Babuuu huyoo Loliondo


Kinyambisi, umeeleza vizuri sana ila mwishowe umeonesha kuchanganyikiwa. Ungeweka wazi tu kwamba huyu BABU NI MWONGO...fulll stop! Laws za nature hazikubaliani na hayo mambo na tumeshuhudia vitu vingi sana vinavyozitumia jinsi ambavyo vimefanya mapinduzi makubwa katika maisha ya binadamu. Hakuna ushahidi hata mmoja ambao unaonesha kuwa maisha ya binadamu yameboreka kwa njia ya imani za kishirikiana kama hizo za babu. Anyone can prove me wrong and I will shut off!
 

Wanasayansi wameshindwa kazi. Mafungu yote ya tafiti sasa yaondolewe kwenye bajeti za nchi zote duniani badala yake watafiti wa dawa za kienyeji wajengewe uwezo zaidi.
 

Kukataa moja kwa moja nashindwa kwa sababu:
Kabla dawa za kisasa ama wazungu hazijaja, tulikuwa na dawa zetu nzuri toka kwenye miti yetu.
Walipokuja wazungu wakaziita ushenzi, matokeo watu wakaenda kanisani na kuzikataa wakiziita ushenzi na kuacha kuendelea kuzirithisha kwa vizazi vyao. Zikabaki kwa wachawi na waganga wa kienyeji ambao hawakuukubali ujumbe wa mzungu moja kwa moja na hadi leo wanazifanyia kazi na matokeo yapo japo mengine kisayansi hayathibitiki (watu waliokufa wanatokea tena wazima, watu wanaotibiwa kwa sangomas wanapata nafuu etc.).
Nimetibiwa kwa dawa za Asia - China ni mitishamba mitupu. Wao wenzetu waliendelea kuheshimu mila zao na dawa zao za miti na wamezifanyia utafiti zinatumika mahospitalini kwao japo vipimo ni vya kisasa. Nasema nimetibiwa na dawa hizo na nimepona kabisa.

Sasa hapa kukataa moja kwa moja kwamba dawa ya Mchungaji ni kiini macho kwa mie niliyeishatumia dawa za mitishamba toka taifa lingine nashindwa. Labda sana sana kama imani ya kukubali moja kwa moja inatia shaka, naweza kuamini kuna siri ambayo babu hajaamua kuisema. Pengine kuna kamzizi kengine anakoongezea kwenye hiyo dawa yake ambako, hajaamua kukataja. Angalau hilo nadhani linawezekana.
 

Nikuulize swali moja tu Viper. Hivi huamini kuwa kuna MIUJIZA ya Mungu? Kama umeshawahi kuona miujiza basi amini hii ni mojawapo ya miujiza ya Mungu kuponya viumbe wake maana magonjwa yamezidi. Ukifuatilia sana Sayansi unaweza kuamini kuwa HAKUNA MUNGU, na hapo utapingana na wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…