'Baby walker' yangu inataka kunipasua kichwa!

Mlolongo, mbona unaona aibu kutaja aina ya gari yako? Hivi ungekuwa na BMW au Mercedes Benz, ungeona aibu hii uinayo sasa?
 
Aiseeh hii kali!! Ist/passo si zipo nyingi sana mjini sasa atajuaje
Anafaham eneo naloishi. Lakin exact mtaa haujui. Na anajua nina gari ndogo.
Kwa msala ule aliniachiaga mpaka kunitumia 'ma-baunsa' aisee niko chonjo.
 
Kwani mkuu kwenye mteremko ukiweka neutral na kukanyaga break gari litaserereka?
Mkuu... Heshima yako kwanza.

Story iko hivi.
Gari za siku hizi (zinazotumia umeme) ili iwake (ignition) lazima gear iwe kwenye Parking au Neutral.
Sasa tatizo ni kuwa Parking haioneshi, maana yake the only option ni kuwasha gari ikiwa kwenye Neutral.

Haya, unasema kukanyaga brake, brake za gari ya umeme haifanyi kazi kama gari haijawaka.
Na ndio maana ukijaribu kukanyaga brake wakat gari imezima utaona kabisa brake pedal haishuki chini. Mpaka engine iwake.

Kwahiyo nawashaje gari:
Naingia, nachomeka funguo, naweka Neutral (Foot Brake Haina kazi hapa, maana gari imezima), kisha nazungusha funguo. Kama gari ilikua kwenye mteremko lazima isereke kidogo kisha inasimama kwa msaada wa 'Hand Brake'.

Kuserereka nakomaanisha ni pale gari haijawaka, ndio umeweka Neutral unataka uiwashe sasa. Kumbuka hapo foot brake haifanyi kazi maana engine haijawaka bado.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…