kila mmoja kumuuacha na meneja wake linalobakia ni jukumu lao kuangalia namna gani wanajiongeza,”

“Kama mnavyoona, hivi karibuni Lavalava aliachia wimbo wa ‘Tekenya’. Naona kaamua kuwatekenya mashabiki, na Queen Darleen inshallah naye hivi karibuni ataachia kazi”

Meneja huyo amedai wao kama WCB wanatoa mazingira sawa kwa kila msanii ili kuhakikisha anafanya vizuri katika safari yake ya muziki.
 
Queen darleen wangempa kazi ingine afanye haeleweki anachofanya kabisa mie kwa upande wangu simuelewi anavyoimba jukeaani ndio hakuna kabisa lava lava yeye yupo vizur
 
Labda sio swala la nyota kung'aa bali ni kulazimisha kipaji au wakati wao haujafika
 
Queen Darleen mbeleko tu za kaka yake,Ila Lavalava alianza vizuri kashindwa kumaintain.

Alafu mara nyingi kwenye label wote hamuwezi kuwa sasa,Marvin ina wasanii kibao lkn waliokuwa wakivuma Koredo Bello,Tiwa na Rikardo Bank,YCMB ina wasanii kibao lkn waliovuma Nick Minaj,Tyga,Drake nk, kwa hiyo ni kitu cha kawaida ila cha msingi ni wao wenyewe kujipanga na kuona wanawainuaje tena,ila Queen Diamond amuweke kwenye maswala yake ya Label mngt,Queen mziki ushamkataa.
 
Queen Darlin hamna kitu.

Lavalava hana muonekano wa kisanii. Dizain anaforce game hivi.
 
Lavalava yupo vizuri na miziki yake inafanya vizuri sema tu ajafanyiwa uwekezaji international kutokana na mziki anaofanya Ila queen darling hamna kitu.
 
Nadhani tu uwezo wao kimziki ni mdogo.
 
Back
Top Bottom