Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila dingi alikuwa mjasiriamali sana hata dhalim na jeuri yake alipigwaView attachment 92496
Stori:Mwandishi Wetu
Katika kuonesha kuwa Mchungaji Mstaafu, Ambilikile Mwasapile ‘Babu wa Loliondo' bado ana fedha baada ya kuzikusanya kutoka kwa wateja wake wa huduma ya kikombe, hivi karibuni alinaswa ndani ya Benki ya NMB akipata huduma.
Babu alibambwa ndani ya benki hiyo Tawi la Loliondo mkoani Manyara akihudumiwa na mmoja wa wafanyakazi aliyefahamika kwa jina la Lembris Lesion ambapo inaelezwa alikuwa akielekezwa jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya Jisevie.
Akiwa benki hapo, Babu alionekana akijaza fomu huku akiwa na begi ambalo linashukiwa kuwa na fedha ndani yake ambapo baadhi ya watu waliokuwa wakimpiga chabo hawakuonesha kumshangaa wakiamini bado ana mkwanja wa kutosha kutokana na ile tiba ailiyokuwa akiitoa kwa watu wengi hivi karibuni.
"Unajua Babu alipata pesa nyingi sana na bado anaendelea kuzikusanya, kimsingi ana pesa ndefu benki," alisema mmoja wa wateja aliyekuwa eneo hilo. GPL