Jaman hivi kweli vyuo vya tanzania vitakua vinatoa bachelor of science in clinical medicine kwa ajili C.O. mwenye uelewa hili msaada tafadhali anisaidie na itachukua miaka mingapi?
Asanteni sana.
=================================
Asanteni sana.
=================================Poleni na hongereni kwa majukumu ya kujenga Taifa, leo asubuhi nimeingia kwenye website ya NACTE pmoja na mengi mapya niliyoyakuta kuna hili moja sijalieliwa vizuri.
Kuna hii kozi ya degree in clinical medicine ambayo imetangazwa kutolewa na chuo cha ST.JOSEPH ambayo itakuwa na ya miaka 4 na wanaotakiwa kuapply ni wale tu waliofanya diploma ya clinical medicine wenye GPA 2.7 na kuendelea.
Ninachoomba kujua ni je hii degree na ile ya Medicine ina tofauti gani? Na ni yupi anayesabika kuwa juu ya mwingine kati ya hao wawili?
=================================
Imechelewa sana kuja hiyo. Maana yake ni kwamba AMO inaishia na badala yake inakuja BCM.
Wakijamaliza kozi hiyo nakwambia watu hao watakuwa wakali sana kiutendaji (yaani wazuri sana) kwa kuwa wano uzoefu wa nenda rudi katika kazi na sasa wanasuguliwa upya kusukwa kitaaluma.
Mambo mengi sana anayofanya MD wanafanya watu hao kwa kujituma sana ila kikwazo chao elimu tu. Sasa kwa kuwa ukienda Muhimbili unasota miaka 5 mizima na internship juu, sasa hawa jamaa watakuwa one year less lakini full exposure to clinical medicine.
Kwa kifupi, Curriculum yao iko tofauti kidogo na ya MD kwa sababu hawa jamaa ni upgrading wakati MD sehemu kubwa ni kutoka form six moja kwa moja. CO ukijiunga na MD utasoma kwa taratibu za ki - MD lakini ukienda St Joseph na kwingineko kwenye BCM utafuata taratibu za kule.
Product hazipishani sana kwa sababu majina ya Degree yameweka utambulisho tofauti tu kati ya aliyesoma NACTE system na yule wa CTU (MD).
Huo ni ukombozi kwa walio wengi. Nadhani hata AMO anaweza kwenda BCM kama anataka atambuliwe kimataifa professionally, aweze kuserereka kwenda PhD.
Wapo walioanza na RMA wakapanda kwenda CO then AMO na kasha MD, Masters na PhD lakini kwa kusota usipime!!! Wengine ni maprofesa nawajua. Sasa mtiririko huu unamfanya Medical Assistant anayetaka kujiendeleza iwe rahisi kwake. Mtu mmoja mwenye ADO (sawa na AMO)anayetoka Kenya aliniambia aligomewa kutambuliwa na ADO yake alipokwenda Kenya ili akafanye kazi huko. Walimwambia lazima asome degree.
Sasa Kenya wanayo pia Bachelor of Medicine (BD) au BDS - Machelor of Dental Surgery) tofauti na Tanzania penye DDS na MD. Kwa maana hiyo waliofuzu watakuwa na uwezo wa kutambuliwa nje ya Tanzania hata hapa Afrika Mashariki.
Kuna nchi wanatoa Bachelor in Clinical Medicine (naomba nisitaje nchi kulinda utengamano wa EAC) lakini usiombe ukakutana na graduate wa degree hiyo wa nchi hiyo, utendaji wao ni chini kuliko wa RMA wa Tanzania.
Watanzania kitabu wanakisarandia sana lakini basi tu kwamba wakimaliza hawaenziwi kwa kupewa vifanyia kazi na wao kutunzwa vizuri. wakienda nje ya nchi kazi zao zinakubalika saaaaana! Nakwambia aiseee.
Asante kwa kuleta uzi huu. Watu wa NACTE inabidi waje hapa watupe ufafanuzi zaidi. Sikutaka ukae muda mrefu na dukuduku zito. I hope you are better now.