Jamani jaribuni kuwa na busara ya upembuzi. Babu aliposema watu wasirudie alikuwa na maana kuwa mtu ukinywa uondoke eneo lile, uendelee na dawa zako ukiwa na imani kuwa itakusaidia kupona.
Angeruhusu kurudia na jinsi binadamu anavyopenda kupona haraka, watu wasingebanduka kule mpaka wahakikishe wamepona ndo warudi makwao.
Lakini basi kwa kuwa kuna waliopona kwa kufuata utaratibu, na waliokufa kwa kutokufuata taratibu; wanaotaka kupona kwa sasa ni ruksa kwenda tena lakini kwa utaratibu ule ule kwamba kikombe kimoja halafu unachapa yebo.
Mnaombeza babu kuwa dawa yake ni hatari, ulizieni taarifa ya utafiti ya NIMRI juu ya dawa hiyo. Mbona mpaka leo hawajathibitisha wala kuipinga. Kwa utaratibu mtu ukikaa kimya inamaana umekubali.
Nawasilisha.