Babu Tale amuomba Waziri ampunguzie kazi ya kuzuia mvua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Tunaofanya burudani za viwanjani tumekuwa tukipigia sana simu Babu zetu vijijini wazuie mvua, katika hotuba ya Waziri sijaona akisema ujenzi wa Sports Arena, hakuna msanii asiyejua kama mimi ndiyo naongoza kufunga mvua, Waziri naomba unipunguzie hii kazi".

======

photo_2021-05-31_16-09-45.jpg

Mbunge wa Morogoro Kusini, Khamisi Taletale amesema huwa anawapigia simu wazee vijijini ili wazuie mvua kuruhusu shughuli za kimziki ziendelee.

Amesema Hotuba ya Waziri wa Ujenzi haijazungumzia kujenga Viwanja vya Michezo na Burudani hali ambayo itamfanya yeye aendelee na kazi ya kuendelea kuomba wazee wafunge mvua ili kufanya shughuli za Burudani.

Amemuomba Waziri ampunguzie kazi hiyo kwa kuwa yeye ndiye anayeongoza kufunga mvua nchini.
 
Awali niliposikia tetesi kuwa mwanaccm mwenzangu na mbunge wa Morogoro kusini babu Tale kuwa ni mchawi niliwabishia na kuwaambia Tale ni mwanamazingaombwe.

Lakini leo yeye mwenyewe babu Tale ndani ya bunge amekiri kuwa mara nyingi amekuwa akizuia mvua isinyeshe na mazao yanyauke ili mradi tu timu za mpira wa miguu zicheze na vijana wanaocheza kamari mikeka yao iweze kujibu.

Ama kwa hakika uchawi upo unaumiza wakulima kwa sababu ya kamari?

Niishie hapo!
 
Tunaofanya burudani za viwanjani tumekuwa tukipigia sana simu Babu zetu vijijini wazuie mvua, katika hotuba ya Waziri sijaona akisema ujenzi wa Sports Arena, hakuna msanii asiyejua kama mimi ndiyo naongoza kufunga mvua, Waziri naomba unipunguzie hii kazi".

Tabu kweli kweli
 
Wabunge wa ccm wapo peke yao Bungeni lakini wanajadili hoja za kijinga na mambo ya kitoto sana

Hakuna mbunge mwenye vision wa ccm Bungeni, Hawajui washike lipi na Waache wapi

Aina ya wabunge kama hao walienda Bungeni kimkakati kwa ajili ya kubadili katiba

Hakuna mbunge anayewaza lini Tanzania tutakuwa na kiwanda cha magari yetu ya umeme wa jua

Hakuna mbunge anayewaza kubadili chuo chetu Cha Muhimbili au udsm kuwa centre za utafiti na uvumbuzi wa chanjo za magonjwa ya virusi

Kazi kubwa wanayoweza Bunge hili ni kuvamia misiba, Kukata mauno, na kujadili Mbowe na Chadema

Hawana Forecast

Sent from my INE-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Awali niliposikia tetesi kuwa mwanaccm mwenzangu na mbunge wa Morogoro kusini babu Tale kuwa ni mchawi niliwabishia na kuwaambia Tale ni mwanamazingaombwe...
Bwasheeeeee! 😅 😅😅

Ndiyo maana alipita bila kupingwa! Nasikia waliokuwa wanafuata form, wanasahau njiani walikuwa wanaenda wapi, hadi deadline ikapita!

Chama kimeshika hatamu!

Everyday is Saturday................................😎
 
Azuie na baridi Matombo, Mahenge, Arusha, Lushoto, Mufindi, Makete, Njombe na Mbinga.
Shukurani!

Everyday is Saturday................................😎
 
Wabunge wa ccm wapo peke yao Bungeni lakini wanajadili hoja za kijinga na mambo ya kitoto sana

Hakuna mbunge mwenye vision wa ccm Bungeni, Hawajui washike lipi na Waache wapi

Aina ya wabunge kama hao walienda Bungeni kimkakati kwa ajili ya kubadili katiba

Hakuna mbunge anayewaza lini Tanzania tutakuwa na kiwanda cha magari yetu ya umeme wa jua

Hakuna mbunge anayewaza kubadili chuo chetu Cha Muhimbili au udsm kuwa centre za utafiti na uvumbuzi wa chanjo za magonjwa ya virusi

Kazi kubwa wanayoweza Bunge hili ni kuvamia misiba, Kukata mauno, na kujadili Mbowe na Chadema

Hawana Forecast

Sent from my INE-LX2 using JamiiForums mobile app
Forecast °=Focus
 
Tunaofanya burudani za viwanjani tumekuwa tukipigia sana simu Babu zetu vijijini wazuie mvua, katika hotuba ya Waziri sijaona akisema ujenzi wa Sports Arena, hakuna msanii asiyejua kama mimi ndiyo naongoza kufunga mvua, Waziri naomba unipunguzie hii kazi".

======

Mbunge wa Morogoro Kusini, Khamisi Taletale amesema huwa anawapigia simu wazee vijijini ili wazuie mvua kuruhusu shughuli za kimziki ziendelee.

Amesema Hotuba ya Waziri wa Ujenzi haijazungumzia kujenga Viwanja vya Michezo na Burudani hali ambayo itamfanya yeye aendelee na kazi ya kuendelea kuomba wazee wafunge mvua ili kufanya shughuli za Burudani.

Amemuomba Waziri ampunguzie kazi hiyo kwa kuwa yeye ndiye anayeongoza kufunga mvua nchini.
Kama nchi, tuna safari ndefu sana, badala yakujadili namna ya kuwekeza kwenye sayansi, wawakilishi wetu wanajisifia bungeni namna wanavyopotosha uhalisia wa sayansi
 
Back
Top Bottom