Babu Tale meneja bora, Mbona hawalipii kina Madee, Tundaman video za gharama kama WCB?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
habari wadau..

nimekutana na tunda man nikakumbuka ni msanii wa tip top na bosi wake ni babu tale...

naona bosi kama ana upendeleo vile.. nikitazama video za WCB ni za ukweli zinafanyika sana majuu.. na nikichek video za Madee, tundaman, dogo janja naona sio za kiwango cha kupigwa vituo vikubwa africa...

je bosi anapendelea au nae WCB hafanyi maamuzi yeyote ya video anajiganyia diamond tu???
 
Kwa mwenye uelewa kuhusu mameneja wa wasanii wa bongo naomba msaada kujua kazi zao hasa ni nini kwa wasanii
 
Mwenye nacho huongezewa. Dai mjanja anajua kujiongeza tofauti na hao uliowataja hasa dogo janja sijui ile kiki ya ndoa ikiishia wapi
 
Wabongo uwa mnadhani meneja ndiye anagharamia msanii hapana haiko hivyo...
Msanii ndiye anamwajiri meneja na gharama za studio na za video zinatoka kwenye fungu la msanii.
So usilaumu babu tale kuhusu video za tip top
 
Babu tale na Salaam wapo WCB kama waajiriwa tu. Kiufupi tale na Salaam ndio wanalipwa na diamond baada ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku waliyopangiwa na Diamond. Kiufupi dogo Mond namuona kama Didy wa bongo vile jinsi anavyopiga hatua. Japo mm ni mzee wa riddim mix, Ila Mungu ampe uzima huyu kijana. Mpambanaji sana huyu kijana..
 
We unafikiri Babu Tale anasaidia watu kama Red Cross?
 
Kwa uelewa wangu mduchu,,,,WCB haipo chini ya babu tale wala salam iko chini ya Baba tiffah sasa inapokuja kwenye mambo ya shooting baba t ndie anaeamua ifanyikie wapi kulingana na mfuko wao unavyowaambia ila sio tale so na hao wengine kipato chao kikiongezeka pia tutaona video zenye kiwango na ndio maana hawalalamiki sababu wanajua pato lao likoje
 
hahaa mkuu mi naamin issue za pesa zote anasimamia diamond
 
Dua zako zitimie, Amina. Mchizi ana moyo sana wa kuwasaidia wenzake. Wacha aendelee kufanikiwa.
 
Mkuu wamiliki wa Wasafi ni Diamond,Tale,Sallam na Saidi Fela.

Alafu kuna meneja pale kama Ricardo Momo,Sallam,Tale na Saidi Fella.

Kwa hiyo usidanganyike kuwa Diamond anawalipa mishahara kina Tale wale ni Maboss zake au Maboss wenzake ile ni Kampuni na wanagawana faida sio kuwalipa mishahara.
 
Kimsingi Babu Tale sio bosi wa WCB ila ni muajiriwa na anavuna vizuri kuliko anavyovyuna TipTop. Na ndio maana ameitelekeza TipTop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…