Babu Tale: Naweka V8 ya mwaka 2020, Mwakinyo apigane na Kiduku

Babu Tale: Naweka V8 ya mwaka 2020, Mwakinyo apigane na Kiduku

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mbunge wa Morogoro Kusini, Khamis Tale maarufu kama Babu Tale amesema ataleta gari aina ya V8 ya mwaka 2020 ili kuwashindanisha Hassan Mwakinyo na Twaha Kiduku

Maneno hayo ameyasema baada ya Twaha kumtwanga Dulla Mbabe kwa mara nyingine, huku lengo likiwa ni kupambana na Mwakinyo

Mwakinyo ameweka msimamo wake kuwa hatopambana na bondia wa ndani ya nchi lakini inaonekana wadau wanapenda kuona mpambano unatokea kati yao

Wadau wa Morogoro wanalalama kuwa lazima tuwe na mbabe mmoja nchini sio wawili

Kwa suala la uzito, Twaha alikubali kukata ili aufuate uzito wa Mwakinyo

Hela zinazidi miminika.

Je zichapwe!!!
 
Kiduku atoke kwanza nje ya Tanzania tuone
 
Hamna shortcut, Kiduku apambane afike juu levo ya mwakinyo kidaraja kisha apunguze uzito atapigana na Mwakinyo
 
Hamna shortcut, kiduku apambane afike juu levo ya mwakinyo kidaraja kisha apunguze uzito atapigana na Mwakinyo
Hizo uzito huwa una side effect gani. Kwani hawawezi kupigana mpaka wote wawe na the same weight?
 
Mbunge wa Morogoro Kusini, Khamis Tale maarufu kama Babu Tale amesema ataleta gari aina ya V8 ya mwaka 2020 ili kuwashindanisha Hassan Mwakinyo na Twaha Kiduku

Maneno hayo ameyasema baada ya Twaha kumtwanga Dulla Mbabe kwa mara nyingine, huku lengo likiwa ni kupambana na Mwakinyo

Mwakinyo ameweka msimamo wake kuwa hatopambana na bondia wa ndani ya nchi lakini inaonekana wadau wanapenda kuona mpambano unatokea kati yao

Wadau wa Morogoro wanalalama kuwa lazima tuwe na mbabe mmoja nchini sio wawili

Kwa suala la uzito, Twaha alikubali kukata ili aufuate uzito wa Mwakinyo

Hela zinazidi miminika.

Je zichapwe!!!
Kambi ya Mwakinyo inataka dau la $2,000,000/- ili apigane na Twaha Kiduku siyo V8 ya 2020.
 
Mwakinyo anaogopa aibu. Ki ukweli sijawahi kuelewa ubondia wa mwakinyo na hana uwezo wa kumpiga twaha
 
Aisee, mwakinyo si alisema hataki kupigana na bondia yoyote wa ndani au waweke madolari ambayo team mwakinyo wametaka Sasa hayo ma Toyota ya Nini?.....watu wanataka pesa mi gari ya nn sasa. Au pesa ya iyo gari ilete bondia from abroad....itakua raha hizi harakati tuhamishie uko abroad kwa nguvu zote...
 
Watanzania wenzangu, mwenzetu Mwakinyo ni professional boxer hawezi kupigana na street boxer... maisha yana level...
 
Aisee, mwakinyo si alisema hataki kupigana na bondia yoyote wa ndani au waweke madolari ambayo team mwakinyo wametaka Sasa hayo ma Toyota ya Nini?.....watu wanataka pesa mi gari ya nn sasa. Au pesa ya iyo gari ilete bondia from abroad....itakua raha hizi harakati tuhamishie uko abroad kwa nguvu zotupo e...
Itakuwa Gari ya diamond
 
Hizo uzito huwa una side effect gani. Kwani hawawezi kupigana mpaka wote wawe na the same weight?
Sheria za boxing zinahitaji uzito uwe sawa au kuzidiana not less than 5kgs
Ndio maana uzani wa ngumi upo kuanzia amateur mpaka heavy weight
 
Mwakinyo anaogopa aibu. Ki ukweli sijawahi kuelewa ubondia wa mwakinyo na hana uwezo wa kumpiga twaha
Ni taratibu tuu za mchezo mwakinyo kwa sasa ni global champion twaha hajafanya international games za UBO, WBO etc sasa atawezaje kufika rank io anatakiwa nacheza mapambano yanayofanana na Mwakinyo ashinde kisha aombe nae match bado ni harmatcher tuu kwa mwakinyo
 
Back
Top Bottom