Babu Tale amuomba Waziri ampunguzie kazi ya kuzuia mvua

Babu Tale amuomba Waziri ampunguzie kazi ya kuzuia mvua

Hivi unaijua arena ?

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
Aliposimama alizungumzia kuhusu arena tu?!!hayo mambo ya jina la rais, na kuzuia mvua, umeyaacha wapi?kifupi hana uwezo wa kujenga hoja, na ni kutokana na kiwango chake cha elimu , hivyo tutegemee mengi tu, siku zote elimu haina janja janja, kuna sehemu utakwama tu,
 
Azuie na baridi Matombo, Mahenge, Arusha, Lushoto, Mufindi, Makete, Njombe na Mbinga.
Shukurani!

Everyday is Saturday................................😎
Baridi hana maslahi nalo inavyoonesha
 
Taletale leo amekubali mbele ya bunge ye ni mchawi wa kufunga mvua kuhusu kumtoa mke wake kafara anakataa hakuna uchawi bila kafara aache ujinga.


Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Awali niliposikia tetesi kuwa mwanaccm mwenzangu na mbunge wa Morogoro kusini babu Tale kuwa ni mchawi niliwabishia na kuwaambia Tale ni mwanamazingaombwe.

Lakini leo yeye mwenyewe babu Tale ndani ya bunge amekiri kuwa mara nyingi amekuwa akizuia mvua isinyeshe na mazao yanyauke ili mradi tu timu za mpira wa miguu zicheze na vijana wanaocheza kamari mikeka yao iweze kujibu.

Ama kwa hakika uchawi upo unaumiza wakulima kwa sababu ya kamari?

Niishie hapo!
🤣
 
Huyo ndiye Komredi Khamis Tale!!

Uzalendo wake kwa mila na tamaduni za mwafrika ni mkubwa kupita kiasi....

Vijana wanapiga Pesa kupitia juhudi zake hizo......asipuuzwe kabisa 🤣

#SiempreCCM
#KaziIendelee
 
Wabunge wa ccm wapo peke yao Bungeni lakini wanajadili hoja za kijinga na mambo ya kitoto sana

Hakuna mbunge mwenye vision wa ccm Bungeni, Hawajui washike lipi na Waache wapi

Aina ya wabunge kama hao walienda Bungeni kimkakati kwa ajili ya kubadili katiba

Hakuna mbunge anayewaza lini Tanzania tutakuwa na kiwanda cha magari yetu ya umeme wa jua

Hakuna mbunge anayewaza kubadili chuo chetu Cha Muhimbili au udsm kuwa centre za utafiti na uvumbuzi wa chanjo za magonjwa ya virusi

Kazi kubwa wanayoweza Bunge hili ni kuvamia misiba, Kukata mauno, na kujadili Mbowe na Chadema

Hawana Forecast

Sent from my INE-LX2 using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tunaofanya burudani za viwanjani tumekuwa tukipigia sana simu Babu zetu vijijini wazuie mvua, katika hotuba ya Waziri sijaona akisema ujenzi wa Sports Arena, hakuna msanii asiyejua kama mimi ndiyo naongoza kufunga mvua, Waziri naomba unipunguzie hii kazi".

======

View attachment 1805289

Mbunge wa Morogoro Kusini, Khamisi Taletale amesema huwa anawapigia simu wazee vijijini ili wazuie mvua kuruhusu shughuli za kimziki ziendelee.

Amesema Hotuba ya Waziri wa Ujenzi haijazungumzia kujenga Viwanja vya Michezo na Burudani hali ambayo itamfanya yeye aendelee na kazi ya kuendelea kuomba wazee wafunge mvua ili kufanya shughuli za Burudani.

Amemuomba Waziri ampunguzie kazi hiyo kwa kuwa yeye ndiye anayeongoza kufunga mvua nchini.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] bunge la vibungi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wa morogoro kusini wamelamba hasara kua na mbunge mbumbumbu kama huyu Tale ...hajawahi kuongea point toka alivyoingia bungeni ni porojo tu.
 
Back
Top Bottom