Bacca Carlos, Kondakta wa basi na mvuvi aliyehamisha nyavu kutoka baharini kwenda uwanjani na kufanikiwa kuwa mshambuliaji bora

Bacca Carlos, Kondakta wa basi na mvuvi aliyehamisha nyavu kutoka baharini kwenda uwanjani na kufanikiwa kuwa mshambuliaji bora

Rahma Salum

Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
30
Reaction score
59
Carlos Bacca ni miongoni mwa wachezaji bora wa Amerika ya Kusini ambaye huwezi kushuku kipaji chake. Mara kadhaa amekuwa nguzo bora na muhimu kwa klabu aliyoitetea kushinda tuzo.

Msimamo mzuri wa Carlos Bacca umemuongoza kuwa na uwezo wa kutumia fursa kidogo ya kufanya maajabu katika dhamira yake. Nyuma ya kazi nzuri ya Carlos Bacca, kuna mapambano ya ajabu ambayo hupamba safari ya mafanikio yake.

Carlos Artuto Bacca Ahumada, amezaliwa Septemba 8, 1986 katika Kijiji kidogo cha Puerto, Colombia. Baba yake alikuwa mvuvi, na mama yake alimsaidia kuuza samaki.

Kukulia katika kijiji cha Puerto kulimfanya Bacca awe kijana jasiri sana, alizoea kuishi maisha ya utafutaji. Tangu akiwa mdogo alikuwa akimsaidia baba yake kuvua ili kuweza kusaidia kujikwamua kiuchumi yeye na familia yake.

Akiwa mdogo muda mwingine alikuwa anajaribu kuiba muda baada ya kutoka kuvua samaki na baba yake na kwenda kucheza mpira na wenzake. Baada ya wazazi wake kugundua mapenzi ya Bacca ya mpira walimpeleka katika shule inayofundisha mpira wa miguu.

Akiwa na umri wa miaka 8 Bacca rasmi alianza kupata mafunzo kutoka katika akademia ya ndani ya kijiji chao.
Bacca aliweza kuonesha nyota yake inayong’ara ndani ya muda mfupi katika akademia hiyo. Kutokana na hali duni ya maisha ilimuwia vigumu Bacca kuonesha kipaji chake nje ya Mji.

Kutokana na uhitaji wa fedha aliokua nao Bacca na familia yake alilazimika kutafuta chanzo kingine cha fedha, ndipo alipoamua kufanya kazi ya konda wa basi. Katika kipindi hichi Bacca alianza kukata tamaa na ndoto za kuwa mchezaji mpira.

‘’Katika umri wa miaka 20, niliishi katika kijiji cha Puerto Colombia nikifanya kazi ya kondakta wa basi. Maisha kipindi hicho hayakuwa ya urahisi. Nimetokea katika familia ya kimaskini na nilitakiwa kutafuta pesa ili kuwasaidia’’ Bacca

Mwaka 2006 Bacca alienda kufanya majaribio katika klabu ya Atlentico Junior, klabu ambayo ipo jirani na kijiji anachotokea yeye, panaitwa Barranquilla.

‘’Milango ya mpira ilifungwa kwangu katika kipind hicho, hicho kilikuwa kitu ambacho nilihitaji kufikiria tena. Lakini nilifanya majaribio kwa timu ya Junior Barranquilla na kwa bahati nzuri walinichagua’’ Bacca

Japo mwanzo ulikuwa mgumu kwake mara baaya ya kuchaguliwa katika timu hiyo, ndani ya misimu 3 Bacca aliweza kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa ligi, na kuisaidia timu kushinda ligi misimu 2.

Nyota yake ilizidi kung’ara zaidi na zaidi ndipo 2011 aliposajiliwa katika klabu ya Brugge ya Ubelgiji. Moja kwa moja alipewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo. Alipata changamoto ya kuonesha kipaji chake zaidi kutoka kwa mshambuliaji wa Nigeria, Joseph Akpala, ambaye alimkuta kinara katika klabu hiyo.

Baada ya Joseph Akpala kuhama klabu hiyo ilikuwa baraka kwa Bacca kwani aliweza kuwa chaguo la kwanza la kocha na kutengeneza magoli 18 ingawa mashindano yalikuwa yakizunguka nusu msimu tu.

Katika msimu wake wa pili akiwa Barani Ulaya, Bacca alishinda tuzo ya mchezaji bora na mfungaji bora wa ligi ya Ubelgiji. Ndipo Sevilla walipokiona kipaji cha mshambuliaji huyu mwenye ndoto kubwa.

2013 kwa ada ya uhamisho wa takribani euro milioni 7, Bacca rasmi akawa mchezaji anayekichapa katika moja ya ligi bora Duniani, Sevilla. Huko Sevilla, mafanikio yake hayakuweza kudhoofishwa. Alifanikiwa kukumbatia tuzo ya Europa League akishindana na mmoja wa wagombea tuzo wa La Liga.

Bacca akafanikiwa kuwa mshambuliaji muhimu zaidi kwa klabu yake pindi Sevilla iliposhinda dhidi ya Dnipro Dnipropetrovsk mwaka 2015 katika fainali ya UEFA ligi ya Ulaya, ambapo Savilla ilishinda kwa mabao 3-2, Bacca akifunga mabao 2 huku akisababisha goli la 3. Katika mechi hii Bacca alikuwa ndiye mchezaji aliyecheza vizuri zaidi.

Alisajiliwa na AC Milan 2018 kwa ada ya euro millioni 30 na kucheza kwa misimu miwili tu. Kwa sasa Bacca yupo Hispania akichezea klabu ya Villarreal.

20210327_171803.jpg
20210327_171819.jpg
 
Namkumbuka akiwa Sevilla alikuwa moto kweli, kitendo cha kutoka tu Sevilla ndio mpira wake ukapotea, nahisi kuna wachezaji wameumbwa kuchezea timu moja tu kama Messi, akijaribu kutoka kwenda kwingine ndio mwisho wake.
 
Ndio huyu aliwavuruga liverpool europa....ikiwa fainali ya kwanza kwa klopp
 
Dunia hii aijuaye kesho ya Mtu ni Mungu tu, unaweza sema kuna bahati kwa baadhi ya watu lakini si kweli bali Mungu alivyopanga juu yako iwe ndicho hutokea. Huyu mwamba kwa mazingira aliyozaliwa na kukulia kutoboa ilikuwa mtihani lakini juhudi zake na mapenzi ya Mungu yalipelekea kutoboa. Nilikuwa namkubali kazi yake
 
Alicheza vizuri ac milan akiwa mdungaji bora kwa ac milan ila figisu za carlos montella aliyekuwa kocha kipindi hicho akimweka benchi na kuwapa nafasi wachezaji wa kiitaliano zilitosha kumkimbiza, mpaka sasa ni Ibrahimovic pekee anayeweza kufikisha zaidi ya magoli 15
 
Back
Top Bottom