Bachelor of Science in Clinical Medicine, ufafanuzi

Ba Liz

Member
Joined
Aug 10, 2013
Posts
58
Reaction score
8
Jaman hivi kweli vyuo vya tanzania vitakua vinatoa bachelor of science in clinical medicine kwa ajili C.O. mwenye uelewa hili msaada tafadhali anisaidie na itachukua miaka mingapi?

Asanteni sana.
=================================
=================================

 
Poleni na hongereni kwa majukumu ya kujenga Taifa, leo asubuhi nimeingia kwenye website ya NACTE pmoja na mengi mapya niliyoyakuta kuna hili moja sijalieliwa vizuri.

Kuna hii kozi ya degree in clinical medicine ambayo imetangazwa kutolewa na chuo cha ST.JOSEPH ambayo itakuwa na ya miaka 4 na wanaotakiwa kuapply ni wale tu waliofanya diploma ya clinical medicine wenye GPA 2.7 na kuendelea.

Ninachoomba kujua ni je hii degree na ile ya Medicine ina tofauti gani? Na ni yupi anayesabika kuwa juu ya mwingine kati ya hao wawili?
 
Imechelewa sana kuja hiyo. Maana yake ni kwamba AMO inaishia na badala yake inakuja BCM.

Wakijamaliza kozi hiyo nakwambia watu hao watakuwa wakali sana kiutendaji (yaani wazuri sana) kwa kuwa wano uzoefu wa nenda rudi katika kazi na sasa wanasuguliwa upya kusukwa kitaaluma.

Mambo mengi sana anayofanya MD wanafanya watu hao kwa kujituma sana ila kikwazo chao elimu tu. Sasa kwa kuwa ukienda Muhimbili unasota miaka 5 mizima na internship juu, sasa hawa jamaa watakuwa one year less lakini full exposure to clinical medicine.

Kwa kifupi, Curriculum yao iko tofauti kidogo na ya MD kwa sababu hawa jamaa ni upgrading wakati MD sehemu kubwa ni kutoka form six moja kwa moja. CO ukijiunga na MD utasoma kwa taratibu za ki - MD lakini ukienda St Joseph na kwingineko kwenye BCM utafuata taratibu za kule.

Product hazipishani sana kwa sababu majina ya Degree yameweka utambulisho tofauti tu kati ya aliyesoma NACTE system na yule wa CTU (MD).

Huo ni ukombozi kwa walio wengi. Nadhani hata AMO anaweza kwenda BCM kama anataka atambuliwe kimataifa professionally, aweze kuserereka kwenda PhD.

Wapo walioanza na RMA wakapanda kwenda CO then AMO na kasha MD, Masters na PhD lakini kwa kusota usipime!!! Wengine ni maprofesa nawajua. Sasa mtiririko huu unamfanya Medical Assistant anayetaka kujiendeleza iwe rahisi kwake. Mtu mmoja mwenye ADO (sawa na AMO)anayetoka Kenya aliniambia aligomewa kutambuliwa na ADO yake alipokwenda Kenya ili akafanye kazi huko. Walimwambia lazima asome degree.

Sasa Kenya wanayo pia Bachelor of Medicine (BD) au BDS - Machelor of Dental Surgery) tofauti na Tanzania penye DDS na MD. Kwa maana hiyo waliofuzu watakuwa na uwezo wa kutambuliwa nje ya Tanzania hata hapa Afrika Mashariki.

Kuna nchi wanatoa Bachelor in Clinical Medicine (naomba nisitaje nchi kulinda utengamano wa EAC) lakini usiombe ukakutana na graduate wa degree hiyo wa nchi hiyo, utendaji wao ni chini kuliko wa RMA wa Tanzania.

Watanzania kitabu wanakisarandia sana lakini basi tu kwamba wakimaliza hawaenziwi kwa kupewa vifanyia kazi na wao kutunzwa vizuri. wakienda nje ya nchi kazi zao zinakubalika saaaaana! Nakwambia aiseee.

Asante kwa kuleta uzi huu. Watu wa NACTE inabidi waje hapa watupe ufafanuzi zaidi. Sikutaka ukae muda mrefu na dukuduku zito. I hope you are better now.
 
Thanks, Mkuu umeeleza kiuzuri na nimipata kitu, Tuzidi kuwasubiri wadau
 
Hii ni kama kusoma internal medicine .Mwanafunzi atabobea sana kwenye internal medicine lakini hataweza kusoma surgery kwenye masters kama angeamua hapo baadaye.
 
Hii ni kama kusoma internal medicine .Mwanafunzi atabobea sana kwenye internal medicine lakini hataweza kusoma surgery kwenye masters kama angeamua hapo baadaye.
fafanua zaidi mkuu,kwanini?
 
Hapo naona ni vigumu kusoma specialities za surgery.
 
Thanks, Mkuu umeeleza kiuzuri na nimipata kitu, Tuzidi kuwasubiri wadau

nineifuatilia sana sana ila hawataki kuitambua kama ni equivalent na MBBS au MD kwahiyo mtu akimaliza hii, anakuwa chini ya hawa waliomakiza kozi ya MD ambapo kiutendaji sioni tofauti .kwani MBBS sehemu nyingine ni miaka 4 tu. kwahy hii ni AMO ya ngazi ya degree. ukiritimba mkubwa.
 

Kwa jinsi ulivoeleza inaonyesha we Ni AMO na mmoja wa wakereketwa wa mfumo huo wa kupata MD hongera kwa sasa unaweza kupata MD/ BCM
 
Kwa jinsi ulivoeleza inaonyesha we Ni AMO na mmoja wa wakereketwa wa mfumo huo wa kupata MD hongera kwa sasa unaweza kupata MD/ BCM

Pole sana mkuu. Labda nailipokee la ukereketwa. Mimi sio AMO lakini nimepitia mfumo ambao haumruhusu mtu wa aina ya ADO kujitanua kwa kasi aitakayo. Kuliko kuendelea na misuguano kati ya AMO na MD kwa sababu tu vyeti vina majina tofauti ingawa performance zao saa nyingine zinachuana vikali sana, bora sasa AMO naye apewe nafasi ya kupata degree. Sio AMO tu, mchakato huu wa Bachelor degree utawahusu watu wote wanaosomea Advanced Diploma za NACTE, maana hakutakuwa na ADVANCED ambayo waingereza wanaisema ni equivalent to degree. Tunapochangia hapa hatumaanishi yanatuhusu moja kwa moja, lakini tunachangia uzoefu kwa kukutana na changamoto zitokanazo na mambo hayo tuchangiayo. Ungenitendea haki kama angalau ungesema naweza kuwa mwalimu wao. Hongera kwa kutumia uhuru wako wa kutoa mawazo yako ingawa kwa dharau. Nina hakika wewe au ndugu zako wamepitia mikononi mwa AMO na wndio maana wanaishi hata sasa kwa kuwa hao MD unaowaenzi hawako kilamahali.
 
naomba niulze kuna ukwel wwte juu ya bachelor ya clincal medcne tz tyr imeanza? na je ukimlza unkua na hadh gn? kzn yan i mean unkua km medical dr.(MD)? ama? na vyuo vngp tyr vmetngza kutoa hyo coz
 
nauliza jamani bachelor in clinical medicine kwa tanzania iko ready introduced? na inatolewa na vyuo gan guys?
 
nilikua nataka kujua kuhusu hii course mpya ya clinical medicine je ni vigezo vipi ili uweze kuisoma. vipi kuhusu ajira zake hapa nchini? mwenye uelewa naomba anieleweshe pleaseeeee
 
Hii mada imesha zungumuzwa sana humu,tafuta uzi huu.kwa ufupi tu ni kwamba kozi hii inachukua walio maliza diploma of clinical medicine au Advance diploma in clinical medicine,kozi hii imedhiniwa na wizara ya Afya na T.C.U,kutolewa na chuo kikuu cha St.Joseph university college of health and applied science kwa miaka minne
 
ok nimekupata bro kwa iyo inapatikana kwenye chuo kimoja tuu?
 
Mpaka march 2015...ilikuwa inatolewa na chuo hicho kwa sasa hivi sijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…