'Baby walker' yangu inataka kunipasua kichwa!

'Baby walker' yangu inataka kunipasua kichwa!

Mkuu... Heshima yako kwanza.

Story iko hivi.
Gari za siku hizi (zinazotumia umeme) ili iwake (ignition) lazima gear iwe kwenye Parking au Neutral.
Sasa tatizo ni kuwa Parking haioneshi, maana yake the only option ni kuwasha gari ikiwa kwenye Neutral.

Haya, unasema kukanyaga brake, brake za gari ya umeme haifanyi kazi kama gari haijawaka.
Na ndio maana ukijaribu kukanyaga brake wakat gari imezima utaona kabisa brake pedal haishuki chini. Mpaka engine iwake.

Kwahiyo nawashaje gari:
Naingia, nachomeka funguo, naweka Neutral (Foot Brake Haina kazi hapa, maana gari imezima), kisha nazungusha funguo. Kama gari ilikua kwenye mteremko lazima isereke kidogo kisha inasimama kwa msaada wa 'Hand Brake'.

Kuserereka nakomaanisha ni pale gari haijawaka, ndio umeweka Neutral unataka uiwashe sasa. Kumbuka hapo foot brake haifanyi kazi maana engine haijawaka bado.
Mkuu umeandika vizuri ila navyojua mimi hata engine iwe off, brakes zipo sema unahitaji kuvumia nguvu kidogo wakati unazikanyaga.
Ukipark gari kwenye muinuko hand brake/ parking brakes ndo zinatakiwa kulifanya gari lako lisiserereke na sio gear ya parking, Hiyo ipo hapo kama assuarance kuwa gari haliendi popote.
Kutumia "P" kulishikilia gari lako kwenye muinuko kunawezekana ndo chanzo cha matatizo hayo.
Mimi nikikupa gari ukarudisha umepark bila kuweka hand brake, siku nyingine hulipati!
 
Uzuri jamaa yupo Shekilango pembeni ya Rombo Bar pale.

Kama una muda kesho nenda akuchekie. Ila likija swala la kubadirisha vimiminika peleka sehemu husika au kanunue mwenyewe. Usiwaachie hao jamaa.

Hamis Fundi (Shekilango): +255714504214

Nenda nalo mwenye pale gereji kwake Shekilango. If possible ongea nae sahivi mwambie kanipa jamaa wa Runx.
Hamisi ntu makini
 
huyu mtu sijamuelewa,anazungumzia tatizo la IST then anasema IST Passo
kuna gari inaitwa IST Passo? au anamaanisha gari zote mbili zina tatizo moja
 
huyu mtu sijamuelewa,anazungumzia tatizo la IST then anasema IST Passo
kuna gari inaitwa IST Passo? au anamaanisha gari zote mbili zina tatizo moja
Mtoa mada kaandika IST/Passo maana yake ni moja wapo Kati ya hizo na ame weka wazi sababu ya kuandika hivi comment za juu hapo

Wewe mkosoaji Una andika ISTPasso huoni wewe ndo huja elewa nini kime andikwa hapa ili hali kutaka kuonesha ndo Una fahamu zaidi haya magari
 
Mtoa mada kaandika IST/Passo maana yake ni moja wapo Kati ya hizo na ame weka wazi sababu ya kuandika hivi comment za juu hapo

Wewe mkosoaji Una andika ISTPasso huoni wewe ndo huja elewa nini kime andikwa hapa ili hali kutaka kuonesha ndo Una fahamu zaidi haya magari
Andamana
 
Babywoka yangu (IST/Passo)

Tatizo la kwanza limeanza juzi:
Nimerudi jioni home, nikapaki nikaingia ndani. Usiku nikawasha gari nilisogeze getini nikashangaa 'Parking' gear haioneshi kwenye dashboard.

Yaani 'Parking' haionekani kwenye dashboard ingawa gear ipo kwenye Parking. Gear zingine zote zinaonekana. Nikizungusha funguo niwashe (ignition) haiwaki, mpaka nipeleke kwenye 'Neutral' ndio inawaka.

Tatizo la Pili (Limeanza Leo):
Nalo linahusiana na Mambo ya gear, sema ni wakati naendesha (nipo kwenye mwendo).

Kuna muda nikiwa naendesha (nipo kwenye D) nikakanyaga mafuta kuongeza mwendo zaidi gari inapiga kelele za Race gyyyyyyym.
Ni ile sauti ya ukikanyaga mafuta gari ikiwa kwenye parking. Sasa mimi naisikia nikiwa kwenye mwendo.

Hii imenitokea mara mbili, na inapotokea inabidi niachie mafuta kisha nikanyage tena mdogo mdogo ndio inarudi kwenye hali ya kawaida.

Wakuu, haya matatizo mawili yatakua na uhusiano? Yanaweza kuwa chanzo ni kitu gani? Spark plugs, Coil, nozzle, transmission fluid ama yaweza kuwa Nini wakuu.

Yaani kuwasha gari mpaka niweke Neutral (Kama kuna mteremko gari inaanza kuserereka duh)

Na hiyo ya kupiga resi (kupoteza gear ghafla) napokua nakanyaga mafuta kuongeza mwendo.
Babywalker nayo ni gari ya kuja humu kweli kuomba msaada?.Si una nunua nyingine tu.
 
Anafaham eneo naloishi. Lakin exact mtaa haujui. Na anajua nina gari ndogo.
Kwa msala ule aliniachiaga mpaka kunitumia 'ma-baunsa' aisee niko chonjo.
mmh ulimtoa wapi wa dizain hiyo..mpaka mabaunsa!! ulimfanyia nini?
 
mmh ulimtoa wapi wa dizain hiyo..mpaka mabaunsa!! ulimfanyia nini?
Kuna mali alikua anauza, tukaelewana fresh nikamtumia advance (nusu ya pesa). Akaanza kuniletea uswahili, Sasa sijui ndio alitaka kunitapeli au vipi.

Daaah namie mtoto wa mjini bana, nikaumiza kichwa nikaja kutumia mbinu za kibaharia akajikuta kapigwa karibu mara nne ya pesa nilomtumia mwanzo heheheee...

Alipogundua sasa ikawa msako bin msakuzi, hadi leo. Sema uzuri hanijui kwa sura.
 
Back
Top Bottom