Baby Madaha: Sioni faida ya msanii kuhangaika na Serengeti boys

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
xBaby-Madaha-300x194.jpg.pagespeed.ic.P7YqzUncb2.jpg

Msanii wa filamu Bongo, Baby Madaha amesema kuwa na mpenzi mwenye umri mdogo kwake haoni kama kuna faida yoyote.

Wasanii wa kike wa filamu Bongo wameonekana kuanzisha style mpya kwa kuwateka kwenye mahusiano wasanii wadogo wa muziki na kuwaingiza kwenye himaya zao za mapenzi kama ilivyokuwa kwa Shilole na Nuh Mziwanda, Nisha na Baraka da Prince, Jacquline Wolper na Harmonize, na sasa ikidaiwa kuwa Raymond tayari kashanasa kwenye mtego wa Nisha.

Akiongea na gazeti la Mtanzania, Baby Madaha alisema, “Sijawahi kuwaza kama nitakuwa na Serengeti boy kwangu hawana nafasi sioni faida yoyote kwao, mimi nawashangaa kwa kuwa wengi wao wanatafuta umaarufu hakuna mapenzi wala maisha endelevu hapo.”

Aidha Baby amewataka wasanii wenzake kuwa na wanaume wenye umri wao ama wawe na wanaume watu wazima kama wanataka kulinda heshima zao na kujiongezea mashabiki badala ya kuwa na wanaume wenye umri mdogo.
 
Mbona yeye alimegwa na Kala Jeremiah atukusema kitu.
Mijitu kama hii ndio inasababisha tukose majimama ya kuwachuna.
 
Aendelee na vibabu vyake, na wao waendelee na viserengeti vyao.... Maisha yenyewe yako wapi
 
Sasa Serengeti boys hawana faida, kama anauza.
 
Duhhh ....Mzungu wa haja..... Glutathione at work......

xBaby-Madaha-300x194.jpg.pagespeed.ic.P7YqzUncb2.jpg

Msanii wa filamu Bongo, Baby Madaha amesema kuwa na mpenzi mwenye umri mdogo kwake haoni kama kuna faida yoyote.

Wasanii wa kike wa filamu Bongo wameonekana kuanzisha style mpya kwa kuwateka kwenye mahusiano wasanii wadogo wa muziki na kuwaingiza kwenye himaya zao za mapenzi kama ilivyokuwa kwa Shilole na Nuh Mziwanda, Nisha na Baraka da Prince, Jacquline Wolper na Harmonize, na sasa ikidaiwa kuwa Raymond tayari kashanasa kwenye mtego wa Nisha.

Akiongea na gazeti la Mtanzania, Baby Madaha alisema, “Sijawahi kuwaza kama nitakuwa na Serengeti boy kwangu hawana nafasi sioni faida yoyote kwao, mimi nawashangaa kwa kuwa wengi wao wanatafuta umaarufu hakuna mapenzi wala maisha endelevu hapo.”

Aidha Baby amewataka wasanii wenzake kuwa na wanaume wenye umri wao ama wawe na wanaume watu wazima kama wanataka kulinda heshima zao na kujiongezea mashabiki badala ya kuwa na wanaume wenye umri mdogo.
 
Heshima na Hao mashabiki aliowapata wakati anatembea na watu wazima ni wepi?
 
Back
Top Bottom