Kisa chetu sisi binadamu tunaojidai ujuaji kinafanana na hidisi hii. Mtu mmoja alikuwa anasafiri yeye pomoja na mtoto wake na alimwamuru mtumwa wake amtandikie punda wake, na ndipo alipoanza safari. Alifika kijiji cha jirani akiwa amempanda punda na mwanawe akifuatana nae. Watu walipomwana wakasema huyu mzee vipi? Hana hata haya? Inakuwaje yeye anampanda punda huku akimwacha mwanawe atembee kwa mguu? Basi mzee kwa kusikia hayo alishuka kwenye punda akampakia mwanawe na yeye akifuatana nae kwa miguu. Alipofika katika kijiji kilichofuata watu wakamshangaa sana yule mtoto na kwamba hana adabu, inakuwaje apende punda yeye ilhali babae anaenda kwa miguu?. Basi kwa yale maneno ikabidi baba na mtoto wote wampande yule punda kwa pamoja. Walipofika kijiji kilichofuata watu wakawastajabia sana kwa kuwashutumu kwamba hawana huruma wala hawathamini haki za wanyama, ni kwa nini wanampanda huyu punda kwa pomoja hawajui kwamba wanamsababishia maumivu?. Basi kwa mashutumu hayo, mzee akaamua sasa watembee wote kwa miguu yao bila kumpanda punda huku wakiambatana na punda wao. Na walipokuwa wanakatiza kijiji kilichofukua kinafuata watu waliwacheka sana kisa ni kujitesa kwa kutembea kwa miguu ilihali wana punda wa kuwasaidia kuwabeba? Basi yule mzee akamgeukia mwanae na kumwambia ukiyamaliza mashutumu ya wanadamu unaingia kifoni.
Ndivyo tufanyavyo wale wasio elimu, wenye elimu ya kati na wale wenye ya juu, sooote mwisho wa safari yetu ni kifo. Ni kundi gani kati ya hayo matatu linaloweza kukwepa ama kuimalizia safari yao kwingineko?
.