Babuuu huyoo Loliondo

Huyu babu hajui mambo mengi sana tu!
-Hajui hata hiyo dawa yake inaota vipi? na ipo kiwango gani hapo Loliondo!
Ataendelea kuivuna bila kupanda mpaka lini?
Hajui wagonjwa hao anaowatibu kama kweli wanaumwa magonjwa hayo au vipi?
Hajui wagonjwa wangapi kawahudumia mpaka sasa na wangapi wamepona?
Hajui wasiopona ni wangapi na sababu za kutopona ni zipi!
Hajui-------
Hajui--------
Hajui, hajui, hajui
Na wanaoenda kutibiwa kwake hawajui vilevile!
 


Hivi vipofu wawili wakipoteza fimba zao hawezi kujitokeza mtu mwenye hisia za utu akawasaidia? Ina maana nchi hii sote tumekuwa vipofu?
 
"Huyu babu anajua nini kuhusu ARVs?"

una uhakika gani kama hajui, na kama mtu amepona kuna haja gani ya kutumia ARV's?
 
wale wote mnaobisha nadhani mpo nje ya tanzania ..nenda arusha ukajionee sio unapiga makelele tu hapa!! unadhani wewe ndio una akili kuliko viongozi wako wa nchi ambao wameiruhusu hii huduma iendelee? wtf with ARV sijui ARS wewe ndio umezitengeneza hizo ars ??
 
NI HERI TUNDELEE KUSEMA ILI IONEKANE TOFAUTI YA WAO NA SISI, KULIKO KUNYAMAZA TUKAONEKANA AFADHALI YA WAO KULIKO SISI! Ama wakatufananisha nao..... kweli Tanzania kuna wasomi kwa hili la babu NIMEAMINI!! Hatuna hata uthubutu wa kujiuliza KWANINI?

Ndiyo maana kila siku naimba Tatizo la Tanzania si ccm, leo hii ukificha kamera yako mitaa ya babu utashangaa akina Mbowe,Mrema wanavyomiminika huko.

Ulaya ktk karne ya 15-16 waliteketeza ushirikina kwa serikali kushirikiana na makanisa kwa kuwachapa risasi watu kama BABU wa leliondo.
Leo hii humu watu wanamshabikia babu, lakini babu akibaunsi na watu kufa kama utitiri utatusikia humu ma great sinker tunavyokula U-turn na kui-condem serikali vibaya sana kwamba ilikuwa wapi?

Hata hivyo yawezekana babu anatibu, mimi nawashauri serikali wapeleke wagonjwa kutoka hospitalini wakanywe kikombe cha babu, harafu baada ya mda wawatest. ikionekana babu mwongo wam-arrest na ikiwa babu mkweli wampe noble.
 
Wewe ndio walewale "zidumu fikra za mwenyekiti Zidumu"
Kwani viongozi ni nani? mbona siku hizi ndo wanafanya Madudu mengi mpaka kinyaa!
 
Mkuu,

Sina hamu na nchi hii. Mtoto analia, mama naye anaangua kilio na libaba nalo limeungana nao kulipua vilio!

We are totally doomed!!!


Ndo maana Jenarali anatusaidia hapa
mkuu, kweli Jenerali anatusaidia lakini je katika nchi hii nani atamwambia Mfalme kuwa yu uchi na hali raia wote tu uchi? Ikiwa twajiona tumevaa na tunalithibitisha hilo je nani tutamsikiliza na kumuamini kuwa tuko vile tusivyotakiwa kuwa? Tanzania ni Nchi ya ajabu sana duniani.... UFISADI NI SIFA! Wizi wa mali ya UMMA ni KIPAJI kinachostahili pongezi! Matumizi mabaya ya mali za umma ni SHEREHE! Kwenye maslahi binafsi hakuna kupingana hata kama bajeti ya elimu itanyofolewa! sijui... sijui... saa zingine mtu unawaza kutokomea kabisa uondokane na uoza huu! lakini je utakaowaacha si ndio utakuta wamekwisha kabisa! Nchi ina rasilimali tele...maskini wa kutupwa! Leo hii mawe tu yaliyojaa nchi hii wala huhitajii madini yoyote kujenga uchumi zaidi ya hayo lakini aaagh! HERI BABU AENDELEE KUWEPO kwa maana nayo ni kipimo tosha KWANINI WATANZANIA Ni MASkINI!!!
 

Kwa hiyo wewe unaamini kuwa viongozi wa nchi lazima wa akili kuliko watu wengine wote?


Tumekwisha!!
 


Tatizo letu hata hatulijui. Wote tuko kama wagonjwa wa vichaa. Kila mtu anamwona mwenzake ndiye mgonjwa na kwamba yeye mwenyewe ni mzima. Ila tatizo langu ni moja tu...kwamba nchi yetu ina laaana gani kwamba hata kama sote tu vichaa asiwepo kichaa mwenye unafuu kidogo akatukomboa?
 

nilizungumziA Issue nzima ya placebo.. wadau wakanivamia kwamba sijui chochote..?!! neways tutafika tu mkuu
 
hapo ndipo unapogundua akili za Watanzania....hatujiulizi mara mbili....kiongozi akijisaidia hadharani basi ni mfano wa kuigwa!!! Ni wapumbavu pekee wanaokubaliana kwa kila jambo! Nitaendelea kulipinga hili mpaka ukweli wake utakapojulikana. Nitaendelea kukataa kuwa miongoni mwa wanaofuata mkumbo kwa sababu ya fulani... NAOGOPA SANA KUSEMA KATIKA HILI LA BABU... KUNA MIKONO YA WATU!!!
 
TUNA ZAIDI YA UKICHAA NA KAMA NI LAANA Basi aliyetulaani nae alilaaniwa akafa na LAANA YAKE na YETU! Ukiona nchi inaendeshwa kwa imani basi shukuru Mungu uende zako! Maana iko siku watu wataaminishwa kitu cha hatari sijui itauwaje!! Mkuu heri kusema kuliko kunyamaza.. labda inawezekana TUKAPONA HAYA MARADHI SUGU!
 
Kwa hiyo wewe unaamini kuwa viongozi wa nchi lazima wa akili kuliko watu wengine wote?


Tumekwisha!!
saa zingine unaweza kucheka kwa uchungu mkuu!! hao ndio sisi watanzania.... kiongozi flani amesema...
na viongozi wenyewe ndio hawahawa AKILI kuambiwa!?

Kweli "waacheni wafu wawazike wafu wao"
 

Mkuu lazima tuseme kwa sababu tupo (hata kama ni wachache) tusioamini mambo ya kijinga jinga na kishirikina. Tunaweza kubezwa kwa njia yoyote ile ila bahati nzuri mwisho wa siku kila kitu huenda kama tunavyowaeleza watu.

Hakuna mtu hata mmoja dunia hii anayeweza kutoa hizo tiba za imani/kishirikina kama za Babu wa Loliondo...Mimi naamini hakuna. Wale wanaoamini tofauti na mimi waendelee na imani zao.

Hata wakati wa DECI tuliwaeleza watu wakataka kututoa macho kwamba tuna wivu na hatatuki wapate maendeleo. Tatizo langu ni pale ambapo hata waleo waliotakiwa kusimama mbele yetu kutuongoza wanapogeuka kondoo vibogoyo badala ya wachunga kondoo.
 

AFRIKA HAKUNA MATATA!! ... hehehe!! Hii picha inathibitisha wazi wa TZ tunavodanganyika kirahisi na tunavyopenda njia za mkato.

DAWA YA UKIMWI NI MOJA TU!!! ACHA NGONO ZEMBE!! ..
 
AFRIKA HAKUNA MATATA!! ... hehehe!! Hii picha inathibitisha wazi wa TZ tunavodanganyika kirahisi na tunavyopenda njia za mkato.

DAWA YA UKIMWI NI MOJA TU!!! ACHA NGONO ZEMBE!! ..

Mbona nimesikia kuwa kuna baadhi ya vijana wameshakimbilia huko kutafuta wachumba? Nadhani mwisho wa siku wataupata wengi hapo kwa Babu!

Hili bomu nadhani litalipuka wakati wowote...Yangu macho!
 

Kaka temea mate chini ni mangapi yamewashinda hao wazungu wako ambayo yametatuliwa na nguvu za mungu.usizungumze kabla hujaona.nenda katibiwe acha ubishi wa kijinga
 
Kaka temea mate chini ni mangapi yamewashinda hao wazungu wako ambayo yametatuliwa na nguvu za mungu.usizungumze kabla hujaona.nenda katibiwe acha ubishi wa kijinga

JF kuna mambo!! Penye wengi kuna mengi!

Ngoja nikalale mie!
 

Wajanja wanapopewa chai na kuambiwa ni dawa. Kweli watanzania tumeanza kufirisika kimawazo kila jambo TUTALIAMINI kwa kuwa hakuna pa kushika.

Yaani huyon jamaa mwenye kikombe chekundu ni kama anasema"" tayariiiii""" maaana unaweza kukuta kasubili kwa wiki saba.

Thidanganyikiiiiiiiiiiiiii na manabii wa uongo waliotabiliwa kwenye bibilia....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…